Tumefikaje hapa tulipo?

Tumefikaje hapa tulipo?

Mkandara

Platinum Member
Joined
Mar 3, 2006
Posts
16,024
Reaction score
9,512
Leo hii nimechukua zaidi ya masaa manne kuwasikiliza viongozi wastaafu, maprofesa na wadau mbali mbali katika mdahalo uloandaliwa na TLS.

Hakika nimejifunza mengi na yanilazimu kuwashukuru sana Mzee wetu Jaji Warioba, Profesa Shivji, Mwanasheria kutoka Kenya, Profesa Tibaijika, viongozi wa vyama vya Siasa na taasisi nyinginezo hususani TLS wenyewe. Wote kwa ujumla wao wamezungumzia mambo muhimu kwa mustakabali wa Taifa letu.

Pamoja na yote yale wameniachia maswali magumu zaidi nimekaa na kujiuliza hivi tatizo hasa lipo wapi? Na tumefika hapa kwa sababu gani?

Kubwa zaidi lilojitokeza kwangu linatokana na hotuba ya Profesa Shivji alipozungumzia Misingi mikuu ya Demokrasia akifafanua juu ya pande mbili yaani upande Wananchi na upande wa Utawala. Na kilichojitokeza wazi kwangu ni Kupotea thamani na heshima ya UTU wetu. UTU ndio kiashiria cha ujenzi na usimamizi wa Uhuru na Usalama.

Taifa letu limepoteza UTU kiasi kwamba Utawala hauthamini wala kuheshimu Wananchi na Wananchi hawawathamini wala kuheshimu Viongozi wake. Haiishi hapo, tumefikia kiasi kwamba Utawala hauheshimu viongozi wenzao na Wananchi hawathamini wala kuheshimu Wananchi wenzao.

Na katika hali hii, Uhuru na Usalama wa wananchi upo hatarini kama ilivyo kwa viongozi wenyewe hawaaminiani wala hawaheshimiani isipokuwa kwa yule mwenye nguvu ya utawala na fedha, hii ndio Tanzania ya leo (status quo)

Swali linakuja tumefikaje hapa? Naamini kila mtu ana mtazamo wake lakini binafsi yangu akili yangu inanambia yote haya yametokana utovu wa nidhamu katika miiko na maadili ya UTU wetu kwa kuiga mifumo ya kigeni ambayo ilidhalilisha mila na tamaduni zetu kama ni misingi ya kale (primitive) ilopitwa na wakati.

Mifumo ya Demokrasia tuloichukua ndio chanzo cha kuharibika kwa misingi ya Demokrasia kupitia mabadiliko ya Katiba ya mwaka 1984 na 1992 upande wa Jamhuri pia Uandishi wa Katiba ya Zanzibar mwaka 1984 na mabadiliko yalofuatia mwaka 2002. Isipokuwa nitaacha pembeni Katiba ya Zanzibar, hii inahitaji mada nyingine tofauti kabisa.

Najua hoja yangu inahitaji mjadala mpana zaidi lakini niseme kwamba mabadiliko haya ndio mwanzo wa matatizo yote yanayofuatia katika miongo tofauti ya Kiutawala kufikia leo hii.

Katika makosa makubwa yalofanyika ni kuondolewa kwa Miiko na Maadili ya Viongozi hivyo kupoteza Sifa zinazotakiwa za viongozi wetu Kitaifa. Kwa nafasi walizokuwa nazo viongozi serikalini, Wabunge na hata majaji wakaanza kumiliki utajiri pasi kuulizwa wamepataje mali na utajiri huo, hii njia panda ndio ikawa mwanzo wa mmomonyoko wa maadili na chachu ya rushwa kuzaliwa.

Jambo la pili lilikuwa ujio mfumo wa Vyama Vingi ambavyo havikuzingatia misingi ya Demokrasia ( Uhuru, Utu na Usalama) bali ilikuwa ni tiketi ya jicho la Uheshimiwa na kuingia Ikulu kutawala (mfumo wa Vyama vingi). Vyama vingi ndivyo viloweka nadharia ya kina nani watakuwa Waheshimiwa kati ya Wananchi wote na hii ikazaa tamaa ya utukufu wa nyadhifa hizo. Hakuna Chama hata kimoja kinachosimamia itikadi na Sera zake wakati wote ila kulingana na fursa zinazojitokeza.

