Watanzania, Msichaguwe Chama Chagueni Kiongozi

Sahamani bila dharau wala ukorofi. Hivi hilo neno ni UTULIVU au UTUVU?

Nisijekuwa silifahamu hilo neno jipya linalotumika kwenye Kiswahili maana huwa hufanyi makosa zaidi ya kuwakosoa wengine kila wanapokosea. UTUVU maana yake nini kama siyo Utulivu?

Siyo leo hiyo ni ya zamani, tazama tarehe niliyoiweka.

Huwa hunisomi tu. Ukinisoma kwa utuvu utanielewa tu.
 
Yanini unaandikia mate na wino upo? porojo zako hazisaidii kitu, tulimnganishe na Rais yeyote wa Tanzania umpendae wa kabla yake katika mambo kumi ya Kitaifa na ukipeda Kimataifa vile vile, au kukurahisishia wachanganye Marais wote wa kabla yake kwa pamoja tulinganishe na Kikwete peke yake, katika nyanja zote.1) Elimu.Kikweteshule za sekondari wakati wake zaidi ya 4600.Vyuo vikuu zaidi ya 50.Vyuo vya ufundi?Vyuo vya waalimu?Vyuo vya Udaktari?vyuo vya kijeshi?Tuanze hilo moja, unasemaje?
Katika sekondari alizojenga JK ni sekondari ipi ina hadhi ya mtoto wa JK kusoma au mtoto wa waziri yeyote?
 
muelewe mleta uzi anajaribu kuonesha namna ya kumpata mshindi bila kujali chama.amezungumzia namna walivyochaguliwa bila kujali nini walichokifanya baada ya kuchaguliwani ukweli tuache uchama kwenye nafasi hasa ya urais
Kuna mgombea mwenye ilani binafsi? Au kwani kuna mgombea binafsi,wagombea hata wawe wazuri vipi wanabeba miilani ya vyama
 
Wakati tunaingia kwenye mwaka wa heka heka za uchaguzi wa Wabunge na wa Rais.

Nawaasa Watanzania wasichaguwe chama bali wachaguwe kiongozi.

Mfano mzuri ni kama tuliouonesha mwaka 2005, wakati tulipomchaguwa Kikwete kuwa kiongozi mkuu wa nchi hii. Ushindi alioupata Kikwete wa zaidi ya kura 80% ni dhahiri ulikuwa si kwa kuchaguliwa na wana CCM bali hata wa upinzani na wasio na vyama.

Mfano mwingine ni wa John Shibuda, pale alipoihama CCM na kuhamia Chadema, wana CCM wa jimbo lake wengi walimpa kura zao bila kujali yupo chama kipi. Huo ni uzalendo na unaonesha jinsi Tanzania tunavyoweza kufanya maamuzi bila ya kuburuzwa na chama au wenye chama.

Viongozi wazuri tunao, tena tusingoje wale wanaojitokeza tu kuzitaka hizi nyadhifa kwa udi na uvumba. Tutazame katika jamii, tunapomuona anaefaa kuongoza, hata kama si mwanasiasa, bali tukimuona kuwa haa huyu anafaa kuongoza, tumlazimishe, tumsimamishe, tumchaguwe.

Tukianza kuchaguwa viongozi na si chama tutakuwa sisi wenyewe tumeshakuwa viongozi.Tuanze kwa kujiongoza wenyewe kwa kuchaguwa tukitakacho na si kuburuzwa na wakitakacho wenye vyama.

Tukianza hivyo, hata vyama vyetu vitaweka viongozi tuwatakao na si wawatakao wenye vyama

Nasema haya kwa kuwa nimeona katika vyama vyetu vya siasa vyote, kuna tabia ya kura za maoni. Wananchi wanaweza kuwa na mgombea wao wakampendekeza agombee lakini ikifika kwenye vyama wanakatwa na kuwekwa wale wawatakao wenye vyama. Hii si demokrasia tuitakayo na huleta uvunjifu wa amani.

