Watanzania Wengi Wana Chuki, Wivu na Husda

Watanzania Wengi Wana Chuki, Wivu na Husda

Shida za maisha tutazitatua 😊
Tupige kazi

Naunga mkono hoja
Watu Tanzania wanafanya kazi sana ila bado ni masikini wanaoishi kwa kipato cha hand to mouth, hawana bima za afya, watoto wao wanasoma shule mbovu, miondombinu mibovu halafu serikali inatumia pesa kwenye mambo ya hovyo kama kugawa kwa hao wasanii ili wawe machawa wao kuwasifia. Hapo ndipo chuki inapoanzia.
 
Watu Tanzania wanafanya kazi sana ila bado ni masikini wanaoishi kwa kipato cha hand to mouth, hawana bima za afya, watoto wao wanasoma shule mbovu, miondombinu mibovu halafu serikali inatumia pesa kwenye mambo ya hovyo kama kugawa kwa hao wasanii ili wawe machawa wao kuwasifia. Hapo ndipo chuki inapoanzia.
Chuki nayo muda mwingine ni kujiendekeza tu

Kuna watu wapo vizuri ki uchumi na bado wanabeba chuki
 
Hao wanaokebehi hayo manunuzi ni wangapi kama Una idadi yao?Hizo generalisations ndiyo zilifanya watu wakaua wasio na hatia wengi tarehe 29/10-03/11/2025.Unawaonea Watanganyika kwa watu(konzi ya mkono)kiduchu,tena wapo DSM mitandaoni.
Na Mimi pia namuunga mkono mtoa mada. Zimetamalaki sana chuki, wivu na husda. Unaweza ukaona jinsi watu (wachache lakini) humu mitandaoni wanavyojitahidi kumchukia mama Samia (The Mother of Modern Tanzania). Walifikia (walivyo wajinga na wapumbavu) Hadi hatua ya kutaka kufanya mapinduzi okt 29; shukrani nyingi na za kipekee ziende kwa vyombo vyetu vya ulinzi na wananchi wazalendo waliowazuilia mbali kufikia hatima yao hiyo ovu ya kuliangamiza taifa.
 
Nakumbuka miaka michache nyuma kuna msanii maarufu alinunua Rolls Royce. Kwa kweli mitandao ilichafuka kwa kebehi,kashfa na maneno mengi yenye mlengo hasi. Mara used, mara bei kaongeza sifurimara sio lake,mara matairi vipara basi tu ili mradi watu waliojaa sumu mwilini wazitoe na wamshushe.

Sasa hivi karibuni mke wa huyu msanii kanunua Bentley, yaani maneno yale yale yamerudi. Mara used, bei yake sio ile ni hii yaani ni tafrani ili mradi tu kumshusha. Wengine wanaenda mbali zaidi kuingia mitandaoni kutafuta gari kama hio iliogongwa au kuwa scrapped huko ughaibuni na kusema ndio bei za haya magari.

Kwanini watu wanakuwa na roho za namna hii? Hata humu JF mtu akipost kitu chake gari au nyumba watakuja watu na kuanza kumkashifu kwa maneno ya kejeli na dhihaka. kwanini lakini? Yaani watu wako busy na mitandao mwezi mzima kujadili gari ya mtu kuwa bei ni ndogo sana,mara used sasa hata ikiwa used wewe unapungukiwa nini? Au kama inauzwa 10m yeye kasema 100m wewe unapungukiwa nini?
Yote haya ni sababu ya umasikini ambao umelaaniwa mpaka kwenye vitabu vya dini🙌🙌🙌🙌🙌

Mimi ni mmoja wa ninaoulaani umasikini
 
Ni wivu wa kijinga. Kama mambo ni rahisi hivyo, kwa nini na wewe usinunue alafu uongeze hiyo sifuri? Binafsi, mimi navutiwa na watu wanaopiga hatua kwenye maisha kwa sababu wananipa motisha ya kupambana Zaidi.
Mtu inatakiwa upate moyo na wewe uinuke.
 
Back
Top Bottom