Katika mukhtadha huo tulipoteza Siasa safi za vyama Kiitakadi, hasada ikachukua nafasi baina ya vyama vya Siasa, viongozi kwa viongozi, Wananchi na vyama pinzani na kibaya zaidi rushwa na upendeleo vikatumiwa kama zana katika teuzi toka chaguzi za ndani ya Vyama vya Kisiasa hadi Viongozi wa Kitaifa – Yakaibuka makundi ya timu za Wana, hasada ikazaa Chuki na Uadui matokeo yake UZALENDO kwa Taifa letu UKAPUKUTIKA.

Kwa hiyo tukiacha hoja ya Katiba Mpya pembeni, sisi Watanzania tuna wivu na chuki za kuhasimiana wenyewe kwa sababu ya fursa za madaraka na utajiri zimeletwa kupitia vyama vingi.

Viongozi waliopo madarakani hujiona wapo katika nafasi adimu sana ya Utajiri wa hadhi na mali na wanajua kuna macho ya wivu dhidi yao hata kama wanayofanya nia njema ama kinyume cha misingi ya demokrasia, bado utachikiwa tu. Siasa zetu zimekuwa ni za Ukinzani ambazo kiitikadi hazifanani kabisa na Upinzani kwa nia, dhamira na malengo ya Demokrasia.

Tujiulize wenyewe mpaka hapa tumefika ni viongozi wangapi wameuawa kwa ajali, risasi au sumu na hakuna watu walotiwa hatiani wala kuchukuliwa hatua. Nini hasa sababu za viongozi hao kuuawa? Bila shaka ni kunatokana na UADUI wa kisiasa walojenga dhidi ya kiongozi ama viongozi wengine iwe kwa nia safi au mbaya.

Wivu na Chuki sii lazima vitumike kwa wale washindani tu bali inaweza toka chini kwa wale wanaotaka kufika pale kiongozi alipofika ama kiongozi kulinda maslahi yake dhidi ya wale wanaotaka nafasi yake.

Kwa hiyo tunapozungumzia leo Maombolezi, Maridhiano na sijui Katiba Mpya ni muhimu kwanza sisi wenyewe tukubali mapungufu yetu kimaadili ili TUBADILIKE - Heshima ya Utu wetu na Uzalendo kwa Taifa ni utamaduni ulopitwa na wakati.

Hatuwezi fanya maombolezi ambayo baadhi yetu hawaoni umuhimu wala sababu. Hatuwezi fanya Maridhiano kwa kuwekeana masharti yasiyojali Utu wetu na Uzalendo kwa Taifa hili bali maslahi ya mtu au chama.

Mwisho hatuwezi kuwa na Katiba mpya inayotokana na maoni ya Wananchi wenye wivu, chuki na uadui isipokuwa Katiba lazima iwe ni mwongozo wa Wananchi hao bila kujali tofauti zao - Katiba ni ya Wananchi iheshimiwe na wote.

Maasalaam
 
Naunga mkono hoja.
P
 
..sasa nenda kasikilize interview ya Mzee Butiku alipohojiwa ktk podcast ya Salma na Mjenga ndipo utajua tumefika pabaya.

..tumevuka huko kwenye miiko ya uongozi, sasa hivi tuna tatizo la wana Ccm wanaomwaga DAMU za wapinzani.

..tunahitaji Katiba Mpya bora kwa sasa. Mambo mengine yote tutashughulika nayo tukiwa na Katiba mpya na bora.

..Hata MISAHAFU si ipo pamoja na watu kutenda maovu? Je, tulipaswa kusubiri wanadamu waache dhambi ndipo misahafu iteremshwe?

..KATIBA MPYA NI SASA.
 
