Watanzania Wengi Wana Chuki, Wivu na Husda

Watanzania Wengi Wana Chuki, Wivu na Husda

Siwezi kuwashangaa hao wanaoponda; kwa sababu, kwa mtazamo wao, wapo sahihi kabisa. Maana Umaskini, wivu na chuki mara nyingi uenda sambamba.

Ni sawa na wewe kuanza kumshangaa kichaa kwa matendo yake, wakati unajua kabisa kuwa huyo ni kichaa!
 
UNGEJIULIZA SWALI LA KIMANTIKI NI, KWANINI UPOST MAISHA YAKO KUYAFANYA PUBLIC ALAFU UCHAGUE KUTAKA KUSIFIWA TU!!!

KENGE WAHED,,,,GADDEMITT!!!!


HAO WASANII UCHWARA WANASEEK ATTENTION AND VALIDATION.MSANII KUNUNUA GARI LA GARAMA NA KISHA KULIPOST INASAIDIA NINI MASKINI MILLIONI 61 WALIOBAKI NCHI AMBAYO KULA MILO MITATU NI ANASA!!!

WACHA APOPOLEWE MAANA NI UKWELI ULIO WAZI KUWA HAWANA PESA KAMA WANAVYOJINADI ILA NI MWENDO WA KUFAKE TU.

HAO WASANII UCHWARA,HAWANA PESA BALI NI WATAKATISHAJI WA PESA NA BIASHARA HARAMU HAKUNA MZIKI WALA NINI.

KUNA MWINGINE KILA SIKU MIPICHA YUPO IBIZA MARA YUPO VIWANJA VIKALI ANATAKULA BATA ILA KAZI ANAZOFANYA HAZIJULIKANI. ANAKAZI YA KUNUNUA GARI ZA GHARAMA ALAFU HANA PESA YA KUSAJILI.

😀😀😀WACHA WAPOPOLEWE HAWANA MCHANGO WOWOTE KATIKA NCHI HII ZAIDI YA KUTUKUZA NGONO ZEMBE NA TABIA ZA KIMALAYAMALAYA NA USHOGA!!!
Ok.
 
Hiyo hali ipo hata humu JF,
Mtu akianzisha uzi kua maisha yamempiga,basi atapewa pole,ataambiwa pambana utatoka tu,usikate tamaa,watampa kila neno la faraja,
Ila mtu akileta uzi kua ana maisha mazuri,atapigwa vita,hama hapo kwa shemeji yako,amka kumekucha utajikojolea...

Watu wa aina hii ni watu waliojikatia tamaa ya maisha,akisikia mtu ana dhiki basi anakua anafarijika sana kwa kuona kua kumbe wapo na wengine wana dhiki kama yeye.
Inasikitisha sana.
 
Hoja si uwezo wa kununua, bali mantiki ya matumizi katika mazingira yetu. Hivi: kuvaa mfano mink coat(vazi la bei mbaya) Joto la Dar es saalam inaingia akilini?
Mantiki ya matumizi? Kwa hiyo Bentley au Rolls Royce haitembei hapa Tanzania?
Hio habari ya coat na joto sio Dar tu hata huko yanapotengenezwa huwezi kuvaa summer time. Haya niambie Bentley kuna sehemu wamesema gari yao haiwezi kutumika nchi kama Tz?
 
Mda mwingne unatakiwa ujifunze kabla ya kuraumu au kutukana watu
Ni ivi watu wanakupokea vile umekuja

Alikua na uwezo wa kununua na kunyamaza adi tuione akiendesha ila kitendo cha kupost mtandaoni na kuongea maneno meng bas watu nao wakatoka maoni yao so sizan kama ni roho mbaya ila ni amepokelewa kama alivyokuja
Sasa kanunua kwa hela zake,kapost kwenye ukurasa wake mtandaoni sio kwamba alienda nalo vibarazani kwa watu kuwaringishia
Tatizo nini?
 
Acha hiyo, kuna ile mtu mpo nae ofisi moja, cheo kimoja, mshahara mnafanana. Lakini anakupiga vita, majungu, wivu na chuki. 😊

Unabaki unashangaa! Maana hakuna kitu umemzidi, sio cheo wala mshahara, ila anakuchukia tuu na kukuonea wivu.

