Watanzania, Msichaguwe Chama Chagueni Kiongozi

Watanzania, Msichaguwe Chama Chagueni Kiongozi

Wakati tunaingia kwenye mwaka wa heka heka za uchaguzi wa Wabunge na wa Rais.

Nawaasa Watanzania wasichaguwe chama bali wachaguwe kiongozi.

Mfano mzuri ni kama tuliouonesha mwaka 2005, wakati tulipomchaguwa Kikwete kuwa kiongozi mkuu wa nchi hii. Ushindi alioupata Kikwete wa zaidi ya kura 80% ni dhahiri ulikuwa si kwa kuchaguliwa na wana CCM bali hata wa upinzani na wasio na vyama.

Mfano mwingine ni wa John Shibuda, pale alipoihama CCM na kuhamia Chadema, wana CCM wa jimbo lake wengi walimpa kura zao bila kujali yupo chama kipi. Huo ni uzalendo na unaonesha jinsi Tanzania tunavyoweza kufanya maamuzi bila ya kuburuzwa na chama au wenye chama.

Viongozi wazuri tunao, tena tusingoje wale wanaojitokeza tu kuzitaka hizi nyadhifa kwa udi na uvumba. Tutazame katika jamii, tunapomuona anaefaa kuongoza, hata kama si mwanasiasa, bali tukimuona kuwa haa huyu anafaa kuongoza, tumlazimishe, tumsimamishe, tumchaguwe.

Tukianza kuchaguwa viongozi na si chama tutakuwa sisi wenyewe tumeshakuwa viongozi.Tuanze kwa kujiongoza wenyewe kwa kuchaguwa tukitakacho na si kuburuzwa na wakitakacho wenye vyama.

Tukianza hivyo, hata vyama vyetu vitaweka viongozi tuwatakao na si wawatakao wenye vyama.

Nasema haya kwa kuwa nimeona katika vyama vyetu vya siasa vyote, kuna tabia ya kura za maoni. Wananchi wanaweza kuwa na mgombea wao wakampendekeza agombee lakini ikifika kwenye vyama wanakatwa na kuwekwa wale wawatakao wenye vyama. Hii si demokrasia tuitakayo na huleta uvunjifu wa amani.

Ni wakati muafaka sasa Watanzania tusikubali kuchaguwa wamtakae wenye vyama, tunataka tuwe na viongozi tuwatakao wananchi tulio wengi. Tunataka na wagombea huru, wasio na vyama pia wawepo, ili tuwachaguwe tuwaonao wanatufaa na si wanaowafaa wenye vyama.

Huwa sikupendi,lakini wazo lako naliunga mkono kwa moyo mweupe.
 
Upo tayari kuona JK akihukumiwa kifo kama mahakama ikitoa hukumu kuwa zile suti alizopewa ilikuwa ni rushwa?.

Inaonesha ni dhamira na inaonesha sasa linashughulikiwa ipasavyo. Rushwa imeota mizizi kwa miaka 44 Tanzania hii.

Kikwete kaonesha ari na njia ya kuwa anaishughulikia na matokeo tunayaona. Mwenye macho haambiwi tazama, uliona wapi kabla ya Kikwete rushwa na ufisadi ukijadiliwa bungeni wazi wazi? uliona wapi kabla ya Kikwete mawaziri wakifikishwa mahakamani kwa ibadhirifu wa fedha za Serikali? uliona waoi kabla ya Kikwete mabalozi wakifikishw mahakamani kwa ubadhirifu wa fedha za umma? Ukweli ubaki kuwa ukweli.

Sasa hivi kinachotakiwa tuchaguw wabinge watakaokwenda kuionoa sharia ya rushwa na kuongezea makali, hukumu na adhabu za rushwa. Napendekeza adhabu ya rushwa iwe moja tu, kifo, iwe rishwa ya shillingi mia mbili au ya billioni mia mbili.

Na nnapendekeza kuwe na mahakama ya rushwa, ubadhirifu na ufisadi, mahakimu wabobee huko kama ilivyo mahakama za biashara na za nyumba na za kadhi.
 