Mjomba ulichoshauri hapo mwishoni hakitekelezeki. Mimi natamani kuona muungano unavunjika ili na sisi Watanganyika tujivunie uwepo wa nchi yetu ya Tanganyika, kama wafanyavyo Wazanzibari kwa Zanzibar yao. Kwa kufanya hivi nchi yetu haitokuja kutawaliwa tena na vilaza, mafisadi, wahuni, au watu wasio na chembe ya uzalendo.
 
Leo hii nimechukua zaidi ya masaa manne kuwasikiliza viongozi wastaafu, maprofesa na wadau mbali mbali katika mdahalo uloandaliwa na TLS.

Hakika nimejifunza mengi na yanilazimu kuwashukuru sana Mzee wetu Jaji Warioba, Profesa Shivji, Mwanasheria kutoka Kenya, Profesa Tibaijika, viongozi wa vyama vya Siasa na taasisi nyinginezo hususani TLS wenyewe. Wote kwa ujumla wao wamezungumzia mambo muhimu kwa mustakabali wa Taifa letu.

Pamoja na yote yale wameniachia maswali magumu zaidi nimekaa na kujiuliza hivi tatizo hasa lipo wapi? Na tumefika hapa kwa sababu gani?

Kubwa zaidi lilojitokeza kwangu linatokana na hotuba ya Profesa Shivji alipozungumzia Misingi mikuu ya Demokrasia akifafanua juu ya pande mbili yaani upande Wananchi na upande wa Utawala. Na kilichojitokeza wazi kwangu ni Kupotea thamani na heshima ya UTU wetu. UTU ndio kiashiria cha ujenzi na usimamizi wa Uhuru na Usalama.

Taifa letu limepoteza UTU kiasi kwamba Utawala hauthamini wala kuheshimu Wananchi na Wananchi hawawathamini wala kuheshimu Viongozi wake. Haiishi hapo, tumefikia kiasi kwamba Utawala hauheshimu viongozi wenzao na Wananchi hawathamini wala kuheshimu Wananchi wenzao.

Na katika hali hii, Uhuru na Usalama wa wananchi upo hatarini kama ilivyo kwa viongozi wenyewe hawaaminiani wala hawaheshimiani isipokuwa kwa yule mwenye nguvu ya utawala na fedha, hii ndio Tanzania ya leo (status quo)

Swali linakuja tumefikaje hapa? Naamini kila mtu ana mtazamo wake lakini binafsi yangu akili yangu inanambia yote haya yametokana utovu wa nidhamu katika miiko na maadili ya UTU wetu kwa kuiga mifumo ya kigeni ambayo ilidhalilisha mila na tamaduni zetu kama ni misingi ya kale (primitive) ilopitwa na wakati.

Mifumo ya Demokrasia tuloichukua ndio chanzo cha kuharibika kwa misingi ya Demokrasia kupitia mabadiliko ya Katiba ya mwaka 1984 na 1992 upande wa Jamhuri pia Uandishi wa Katiba ya Zanzibar mwaka 1984 na mabadiliko yalofuatia mwaka 2002. Isipokiwa nitaacha pembeni Katiba ya Zanzibar, hii inahitaji mada nyingine tofauti kabisa.

Najua hoja yangu inahitaji mjadala mpana zaidi lakini niseme kwamba mabadiliko haya ndio mwanzo wa matatizo yote yanayofuatia katika miongo tofauti ya Kiutawala kufikia leo hii.

Katika makosa makubwa yalofanyika ni kuondolewa kwa Miiko na Maadili ya Viongozi hivyo kupoteza Sifa zinazotakiwa za viongozi Kitaifa. Kwa nafasi walizokuwa nazo viongozi serikalini, Wabunge na hata majaji wakaanza kumiliki utajiri pasi kuulizwa wamepataje mali na utajiri huo, hii njia panda ndio ikawa mwwnzo wa mmomonyoko wa maadili na chachu ya rushwa kuzaliwa.

