Watanzania, Msichaguwe Chama Chagueni Kiongozi

Watanzania, Msichaguwe Chama Chagueni Kiongozi

hoja imekuwa nzito kwako na haujuwi uanzie wapi kuijibu.

nalazimika kukupa elimu kidogo.kwani matatizo yetu yetu ni "kiongozi"dada???kama ni kiongozi manake unakiri ya kuwa uongozi wa sasa chini ya profesa dr.kikwete (wa chama chako)ni "mbaya".kama huoni kama tuna "matatizo"???kama unaona kuwa kuna matatizo,je matatizo yetu ni ya kimfumo au uongozi????na kama ni ya kimfumo,tufanye nini zaidi ya uondoa mfumo huu mbaya?????swali je ni mfumo upi mbaya na nani muasisi wa mfumo huo?????jaribu kujiuliza hayo maswali,kisha ndo uandike hayo unayoyaandika.otherwise,utaonekana kituko unayetaka kuchekesha watu wenye fikra pana!!!
 
Mleta mada hajui anaongea nn Na watu Wa namna hiyo ni hovyo kabisa, wezako unaona hata mgombea binafsi hawamtaki kabsa kaa ujiulize kwa nn.Jitambue Na elewa uko sayari gani
 
Wakati tunaingia kwenye mwaka wa heka heka za uchaguzi wa Wabunge na wa Rais.

Nawaasa Watanzania wasichaguwe chama bali wachaguwe kiongozi.

Mfano mzuri ni kama tuliouonesha mwaka 2005, wakati tulipomchaguwa Kikwete kuwa kiongozi mkuu wa nchi hii. Ushindi alioupata Kikwete wa zaidi ya kura 80% ni dhahiri ulikuwa si kwa kuchaguliwa na wana CCM bali hata wa upinzani na wasio na vyama.

Mfano mwingine ni wa John Shibuda, pale alipoihama CCM na kuhamia Chadema, wana CCM wa jimbo lake wengi walimpa kura zao bila kujali yupo chama kipi. Huo ni uzalendo na unaonesha jinsi Tanzania tunavyoweza kufanya maamuzi bila ya kuburuzwa na chama au wenye chama.

Viongozi wazuri tunao, tena tusingoje wale wanaojitokeza tu kuzitaka hizi nyadhifa kwa udi na uvumba. Tutazame katika jamii, tunapomuona anaefaa kuongoza, hata kama si mwanasiasa, bali tukimuona kuwa haa huyu anafaa kuongoza, tumlazimishe, tumsimamishe, tumchaguwe.

Tukianza kuchaguwa viongozi na si chama tutakuwa sisi wenyewe tumeshakuwa viongozi.Tuanze kwa kujiongoza wenyewe kwa kuchaguwa tukitakacho na si kuburuzwa na wakitakacho wenye vyama.

Tukianza hivyo, hata vyama vyetu vitaweka viongozi tuwatakao na si wawatakao wenye vyama.

Nasema haya kwa kuwa nimeona katika vyama vyetu vya siasa vyote, kuna tabia ya kura za maoni. Wananchi wanaweza kuwa na mgombea wao wakampendekeza agombee lakini ikifika kwenye vyama wanakatwa na kuwekwa wale wawatakao wenye vyama. Hii si demokrasia tuitakayo na huleta uvunjifu wa amani.

Ni wakati muafaka sasa Watanzania tusikubali kuchaguwa wamtakae wenye vyama, tunataka tuwe na viongozi tuwatakao wananchi tulio wengi. Tunataka na wagombea huru, wasio na vyama pia wawepo, ili tuwachaguwe tuwaonao wanatufaa na si wanaowafaa wenye vyama.

Your a very great thinker Lady! Huwa nikisoma post zako zimetulia,We the people of this forum.Need people like you.Big up a millions times
 
Back
Top Bottom