mwakaila
JF-Expert Member
- Jan 4, 2014
- 1,053
- 157
Jee, wewe utakichaguwa chama au kiongozi?
Usinivute kujadili hofu zako
Jee, wewe utakichaguwa chama au kiongozi?
Chama si kama underwear kuwa unabadili hata kama haijakuwasha. Sijawahi kuchaguwa kiongozi kwa ajili ya chama chake, nachaguwa kiongozi kwa uwezo wake.
CUF ikimsimisha Lipumba siwezi kumchaguwa, huo ndiyo ukweli, Lipumba angebaki kwenye fani yake tu ya Uchumi wa Kimataifa.
Wakati huohuo kwa upande wa ukawa simuoni mwengine anaemzidi uwezo Lipumba mpaka dakika hii.
FF hapa unazungumzia kuzidi uwezo wa kitu gani, fedha, elimu, kusoma kuruani, urefu, nini? Kwa mantiki hiyo hiyo utuambie kama uwezo wa Kikwete ndio upeo wa juu zaidi kwa wanachama wote wa ccm na kama ndio hivyo basi huko ccm wapo wa kuwasimamisha kwenye udiwani tu.
Usinivute kujadili hofu zako
Mfano mzuri ni kama tuliouonesha mwaka 2005, wakati tulipomchaguwa Kikwete kuwa kiongozi mkuu wa nchi hii. Ushindi alioupata Kikwete wa zaidi ya kura 80% ni dhahiri ulikuwa si kwa kuchaguliwa na wana CCM bali hata wa upinzani na wasio na vyama.
Mfano mzuri ni kama tuliouonesha mwaka 2005, wakati tulipomchaguwa Kikwete kuwa kiongozi mkuu wa nchi hii. Ushindi alioupata Kikwete wa zaidi ya kura 80% ni dhahiri ulikuwa si kwa kuchaguliwa na wana CCM bali hata wa upinzani na wasio na vyama.
Kwahiyo ww na team LUMUMBA ndio Mlituletea Huyu rais dhaifu
Na sasa unakuja na sera yako hii ya UCCHAGUE CHAMA CHAGUA MTU. hii inadhihirisha tayari umeanza kuipiga kibuti CCM yako iliyokufundisha usanii.
Ngoja tuone safarihii utampigia debe nani na akihama ccm unahama nae
Wana ccm msimshambulie sana FF mkidhani kahama chama hapana. Yuko kutekeleza maazimio ya cc ya chama chenu. Kumbukeni mna mambo mawili yanayowavuruga, kumpata mgombea ndani ya chama na pili muungano wa ukawa. Sasa mkakati kazi ni kama ifuatavyo
1. Kuwadhoofisha wenye uchu wa kuteuliwa kushika hizo nyadhifa kwa njia ya kuwapelekea wanachama wapendekeze majina. Njia hii ni rahisi kuwachakachua hao wenye uchu na kuwaambia hamkupendekezwa
2. FF anatimiza mkakati wa kuwavuruga UKAWA akijaribu kuja na majina anayoona kuwa yanafaa, akimaanisha kuwa watu fulani, tuseme waislam wasipoona majina fulani basi wachague jina lingine.
Propaganda ya FF na ccm sio ya kuishabikia harakaharaka, hawa ndio wale ambao hujifanya wamerudisha kadi kumbe ni 'trojan horse', akiingia kambini tu anavuruga kila kitu.
We hujanijua.....ngoja nikupe kali yako
Faiza naona unatafuta njia ya kutokea baada ya kuona hakuna muislam yoyote anaefaa kuwa rais....kwa sisiemu. ....ila karibu ukawa tuna lipumba Jembeeee
Na ndio maana midahalo nyakati za uchaguzi ni ya muhimu sana. Pamoja na kuwa mgombea anasimama kupitis chama flani na sera za chama, ni muhimu kuutambua uwezo binafsi wa mgombea. Chama kinaweza kuwa na sera nzuri lakini msimamizi wa sera ambae ni raisi asipokuwa na weledi na umadhubuti wa kusimamia na kutimiza sera basi inaangusha nchi.
Ni muhimu kupima uwezo binafsi wa individuals na kwa kuanzia, midahalo itakuwa ya muhimu sana kupembua chuya na mchele.
Mfano mwingine ni wa John Shibuda, pale alipoihama CCM na kuhamia Chadema, wana CCM wa jimbo lake wengi walimpa kura zao bila kujali yupo chama kipi. Huo ni uzalendo na unaonesha jinsi Tanzania tunavyoweza kufanya maamuzi bila ya kuburuzwa na chama au wenye chama.
Siwapendi watu wanaoingiza udini katika siasa. UKAWA wasipomsimamisha Prof. Lipumba utahamia chama kipi?
Tumchagueni mtu ambae atatuongoza yeye, sio chama chake. tulikuwa tukiongozwa na ccm sio mtu. agekuwa mtu tungefanya ya maana. Sio kuchagua mtu, mwisho wa siku hana sauti. tunabaki kuongozwa na wajanja ndan ya chama chake. rais lazima awe na maamuzi na ubabe kidogo
Mkuu FF,nakupa "LIKE" mia moja za mdomoni,elimu hii ya uraia unayoitoa hapa JF ndiyo inayotakiwa kutolewa kwa watanzania wote wa maeneo yote ya tanzania nzima na kazi hii ya uelimishaji jamii kama itafanywa kwa wakati na kila mtanzania mwenye uwezo wa kufanya hivyo,basi naamani mabadiliko makubwa sana yatatokea katika uongozi wa nchi hii ambayo yatapelekea mabadiliko makubwa ya kiutendaji.Wakati tunaingia kwenye mwaka wa heka heka za uchaguzi wa Wabunge na wa Rais.
Nawaasa Watanzania wasichaguwe chama bali wachaguwe kiongozi.
Mkuu FF,nakupa "LIKE" mia moja za mdomoni,elimu hii ya uraia unayoitoa hapa JF ndiyo inayotakiwa kutolewa kwa watanzania wote wa maeneo yote ya tanzania nzima na kazi hii ya uelimishaji jamii kama itafanywa kwa wakati na kila mtanzania mwenye uwezo wa kufanya hivyo,basi naamani mabadiliko makubwa sana yatatokea katika uongozi wa nchi hii ambayo yatapelekea mabadiliko makubwa ya kiutendaji.
Mimi wasiwasi wangu ni moja,je ni nani mwenye jukumu rasmi la kueneza elimu hii ya uraia kwa watanzania?
Je hao wenye jukumu hili rasmi,wanatimiza wajibu wao kwa kiasi gani?