Jambo la pili lilikuwa ujio mfumo wa Vyama Vingi ambavyo havikuzingatia misingi ya Demokrasia ( Uhuru, Utu na Usalama) bali ilikuwa ni tiketi ya jicho la Uheshimiwa na kuingia Ikulu kutawala (mfumo wa Vyama vingi). Vyama vingi ndivyo viloweka nadharia ya kina nani watakuwa Waheshimiwa kati ya Wananchi wote na hii ikazaa tamaa ya utukufu wa nyadhifa hizo.

Katika mukhtadha huo tulipoteza Siasa safi za vyama Kiitakadi, hasada ikachukua nafasi baina ya vyama vya Siasa, viongozi kwa viongozi, Wananchi na vyama pinzani na kibaya zaidi rushwa na upendeleo vikatumiwa kama zana katika teuzi toka chaguzi za ndani ya Vyama vya Kisiasa hadi Viongozi wa Kitaifa – Yakaibuka makundi ya timu za Wana, hasada ikazaa Chuki na Uadui matokeo yake UZALENDO kwa Taifa letu UKAPUKUTIKA.

Kwa hiyo tukiacha hoja ya Katiba Mpya pembeni, sisi Watanzania tuna wivu na chuki za kuhasimiana wenyewe kwa sababu ya fursa za madaraka na utajiri zimeletwa kupitia vyama vingi.

Viongozi waliopo madarakani hujiona wapo katika nafasi adimu sana ya Utajiri wa hadhi na mali na wanajua kuna macho ya wivu dhidi yao hata kama wanayofanya nia njema ama kinyume cha misingi ya demokrasia, bado utachikiwa tu. Siasa zetu zimekuwa ni za Ukinzani ambazo kiitikadi hazifanani kabisa na Upinzani kwa nia, dhamira na malengo ya Demokrasia.

Tujiulize wenyewe mpaka hapa tumefika ni viongozi wangapi wameuawa kwa ajali, risasi au sumu na hakuna watu walotiwa hatiani wala kuchukuliwa hatua. Nini hasa sababu za viongozi hao kuuawa? Bila shaka ni kunatokana na UADUI wa kisiasa walojenga dhidi ya kiongozi ama viongozi wengine iwe kwa nia safi au mbaya.

Wivu na Chuki sii lazima vitumike kwa wale washindani tu bali inaweza toka chini kwa wale wanaotaka kufika pale kiongozi alipofika ama kiongozi kulinda maslahi yake dhidi ya wale wanaotaka nafasi yake.

Kwa hiyo tunapozungumzia leo Maombolezi, Maridhiano na sijui Katiba Mpya ni muhimu kwanza sisi wenyewe tukubali mapungufu yetu kimaadili ili TUBADILIKE - Heshima ya Utu wetu na Uzalendo kwa Taifa ni utamaduni ulopitwa na wakati.

Hatuwezi fanya maombolezi ambayo baadhi yetu hawaoni umuhimu wala sababu. Hatuwezi fanya Maridhiano kwa kuwekeana masharti yasiyojali Utu wetu na Uzalendo kwa Taifa hili bali maslahi ya mtu au chama.

M inwisho hatuwezi kuwa na Katiba mpya inayotokana na maoni ya Wananchi wenye wivu, chuki na uadui isipokuwa Katiba lazima iwe ni mwongozo wa Wananchi hao bila kujali tofauti zao - Katiba ni ya Wananchi iheshimiwe na wote.

Maasalaam
sijasoma mada ila tumefika hapa kwa kutembea kwa mguu taratibu taratibu tu
 
..sasa nenda kasikilize interview ya Mzee Butiku alipohojiwa ktk podcast ya Salma na Mjenga ndipo utajua tumefika pabaya.

..tumevuka huko kwenye miiko ya uongozi, sasa hivi tuna tatizo la wana Ccm wanaomwaga DAMU za wapinzani.

..tunahitaji Katiba Mpya bora kwa sasa. Mambo mengine yote tutashughulika nayo tukiwa na Katiba mpya na bora.

..Hata MISAHAFU si ipo pamoja na watu kutenda maovu. Je, tulipaswa kusubiri wanadamu waache dhambi ndipo misahafu iteremshwe?

