Dini maana yake ni njia, kama ulikuwa huelewi, sasa kusema mimi nna "udini" ni kama kuniambia mimi nna njia yangu nnayoifata, wakati huo si ukweli. Mimi nnafata njia inayofundishwa na Uislam, wewe nnauhakika unafata njia inayofundishwa na Ukristo. Na kama hufati njia inayofundishwa na Ukristo wala Uislaam basi lazima una njia yako unayoifata na kama hiyo njia ni yako peke yako basi huo ndiyo "udini".
Kumwita Slaa kuwa padri huo ndiyo ukweli, kama ukweli ndiyo udini kwa maana yako basi utaniona ni mdini sana kwani sisiti kusema ukweli. Siwezi leo hii nikamwita padri Slaa kuwa ni Imamu Slaa. Ntakuwa ni muongo na ntakuwa namfanyia kejeli isiyo na msingi.
Ngao yenu ya kijinga ni hiyo yakumpachika mtu jina la udini ili tu mtimize matakwa yenu ya kupindisha mijadala. Ikiwa kwa muono wako huo finyu unaona mimi ni mdini basi kumbuka kuwa utaniona ni mdini sana, kwa sababu kila maamuzi yangu kwanza na pili na tatu huyafanya kwa Uislam wangu. Wewe una haki ya kufata njia aka dini yako uipendayo na au udini uupendao.
Kum depict mtu kuwa ni mdini ni udini mkubwa sana kuliko hizo maana finyu ulizoelezea. Ikiwa njia yako ya kuubadili mjadala ni kutumia neno udini basi hujafanikiwa, mjadala ndiyo unanoga.
Jee, wewe utachaguwa kiongozi au chama?
Kwenye hoja yako ya kutaka achaguliwe mtu na siyo chama, nakubaliana nawe kiasi lakini natofautiana nawe zaidi.
Nakubaliana nawe kwenye ngazi za chini, kama vile vijiji lakini unapokuja kwenye ngazi ya Taifa ni muhimu pia kutazama sera za chama, umadhubuti wa chama katika kusimamia maamuzi, kupiga vita rushwa na ubunifu wa chama katika kuandaa sera zinazotekelezeka kutokana na ubunifu wa mipango iliyopo.
Nchi kama Singapore imefanikiwa sana kiuongozi, kiutawala na kiuchumi kwa sababu wao mfumo wao ni wa kuchagua chama, na baada ya hapo chama kilichoshinda humchagua Rais baada ya kupitia mchakato mgumu na wa kina. Kuna wakati chama kilichokuwa kimeshinda kilitamka wazi kuwa hakikuwa na mwanachama ndani ya chama chao aliyewathibitishia kuwa ana uwezo wa kutimiza ambayo chama kiliwaahidi wapiga kura. Chama kilimwomba mfanyabiashara awe mwanachama, na kisha kikamkabidhi madaraka ya Urais. Singapore wanasema, siyo rahisi mwananchi wa kule Muze (Rukwa) au Nakapanya (Ruvuma) kufahamu kwa uhakika kabisa kama Kikwete ana uwezo wa kuwa Rais bora au hapana, wao ndani ya chama ndiyo wanaojua.
Utawala wa CCM umetupa fundisho kubwa kuwa ili tupate mabadiliko hatustahili tu kumpigia kura mgombea pekee yake bali ni pamoja na chama. Mara kadhaa tumewachagua wagombea wazuri kupitia CCM lakini wakifika bungeni au wanapoteuliwa kuwa mawaziri wameshindwa kabisa kutimiza yale waliyowaahidi wananchi. Ukikaa nao mmoja mmoja watakuambia kuwa wanashindwa kuleta mabadiliko kutokana na mfumo mbaya wa CCM wa kuwadhibiti wale wanaoenda kinyume na matakwa ya chama.
Kama tunataka kuleta mabadiliko katika nchi yetu, ni lazima tuangalie ubora wa mgombea, na tutazame mgombea huyo anatoka chama gani.
Nimesoma kitabu cha January Makamba, ukitazama aliyoyasema kuhusu Tanzania mpya ni mazuri sana lakini hayatekelezeki akiwa ndani ya CCM. Yeye anataka kuleta fikra mpya, je, CCM yenyewe ina fikra mpya? Tatizo hilo alilipata sana Mkapa na Kikwete, na kuna wakati marais hawa walijaribu kutaka kuwa na nguvu katika chama kwa kuwapeleka mawaziri wao wagombee ujumbe wa halmashauri kuu ili kuleta fikra mpya kuanzia kwenye chama, wote walipigwa chini, hawakupita. Kwa sababu wale wahafidhina wamejenga umoja fulani, na umoja wenyewe ni wa uovu. Wao wanawachagua watu kwa kuangalia nani amewapa bahasha, na huyo mgombea atampa fadhila gani. wale watu wasafi kwa sababu hawawezi kuhonga au kuahidi au kutoa upendeleo kwa wajumbe wanaopiga kura, hawapiti ndani ya CCM. Wengi wa wanaopita katika kugombea uongozi ndani ya CCM ni wale watoa rushwa, na mtoa rushwa hawezi kukosa kupokea rushwa.
Nasisitiza, ni lazima tuangalie ubora wa wagombea na ubora wa chama maana kwa mfumo wetu wa Tanzania chama kina nafasi kubwa sana katika uongozaji na usimamiaji wa serikali.