Wabongo miyeyusho sana aisee.
Kazi ipo
 
Hakuna mtu asiye kua na chuki lakini chuki ya kuchukua mwenzio au kumfuatilia mwenzio hapo uongo, mimi pia ninachuki lakini nachukia sana uminywaji wa haki hapo Tanzania, yaani roho inaniuma sana kuona watanzania hawana raha katika nchi yao mimi hata mtu atembelee semi trela mimi nitampongeza

nina marafiki matajiri na sijali hata kidogo na sitakaa nijali maendeleo au vitu visivyonihusu, lakini dhulma inanitesa sana tunayofanyiwa na viongozi huko ndio chuki ilipo na watanzania tusioneane wivu sisi kwa sisi wabaya ni wake wanatufanyia dhulma sio sisi.
 
Kule mjini ticktock kuna watu wanafanya content majumbani kwao vijijini wanao nesha wanavyopika na kuni na mambo kama hayo, kuna watu huwa wanacomment hizi ndio content zenye uhalisia, Unajiuliza huyu hata maana ya uhalisia anaijua kweli? Maana yake wanaofanya content makwao kwenye mijengo ya migorofa content zao hazina uhalisia 😂

Kuna mchanganyiko wa ujinga na umasikini 🤣
Mambo ya vijiji vya ujamaa, taifa la wakulima na wafanyakazi. Matajiri wakubwa na wafanyabiashara ni wezi, wanyonyaji etc

Unajua silaumu sana kwa sababu hata mimi zamani nilikuwa na hiyo mindset kwa kukosa EXPOSURE kiasi lakini pia kutaka kukubalika kwenye sections flani

Si unajua bongo mtu kuitwa wa kishua au soft life ni kama dhihaka ila ukiitwa mpambanaji, building from scratch ,furaha yetu si pesa ndio unaonekana YES, kwa hiyo wakishua inabidi afanye content flani ili aonekane hafedheheshwi na umaskini

Japo deep down umaskini unabonda na kunyonga. Kwa sasa acha nipambane, staki nifike 40 sijaonja vacation au kujispoil tu vile tamaa zangu zinataka 😁😁😁
 
Ukipost shida na matatizo utapata maneno kibao ya faraja na kujibiwa kwa bashasha
Ndio maana wanaofake shida wanapata michango ya chapchap

Japo hizi ni PR tu, hata uswahilini wanapoishi maskini bado wenye unafuu wa maisha wanathaminiwa zaidi hata kama wanapigwa vita pia kwa wivu na roho mbaya. Au jamii kumlazimisha mtu aishi lifestyle yao hata kama hajaizoea

Ndio maana huwa nasema, kama una unafuu wa kipato usijenge uswahilini. Ipo siku utajuta
 
Nakumbuka miaka michache nyuma kuna msanii maarufu alinunua Rolls Royce. Kwa kweli mitandao ilichafuka kwa kebehi,kashfa na maneno mengi yenye mlengo hasi. Mara used, mara bei kaongeza sifurimara sio lake,mara matairi vipara basi tu ili mradi watu waliojaa sumu mwilini wazitoe na wamshushe.

Sasa hivi karibuni mke wa huyu msanii kanunua Bentley, yaani maneno yale yale yamerudi. Mara used, bei yake sio ile ni hii yaani ni tafrani ili mradi tu kumshusha. Wengine wanaenda mbali zaidi kuingia mitandaoni kutafuta gari kama hio iliogongwa au kuwa scrapped huko ughaibuni na kusema ndio bei za haya magari.

Kwanini watu wanakuwa na roho za namna hii? Hata humu JF mtu akipost kitu chake gari au nyumba watakuja watu na kuanza kumkashifu kwa maneno ya kejeli na dhihaka. kwanini lakini? Yaani watu wako busy na mitandao mwezi mzima kujadili gari ya mtu kuwa bei ni ndogo sana,mara used sasa hata ikiwa used wewe unapungukiwa nini? Au kama inauzwa 10m yeye kasema 100m wewe unapungukiwa nini?
Hiyo hata huku mtaani watu wana husda sana
 
Back
Top Bottom