Watanzania, Msichaguwe Chama Chagueni Kiongozi

Nyerere, dr slaa, kikwete, uislaam hayo ndo maneno pekee ninayoyaona yakiandikwa na kilaza FF

Soma post namba moja halafu nioneshe hayo uyasemayo. Ukishindwa ujuwe kuwe ni fataani. Unajuwa maana ya fataani?
 
nilini umeona hayo?siku zote ulikuwa wapi?au kwasababu tu kundi lako lipo taaban?anyway umenena vema tuko pamoja
 
Wazo zuri sana. Vipi wakichakachua kura? Vipi wakiwaapisha wawapendao wao wenye chama dola?
Wazo zuri? HILI NI WAZO MFU!!!
Hakuna mgombea huru Tanzania. Kila mgombea anabebeshwa ilani ya Chama chake.
Mantiki ya kuchagua mtu kwa kutolea mifano ya Shibuda na Jakaya haina mashiko.
Katiba Mpya imeuawa na hao watangaza nia wa CCM wakati wa Bunge la Katiba.
Kama umesahau, Chama kiliwaweka "jela" wataka Urais.
Vyama ndivyo vinavyoweka wagombea, si vinginevyo.
Vinavyochaguliwa ni vyama.
 
Soma post namba moja halafu nioneshe hayo uyasemayo. Ukishindwa ujuwe kuwe ni fataani. Unajuwa maana ya fataani?

Hakuna chama ni taasisi na ccm imeamua kuwa taasisi ya mafisadi hata akishushwa malaika lazima afuate sheria za taasisi ya chama alichopo kuku kuku tu jogoo jina.
 
Upo huru na mawazo yako na wengine pia tupo huru na mawazo yetu. Hapa kwenye mada siongelei chama, nnaongelea tutakaowachaguwa.

Punguani wahed.
 
Mfano hai ni mwaka 1995 wakati Kikwete alipowania kuwa Rais kwa mara ya kwanza, hakuna asiyejuwa kuwa alishinda ndani ya chama lakini wenye chama hawakutaka, matokeo unayajuwa.

bora alivovyokatwa 1995 mana tumeshuhudia sasa asivofaa kuwa hata katibu tarafa
 
Yanini unaandikia mate na wino upo? porojo zako hazisaidii kitu, tulimnganishe na Rais yeyote wa Tanzania umpendae wa kabla yake katika mambo kumi ya Kitaifa na ukipeda Kimataifa vile vile, au kukurahisishia wachanganye Marais wote wa kabla yake kwa pamoja tulinganishe na Kikwete peke yake, katika nyanja zote.

1) Elimu.

Kikwete
shule za sekondari wakati wake zaidi ya 4600.

Vyuo vikuu zaidi ya 50.

Vyuo vya ufundi?

Vyuo vya waalimu?

Vyuo vya Udaktari?

vyuo vya kijeshi?

Tuanze hilo moja, unasemaje?
 
Wakati tunaingia kwenye mwaka wa heka heka za uchaguzi wa Wabunge na wa Rais.

Nawaasa Watanzania wasichaguwe chama bali wachaguwe kiongozi.

Mfano mzuri ni kama tuliouonesha mwaka 2005, wakati tulipomchaguwa Kikwete kuwa kiongozi mkuu wa nchi hii. Ushindi alioupata Kikwete wa zaidi ya kura 80% ni dhahiri ulikuwa si kwa kuchaguliwa na wana CCM bali hata wa upinzani na wasio na vyama.

Mfano mwingine ni wa John Shibuda, pale alipoihama CCM na kuhamia Chadema, wana CCM wa jimbo lake wengi walimpa kura zao bila kujali yupo chama kipi. Huo ni uzalendo na unaonesha jinsi Tanzania tunavyoweza kufanya maamuzi bila ya kuburuzwa na chama au wenye chama.

Viongozi wazuri tunao, tena tusingoje wale wanaojitokeza tu kuzitaka hizi nyadhifa kwa udi na uvumba. Tutazame katika jamii, tunapomuona anaefaa kuongoza, hata kama si mwanasiasa, bali tukimuona kuwa haa huyu anafaa kuongoza, tumlazimishe, tumsimamishe, tumchaguwe.

Tukianza kuchaguwa viongozi na si chama tutakuwa sisi wenyewe tumeshakuwa viongozi.Tuanze kwa kujiongoza wenyewe kwa kuchaguwa tukitakacho na si kuburuzwa na wakitakacho wenye vyama.

Tukianza hivyo, hata vyama vyetu vitaweka viongozi tuwatakao na si wawatakao wenye vyama.