..KATIBA MPYA NI SASA.
Nimemsikiliza mzee wangu Butiku, yeye nu tafsiri halisi ya kile nilichoandika.ana Chuki na Chadema ni Maadui zake, hivyo hivyi kibaya zaidi hata Chadema mtu yeyite bdani ya CCM ni adui yao. Sababubsio Itikadi wala sera bali Chama.

Samahani Chukulia Magufuli ambae aliiba itikadi na Sera za Chadema mwaka 2015 lakini yeye ndite akawa Adui wa Chadema toka anaapishwa! Halafu Chadem walokuwa wakipinha Ufisadi wakamchukua Lowassa na kumoa sifa zote!

Yote haya ni kutazamwa fursa za kuingia Ikulu hapakuwa na Siasa safi wala Uzalendo kwa nchi yetu. ACT wanaojiita Wajamaa na Wazalendo leo wanapigania Uzanzibar! Tena kibaya zaidi wanarudisha siasa za Hizbu ambazo zilipigwa marufuku baada ya Mapinduzi.
 
Uchaguzi wa Mwaka 2005 ndio uliopanda siasa mpya za nchi hii. Matokeo mengine yote mbegu ilianzia pale na mnakumbuka pia 2010 JK alivyosaka kura kwa kusaidiwa na familia! Kila uchaguzi umekuwa chanzo cha mipasuko na kuzaa makundi yanayohujumiana. Uchaguzi wa 2025 ilikuwa kilele cha matatizo ya muda mrefu. Kuelekea 2030 kama tusiporudi kwenye misingi tutaingia nchi kwenye matatizo yaliyopo Congo.
 
Ukiwa mharifu lazima utakuwa unahisi unachukiwa pale watu wanapojadili mabadiliko. Sasa katiba mpya ni tishio kwa nani? Na kwanini atishike?
Mkuu wangu, ukiwa Kiongozi ikiwa mabadiliko mnayoyataka hayaendani na fursa nilizonazo unategrmea nani atakubali?

Kumbuka Bunge la Katiba lilivunjika kwa sababu pande mbili hazikuafikiana na ukitazama sababu zenyewe tunarudi pale pale hoja zote hazikuzingatia UTU wetu bali tofauti zetu - Tuliishia Patupu.
 
Kubwa zaidi lilojitokeza kwangu linatokana na hotuba ya Profesa Shivji alipozungumzia Misingi mikuu ya Demokrasia akifafanua juu ya pande mbili yaani upande Wananchi na upande wa Utawala. Na kilichojitokeza wazi kwangu ni Kupotea thamani na heshima ya UTU wetu. UTU ndio kiashiria cha ujenzi na usimamizi wa Uhuru na Usalama.
Ukisha "UTU" kuwa msingi; hakuna tena cha zaidi ya hapo.

Mimi nimekusoma hadi hapo kwenye hayo maneno, na sikuwa na maswali zaidi yanayonisumbua kwenye hali ya Tanzania ilivyo sasa.
 
Uchaguzi wa Mwaka 2010 ndio uliopanda siasa mpya za nchi hii. Matokeo mengine yote mbegu ilianzia pale na mnakumbuka pia 2015 JK alivyosaka kura kwa kusaidiwa na familia! Kila uchaguzi umekuwa chanzo cha mipasuko na kuzaa makundi yanayohujumiana. Uchaguzi wa 2025 ilikuwa kilele cha matatizo ya muda mrefu. Kuelekea 2030 kama tusiporudi kwenye misingi tutaingia nchi kwenye matatizo yaliyopo Congo.
Hapana Uchaguzi wa 2015 nadhani ndio ulotugawa zaidi makundi. CCM kule wakagawanyika JK na Lowassa! Chadema Dr. Slaa na Lowassa lakini yote kwa pamoja ni Kusaka Uheshimiwa kuingia magogoni.
Kila upande focus kubwa ilikuwa kuingia Ikulu sio kuwatumikia Wananchi. Na hili limekuwa likisemwa na vyama vyote kwamba nia na dhamira ya Vyama vya Siasa ni Kuingia Ikulu. Wee Mwananchi sio priority yao bali ni njia ya kuwafikisha magogoni. Chama kikisha kuwa na dhamira hiyo, mbinu zake lazima hazitakuwa nzuri hata kidogo, kuua, rushwa na wizi vyote vinaingia katika mbinu zake maadam zimefanikiwa.
 