Naam, pia ni mfano mzuri sana na unadhihirisha kuwa Tanzania hatuchaguwi chama tunachaguwa mtu, sasa isiishie kuchaguwa mtu, tuchaguwe mtu anaeweza kuongoza.

Si unaona Slaa anajidhihirisha kuwa si kiongozi mzuri, si kwa maadili si kwa kisiasa, hana sera. hana mipango hana muono. Yeye anangoja na kuvizia leo atasikia lipi aanze kuhororoja na kubwabwaja, no, hatutaki kiongozi wa namna hiyo hata kidogo.

"Mpaka sasa waliojitokeza kugombea urais CCM hakuna anayefaa" By Kingunge Kombale
FaizaFoxy unawezaje kusema Dr. Slaa hafai wakati ameishinda CCM kila uchaguzi aliogombea nao. Think Big, jiongeze.
 
Last edited by a moderator:
baada ya kugundua kuwa ccm itashindwa.vibaya amekuja na gia mpya ya kupooza makali ya kushindwa
kafie mbele ccm hatuichagui hata afufuke nyerere

CCM haina cha kushindwa na juzi imedhihirisha hilo na kabla ya hapo Chalinze, Kalenga na kata tatu chopa tatu, usisahau.

Hapa mantiki si CCM kushinda au kutokushinda, hili linamuhusu kila Mtanzania, nawaambia msiende mkachaguwa CCM hata kama ni chama chenu lakini mgombea aliyewekwa ni mbovu au msiende mkachaguwa chadema hata kama mgombea waliyemuweka ni mbovu. Nendeni mkachaguwe kiongozi kwa maslahi yenu wenyewe na si ya fulani au fulani au ya wenye vyama.

Hivi leo unajuwa kabisa, huyu nikimchaguwa hana la kuweza kukemea maadili mabovu kwa sababu maadili yake ni mabovu zaidi, halafu unaenda kumchaguwa kwa kuwa ni mwanachama wa chama chako? utakuwa hujitendei haki na huwatendei haki wale ambao hawajafikia umri wa kupiga kura.
 
"Mpaka sasa waliojitokeza kugombea urais CCM hakuna anayefaa" By Kingunge Kombale
FaizaFoxy unawezaje kusema Dr. Slaa hafai wakati ameishinda CCM kila uchaguzi aliogombea nao. Think Big, jiongeze.

Angeshinda uchaguzi si tungemuona Ikulu. Yule si "chaguo la Mungu", Mungu hawezi kumchaguwa Slaa kuongoza hii nchi. Nyota njema huonekana alfajiri.
 
Wakati tunaingia kwenye mwaka wa heka heka za uchaguzi wa Wabunge na wa Rais.

Nawaasa Watanzania wasichaguwe chama bali wachaguwe kiongozi.

Mfano mzuri ni kama tuliouonesha mwaka 2005, wakati tulipomchaguwa Kikwete kuwa kiongozi mkuu wa nchi hii. Ushindi alioupata Kikwete wa zaidi ya kura 80% ni dhahiri ulikuwa si kwa kuchaguliwa na wana CCM bali hata wa upinzani na wasio na vyama.

Mfano mwingine ni wa John Shibuda, pale alipoihama CCM na kuhamia Chadema, wana CCM wa jimbo lake wengi walimpa kura zao bila kujali yupo chama kipi. Huo ni uzalendo na unaonesha jinsi Tanzania tunavyoweza kufanya maamuzi bila ya kuburuzwa na chama au wenye chama.

Viongozi wazuri tunao, tena tusingoje wale wanaojitokeza tu kuzitaka hizi nyadhifa kwa udi na uvumba. Tutazame katika jamii, tunapomuona anaefaa kuongoza, hata kama si mwanasiasa, bali tukimuona kuwa haa huyu anafaa kuongoza, tumlazimishe, tumsimamishe, tumchaguwe.

Tukianza kuchaguwa viongozi na si chama tutakuwa sisi wenyewe tumeshakuwa viongozi.Tuanze kwa kujiongoza wenyewe kwa kuchaguwa tukitakacho na si kuburuzwa na wakitakacho wenye vyama.

Tukianza hivyo, hata vyama vyetu vitaweka viongozi tuwatakao na si wawatakao wenye vyama.