Ni wakati muafaka sasa Watanzania tusikubali kuchaguwa wamtakae wenye vyama, tunataka tuwe na viongozi tuwatakao wananchi tulio wengi. Tunataka na wagombea huru, wasio na vyama pia wawepo, ili tuwachaguwe tuwaonao wanatufaa na si wanaowafaa wenye vyama.

Huwa hatuchagui tunaaambiwa chagua huyu, unaambiwa umemuona yuleee--ndio flani apewe kura, unaaambiwa chukua weka waaaa-utanipaaaaa asiyenipa mchawi anyway sikuizi nakupenda weye umekomaa sasa mdada ki -hoja umebadilika sana huenda una rafiki mpya
 
muelewe mleta uzi anajaribu kuonesha namna ya kumpata mshindi bila kujali chama.
amezungumzia namna walivyochaguliwa bila kujali nini walichokifanya baada ya kuchaguliwa

ni ukweli tuache uchama kwenye nafasi hasa ya urais

Usidanganywe, na huyu MJAHIDINA, huyu swala la dini linamsumbua. Hakuna mkristo mzuri kwake, nyambafu kabisa
 
Sahamani bila dharau wala ukorofi. Hivi hilo neno ni UTULIVU au UTUVU?

Nisijekuwa silifahamu hilo neno jipya linalotumika kwenye Kiswahili maana huwa hufanyi makosa zaidi ya kuwakosoa wengine kila wanapokosea. UTUVU maana yake nini kama siyo Utulivu?

Ni la Kiswahili na utuvu ni kinyume cha utovu.
 
muelewe mleta uzi anajaribu kuonesha namna ya kumpata mshindi bila kujali chama.
amezungumzia namna walivyochaguliwa bila kujali nini walichokifanya baada ya kuchaguliwa

ni ukweli tuache uchama kwenye nafasi hasa ya urais

Nnaamini kabisa Kikwete alipigiwa kura na watu wa vyote bila kujali chama na ndiyo maana mpaka hii leo rekodi yake ya uongozi hakuna hata Rais mmoja wa kabla yake na hata kwa ujumla wao anaeifikia kwenye nyanja zote.
 
Mmh!! Fafanua kwa mifano!!!
 
Shule za JK wanasoma akina kajamba nani hukuti mtoto wa JK,SITA,BILAL,MWINYI WALA KATIBU MKUU.Shule kajenga lkn mwenyewe anaziogopa.

Wana uwezo wa kusomesha watoto wao shule za kulipia. Tatizo nini?

Na wewe jitahidi uwapeleke huko.
 
Wana uwezo wa kusomesha watoto wao shule za kulipia. Tatizo nini?Na wewe jitahidi uwapeleke huko.
Kamwe wanangu hawatasoma kwenye magofu ya JK,Hayo wasome wajukuu zako.Yaani wasome shule za JK Ambapo unaingia tu form one asilimia za kufeli ni kubwa kuliko za kufaulu.Shule za serikali zilikuwa shule enzi za mwalimu sasa hivi zimekuwa magodown tu
 
Kama una uwezo wa kuwasomesha wanao, mbona zipo shule mpaka za dollar 5,000 kwa mwezi? darasa halizidi wanafunzi sita na mwalimu mmoja hafundishi zaidi ya masaa mawili kwa siku.

Hongera sana, na hayo unayaweza leo kwa sera nzuri za Kikwete.

Halafu, hao watoto wa kwenda shule umewapata lini? wewe mwenyewe si bado mwanafunzi na upo nyumbani kwa wazazi wako?
 