Nasema haya kwa kuwa nimeona katika vyama vyetu vya siasa vyote, kuna tabia ya kura za maoni. Wananchi wanaweza kuwa na mgombea wao wakampendekeza agombee lakini ikifika kwenye vyama wanakatwa na kuwekwa wale wawatakao wenye vyama. Hii si demokrasia tuitakayo na huleta uvunjifu wa amani.

Ni wakati muafaka sasa Watanzania tusikubali kuchaguwa wamtakae wenye vyama, tunataka tuwe na viongozi tuwatakao wananchi tulio wengi. Tunataka na wagombea huru, wasio na vyama pia wawepo, ili tuwachaguwe tuwaonao wanatufaa na si wanaowafaa wenye vyama.

Naona Fox leo umenena vema kwa mara ya kwanza!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Siyo leo hiyo ni ya zamani, tazama tarehe niliyoiweka.

Huwa hunisomi tu. Ukinisoma kwa utuvu utanielewa tu.
 
Safi sana siku nyingine unakuwa na point nzuri sana dada mwenyezi Mungu akupe Baraka ubaki na busara zako ulizokuwa nazo leo usibadilike sawa.
 
Hivi, Shibuda ni mfano wa kutoa kwa uongozi uliotukuka? Bi Mkubwa? naomba jibu kwa heshima na taadhima
 
Wakati tunaingia kwenye mwaka wa heka heka za uchaguzi wa Wabunge na wa Rais.

Nawaasa Watanzania wasichaguwe chama bali wachaguwe kiongozi.

Mfano mzuri ni kama tuliouonesha mwaka 2005, wakati tulipomchaguwa Kikwete kuwa kiongozi mkuu wa nchi hii. Ushindi alioupata Kikwete wa zaidi ya kura 80% ni dhahiri ulikuwa si kwa kuchaguliwa na wana CCM bali hata wa upinzani na wasio na vyama.

Mfano mwingine ni wa John Shibuda, pale alipoihama CCM na kuhamia Chadema, wana CCM wa jimbo lake wengi walimpa kura zao bila kujali yupo chama kipi. Huo ni uzalendo na unaonesha jinsi Tanzania tunavyoweza kufanya maamuzi bila ya kuburuzwa na chama au wenye chama.

Viongozi wazuri tunao, tena tusingoje wale wanaojitokeza tu kuzitaka hizi nyadhifa kwa udi na uvumba. Tutazame katika jamii, tunapomuona anaefaa kuongoza, hata kama si mwanasiasa, bali tukimuona kuwa haa huyu anafaa kuongoza, tumlazimishe, tumsimamishe, tumchaguwe.

Tukianza kuchaguwa viongozi na si chama tutakuwa sisi wenyewe tumeshakuwa viongozi.Tuanze kwa kujiongoza wenyewe kwa kuchaguwa tukitakacho na si kuburuzwa na wakitakacho wenye vyama.

Tukianza hivyo, hata vyama vyetu vitaweka viongozi tuwatakao na si wawatakao wenye vyama.

Nasema haya kwa kuwa nimeona katika vyama vyetu vya siasa vyote, kuna tabia ya kura za maoni. Wananchi wanaweza kuwa na mgombea wao wakampendekeza agombee lakini ikifika kwenye vyama wanakatwa na kuwekwa wale wawatakao wenye vyama. Hii si demokrasia tuitakayo na huleta uvunjifu wa amani.

Ni wakati muafaka sasa Watanzania tusikubali kuchaguwa wamtakae wenye vyama, tunataka tuwe na viongozi tuwatakao wananchi tulio wengi. Tunataka na wagombea huru, wasio na vyama pia wawepo, ili tuwachaguwe tuwaonao wanatufaa na si wanaowafaa wenye vyama.
leo natamani tuwe na undugu, nataman tukumbatiane hata kwa dakika tatu, umetema madini
 
Nyerere aliona mbali. Sasa hebu muulize Kikwete "Alikuwa wapi wakati nchi inachukuliwa Vibaka?"

Sahihi yangu inajitosheleza sana. Makongoro kwa hili KAKANDAMIZA haswa.

Mfano hai ni mwaka 1995 wakati Kikwete alipowania kuwa Rais kwa mara ya kwanza, hakuna asiyejuwa kuwa alishinda ndani ya chama lakini wenye chama hawakutaka, matokeo unayajuwa.
 
Hivi, Shibuda ni mfano wa kutoa kwa uongozi uliotukuka? Bi Mkubwa? naomba jibu kwa heshima na taadhima

muelewe mleta uzi anajaribu kuonesha namna ya kumpata mshindi bila kujali chama.
amezungumzia namna walivyochaguliwa bila kujali nini walichokifanya baada ya kuchaguliwa

ni ukweli tuache uchama kwenye nafasi hasa ya urais
 
Back
Top Bottom