Nasema haya kwa kuwa nimeona katika vyama vyetu vya siasa vyote, kuna tabia ya kura za maoni. Wananchi wanaweza kuwa na mgombea wao wakampendekeza agombee lakini ikifika kwenye vyama wanakatwa na kuwekwa wale wawatakao wenye vyama. Hii si demokrasia tuitakayo na huleta uvunjifu wa amani.

Ni wakati muafaka sasa Watanzania tusikubali kuchaguwa wamtakae wenye vyama, tunataka tuwe na viongozi tuwatakao wananchi tulio wengi. Tunataka na wagombea huru, wasio na vyama pia wawepo, ili tuwachaguwe tuwaonao wanatufaa na si wanaowafaa wenye vyama.

Naomba sana ubadilishe hilo wazo elewa hivi chama ndicho kina sera, mtu ana maono binafsi hivyo hawezi kuleta mabadiliko ya kweli kwenye jamii kubwa. kwa kifupi nitapigia kuRA CHAMA si mtu mwambie jirani yako achague CHAMA
 
Umeamka vizuri leo, kesho alikuamsha mwambie akuamshe kila siku, au amkia kila siku ubavu ulioamkia leo. FaizaFoxy

Sio kaamuka vizuri kasoma alama za nyakati huo ni ujanja kaona chama lake watu wamelisusa na sasa halina ushawishi tena,linaelekea kule ilikoelekea KANU ya Kenya,hata mwenyewe FF keshaona sasa hapo nia yake ni kutuletea Mpemba awe raisi wa JMT.Hiyo hatukubali safari hii ni mtu wa msalaba ndie atakuwa presidaa na sio mtu wa mwezi na nyota baasi.
 
Wakati tunaingia kwenye mwaka wa heka heka za uchaguzi wa Wabunge na wa Rais.

Nawaasa Watanzania wasichaguwe chama bali wachaguwe kiongozi.

Mfano mzuri ni kama tuliouonesha mwaka 2005, wakati tulipomchaguwa Kikwete kuwa kiongozi mkuu wa nchi hii. Ushindi alioupata Kikwete wa zaidi ya kura 80% ni dhahiri ulikuwa si kwa kuchaguliwa na wana CCM bali hata wa upinzani na wasio na vyama.

Kwa nini unaleta wazo la mtu badala ya chama baada ya kuona jina CCM haliuziki? CCM haina soko tena ndo maana inabiodi nguvu ndo itumike kupita ktk nafasi. CCM walizoea kujiita nambari wani sasa nambari wani imegeuka kuwa nambari chafu ndo mashabiki wake munaanza kuleta wazo jipya la kuchagua mtu.

Kwa tunaojua kufuatilia mambo, tulishauona mwisho wa CCM. Kwa demography hii wanaoabudu CCM wako 'kiduchu'.
 
Mwaka huu mzuri Mdini FaizaFoxy kabadilika na kuongea point , badala ya kusifia Kikwete tu , nafkiri zama za kumponda Baba wa Taifa zimeisha tugange yajayo ya kuwa safari hii ni zamu ya Wakristo kutoka Zanzibar na Zanzibar kuna Jaji Augostino Ramadhani, ni mwadilifu na Kiongozi mzuri asiye na kashifa na umri wake unaruhusu kwa kuwa kastaafu juzi tu.
 
Hapana mkuu!
Huyu ni mnafiki hana mapenzi na chama,kachungulia maazimio ya CC kaona wa dini yake kuteuliwa CCM ni vigumu ndo maana anakuja hapa na ngonjera za kuchagua mtu wala sio chama!
kwake yeye uislamu kwanza mengine badae....UKAWA wakimsimamisha muislamu anawaunga mkono!
yaani huyu twaweza kumuita CONDOMU au TOILET PAPER
haa haa umeshamgundua eeh!
 
Uwanja ni wako na una haki ya kubwabwaja na kuhororoja upendavyo.

Slaa alibwagwa na Kikwete na kwa maadili mabovu aliyonayo huyo atakuwa ni chaguo lako lakini nnauhakaika hatokuwa chaguo la Watanzania wengi wanaopenda maadili mema.