Kama una uwezo wa kuwasomesha wanao, mbna zzipo sule mpaka za dolaar 5,000 kwa mwezi? darasa halizidi wanafunzi sita na mwalimu mmoja hafundishi zaidi ya masaa mawili kwa siku.Hongera sana, na hayo unayaweza leo kwa sera nzuri za Kikwete.Halafu, hao watoto wa kwenda shule umewapata lini? wewe mwenyewe si bado mwanafunzi na upo nyumbani kwa wazazi wako?
Nipo kwa wazazi,nitake radhi kwa hili tafadhali? Unafikiri kwa mie kuweza kuwapeleka watoto kwenye shule zenye unafuu wa elimu basi kila MTZ anaweza nenda kaangalie shule za JK zilivojaa na watoto wanaambulia 0
 
Wewe unavyoaandika tu unaonesha ni bado kula kulala nyumbani.

Kama wazee wana una uwezo wa kukusomesha nje ya shule hizo ni pia kwa sera nzuri za Serikali hii hii. Kumbuka hilo.
 
Hata achaguliwe Malaika endapo mfumo ni wa kutekeleza ilani ya chama ufisadi utaendelea tu hakuna jipya!
Wakati tunaingia kwenye mwaka wa heka heka za uchaguzi wa Wabunge na wa Rais.

Nawaasa Watanzania wasichaguwe chama bali wachaguwe kiongozi.

Mfano mzuri ni kama tuliouonesha mwaka 2005, wakati tulipomchaguwa Kikwete kuwa kiongozi mkuu wa nchi hii. Ushindi alioupata Kikwete wa zaidi ya kura 80% ni dhahiri ulikuwa si kwa kuchaguliwa na wana CCM bali hata wa upinzani na wasio na vyama.

Mfano mwingine ni wa John Shibuda, pale alipoihama CCM na kuhamia Chadema, wana CCM wa jimbo lake wengi walimpa kura zao bila kujali yupo chama kipi. Huo ni uzalendo na unaonesha jinsi Tanzania tunavyoweza kufanya maamuzi bila ya kuburuzwa na chama au wenye chama.

Viongozi wazuri tunao, tena tusingoje wale wanaojitokeza tu kuzitaka hizi nyadhifa kwa udi na uvumba. Tutazame katika jamii, tunapomuona anaefaa kuongoza, hata kama si mwanasiasa, bali tukimuona kuwa haa huyu anafaa kuongoza, tumlazimishe, tumsimamishe, tumchaguwe.

Tukianza kuchaguwa viongozi na si chama tutakuwa sisi wenyewe tumeshakuwa viongozi.Tuanze kwa kujiongoza wenyewe kwa kuchaguwa tukitakacho na si kuburuzwa na wakitakacho wenye vyama.

Tukianza hivyo, hata vyama vyetu vitaweka viongozi tuwatakao na si wawatakao wenye vyama.

Nasema haya kwa kuwa nimeona katika vyama vyetu vya siasa vyote, kuna tabia ya kura za maoni. Wananchi wanaweza kuwa na mgombea wao wakampendekeza agombee lakini ikifika kwenye vyama wanakatwa na kuwekwa wale wawatakao wenye vyama. Hii si demokrasia tuitakayo na huleta uvunjifu wa amani.

Ni wakati muafaka sasa Watanzania tusikubali kuchaguwa wamtakae wenye vyama, tunataka tuwe na viongozi tuwatakao wananchi tulio wengi. Tunataka na wagombea huru, wasio na vyama pia wawepo, ili tuwachaguwe tuwaonao wanatufaa na si wanaowafaa wenye vyama.
 
hata aje malaika toka mbinguni awe kiongozi kupitia ccm hali itakuwa ni mbaya tu.
 
Mfano hai ni mwaka 1995 wakati Kikwete alipowania kuwa Rais kwa mara ya kwanza, hakuna asiyejuwa kuwa alishinda ndani ya chama lakini wenye chama hawakutaka, matokeo unayajuwa.

FF
Mwaka 1995 JK hakushinda ndani ya CCM ndo maana hakuwa kiongozi katika kipindi hicho 1995/2005. Na kama unajitoa ufahamu kwa hili ni sawa na kusema uchaguzi mkuu wa 2010 JK hakushinda, matokeo unayajua.
 
Back
Top Bottom