hivyo hivyi kibaya zaidi hata Chadema mtu yeyite bdani ya CCM ni adui yao. Sababubsio Itikadi wala sera bali Chama.
Wewe huna tofauti yoyote na huyo Butiku. Hili la CHADEMA kuwachukulia CCM kuwa maadui unayo mifano ya kutuonyesha hili?
CHADEMA walishawaua watu wa CCM wangapi, kwa mfano? Lakini tunajuwa ni kiasi gani CHADEMA wamevurugwa sana UTU wao na hao CCM.

Tatizo la mada hizi za kujifichaficha vichakani, huku zikiwa na lengo maalum ni tatizo kubwa sana. Na Samia na Genge lake ni mashuhuri sana kwa tabia za namna hii.
 
Yaani hawa kwa vile wamewaua cdm wanahofu wasije kugeuziwa kibao
 
Mjomba ulichoshauri hapo mwishoni hakitekelezeki. Mimi natamani kuona muungano unavunjika ili na sisi Watanganyika tujivunie uwepo wa nchi yetu ya Tanganyika, kama wafanyavyo Wazanzibari kwa Zanzibar yao. Kwa kufanya hivi nchi yetu haitokuja kutawaliwa tena na vilaza, mafisadi, wahuni, au watu wasio na chembe ya uzalendo.
Muungano haukuasisiwa kuwa nyenzo ya kuwafanya waTanganyika kuwa koloni la Zanzibar; lakini wenye ajenda zao sasa wameufanya kuwa nyenzo ya kuingiza maswala mazito zaidi ya ukoloni.

Sioni muungano huu ukiendelea kuwepo.
Itakuwa ni uenda wazimu.
 
Mpya ni muhimu kwanza sisi wenyewe tukubali mapungufu yetu kimaadili ili TUBADILIKE -
Nimekuelewa mkuu. Unayo hoja ya msingi.

Sasa tunaomba muongozo wa namna gani tutatekeleza suala la sisi wenyewe kukubali mapungufu yetu kimaadil. Nani anaanza kukubali? Nani anafuata? Nani anasimamia zoezi la kukubali mapungufu? na maswali.mengine ya namna hiyo.

Kisha ni nani atasimamia.kuhakikisha upungufu wa kiamaadili haujitokezi tena? Na anapewa instruments zipi kuhakikisha hili linatekelezeka?

Natanguliza shukrani kwa majibu.
 
Yaani hawa kwa vile wamewaua cdm wanahofu wasije kugeuziwa kibao
Lakini hiyo ya "kugeuza kibao" haikuwa sababu ya kuwaua watu wa CHADEMA.

Sasa iwepo hofu au isiwepo, ni jukumu la waTanzania wasiokubaliana na upuuzi huu kuwakataa na kuwaondoa kwa njia zozote zitakazowezekana..
Na kwa vile wanayo hofu tayari, maana yake ni kwamba kuua ndiyo njia pekee waliyobaki nayo kuendelea kuwa madarakani.
 
Wewe huna tofauti yoyote na huyo Butiku. Hili la CHADEMA kuwachukulia CCM kuwa maadui unayo mifano ya kutuonyesha hili?
CHADEMA walishawaua watu wa CCM wangapi, kwa mfano? Lakini tunajuwa ni kiasi gani CHADEMA wamevurugwa sana UTU wao na hao CCM.

Tatizo la mada hizi za kujifichaficha vichakani, huku zikiwa na lengo maalum ni tatizo kubwa sana. Na Samia na Genge lake ni mashuhuri sana kwa tabia za namna hii.
Mkuu wangu mimi nasikiliza sana Hotuba za Viongozi wote. Labda nikeambie tu.kwamba wote hutumia neno hao MAADUI ZETU kama ni Upinzani. Huamini nitaziweka hapa.
 
Back
Top Bottom