Usafishaji wa miji na majiji ilitakiwa iwe kazi ya manispaa husika.
Kwa sababu kodi zinalipwa na Halmashauri zinakusanya ushauri kwa namna zao.
Halafu bila aibu zinaletwa tozo za taka ambazo hizo taka hazizolewi kwa wakati.
Hii nchi Kuna vitu vingi haviko sawa.
Manispaa ya Moshi wakati ule walijitahidi kuweka dustbin za uchafu nadhani Kila baada ya mita 15 au 20.
Unanunua kitu, sehemu ya kutupa unaiona na usipo fanya hivyo wanakukamata ukalipie huko 50,000.
Sasa dar ina hiyo miundombinu iliyowekwa mahususi ili iweze kukidhi, kabla ya kuanza kukamata na kutoa adhabu?