Mimi sitomchaguwa Slaa hata akibaki kuwa ni mgombea pekee.

Kwahiyo ww na team LUMUMBA ndio Mlituletea Huyu rais dhaifu
Na sasa unakuja na sera yako hii ya UCCHAGUE CHAMA CHAGUA MTU. hii inadhihirisha tayari umeanza kuipiga kibuti CCM yako iliyokufundisha usanii.
Ngoja tuone safarihii utampigia debe nani na akihama ccm unahama nae
 
Nnamaanisha wapo kwenye vyama wanaoamini kuwa wao ndiyo wenye vyama na maamuzi yao ni ya mwisho. Na wapo wanachama wanaoamini kuwa hivi vyama vina wenyewe. Hilo linatokea sana kwenye vyama vyetu. Mfano mzuri ni kura za maoni na nimeelezea juu huko, kaisome vizuri post namba moja.
bado hujaeleweka kamwe! Je ndani ya chama nani mwenye chama? Maana chama ni wanachama! Kwa mfano wenye ccm ni wanaccm. Sasa tatizo ni nin?
 
FaizaFoxy
===>Kuna wakati na wewe huwa unakuwa unawaza vizuri,nakuomba uache kula sana Ugoro kabla ya kuchangia hapa JF,
Hongera sana kwa mawazo mazuri.
 
Last edited by a moderator:
Chama si kama underwear kuwa unabadili hata kama haijakuwasha. Sijawahi kuchaguwa kiongozi kwa ajili ya chama chake, nachaguwa kiongozi kwa uwezo wake.

CUF ikimsimisha Lipumba siwezi kumchaguwa, huo ndiyo ukweli, Lipumba angebaki kwenye fani yake tu ya Uchumi wa Kimataifa.

Wakati huohuo kwa upande wa ukawa simuoni mwengine anaemzidi uwezo Lipumba mpaka dakika hii.
contradictions!! Sitaki nataka.
 
Huo ni uzalendo na unaonesha jinsi Tanzania tunavyoweza kufanya maamuzi bila ya kuburuzwa na chama au wenye chama.

Tukianza kuchaguwa viongozi na si chama tutakuwa sisi wenyewe tumeshakuwa viongozi.

Ni wakati muafaka sasa Watanzania tusikubali kuchaguwa wamtakae wenye vyama, tunataka tuwe na viongozi tuwatakao wananchi tulio wengi.

Nina kunukuu, "Huo ni uzalendo....Tukianza kuchaguwa viongozi na si chama tutakuwa sisi wenyewe tumeshakuwa viongozi." Mwisho wa kukunukuu.

Umeandika kizalendo, hasa wananchi wakijitambua kwamba wao wenyewe ni viongozi.Tuanze kwa vitendo mwaka huu 2015 Oktoba....
 
bado hujaeleweka kamwe! Je ndani ya chama nani mwenye chama? Maana chama ni wanachama! Kwa mfano wenye ccm ni wanaccm. Sasa tatizo ni nin?

Ingawa naona upo shallow sana kwa kutonielewa juu ya kukuelewesha kote huko, ngoja nitumie njia nyingine ya kukuelewesha;

Umeshawahi kuwa na wadhifa upi kwenye chama chako?
 
Kwahiyo ww na team LUMUMBA ndio Mlituletea Huyu rais dhaifu
Na sasa unakuja na sera yako hii ya UCCHAGUE CHAMA CHAGUA MTU. hii inadhihirisha tayari umeanza kuipiga kibuti CCM yako iliyokufundisha usanii.
Ngoja tuone safarihii utampigia debe nani na akihama ccm unahama nae

Kikwete ni "chaguo la Mungu" -Askofu Kilaini.

Kutakuwepo tu na "chaguo la Mungu" lingine, wala usiwe na kiherehere.
 
contradictions!! Sitaki nataka.

Hujamfahamu huyo dada kwa uislam, huwa hana agenda nyingine, ameona chama chake hakina mgombea muislam mwenye mvuto, sasa anajifanya yeye hajali chama. Akiwekewa Lipumba na UKAWA huyu atamchagua. Yeye akili yake imeegemea dini tu.
 
Back
Top Bottom