Watanzania kabla ya kuanza mradi wa Bandari ya Bagamoyo tafuteni Articles za 'Lesson from Sri Lanka Hambantota Port'

Hiyo ni sehemu ya bandari tu

Kwenye viwanda serikali wala hawajawapa masharti hayo wawekeze tu kama wawekezaji wengine ata kesho.

Wao ndio hawataki kwa sababu wanataka raia wataoenda kufanya kazi hizo sehemu wasisumbuliwe kupata vibali vya kazi, viwanda vipewe maji na umeme kwa bei nafuu na tax holidays.

Sasa ukishafanya ivyo na machine zake za kuzalishia ajalipia kodi hata huyo Bakhresa ataweza shindana nae kwenye low prices.

Muwe mnafikiria vitu mnavyotetea Magufuli is dead Tanzania lives on; chuki kwakwe zisiwape upofu what is at stake kwenye huu mradi nchi ikikubali kila takwa la mchina.
Sasa mkuu EPZ zote tax holidays lazima,kuleta miundombinu ni jukumu la serikali sio mwekezaji,kwa mfano unatoa tax holiday kwa viwanda vya mbolea na usindikaji Mazao ya kilimo ,hapo huoni umeongeza value kwenye mnyororo wa thamani?

Economic benefits sio Kodi tuu na ajira
 
Mkuu 'macho_mdiliko'
Nami nilitaka kuanzisha mada juu ya hii 'project' ya Bagamoyo, lakini zimekuwepo nyingi kiasi kwamba huenda mada nitakayoanzisha itaishia kwenye kuunganishwa na hizi ndefu na kuishia bila kusomwa.

Ni dhahiri, mradi huu una makundi yenye maslahi wanaouchochea kuupa nguvu, hasa hawa wa upande wa wachina, bila kujali maslahi ya Tanzania.

Mimi ningependa kuuliza na kupata maoni ya wachangiaji juu ya ugumu wa mradi huu kuufanya uwe wetu halafu tuwakaribishe wawekezaji wafanye wanavyotaka kuwekeza kwenye mradi wetu.

Hapo majirani Kenya na mradi wao wa Lamu wameuanzisha wenyewe, baada ya kuona kwamba wakitegemea wawekezaji ndio wauanzishe, huenda mradi huo usiwepo kabisa.

Kenya wamejenga Ghati tatu sasa; moja iko tayari na mbili hazipo mbali. Bandari inaweza kuanza kufanya kazi, na atakayetaka kwenda kuwekeza hapo kwa kujenga ghati nyingine, hadi zitimie 32, anakaribishwa.

Bagamoyo, kwa hakika ina sifa tofauti zaidi ya Lamu, sifa zinazovutia kwa uwekezaji; kama hali ya usalama, na ukaribu zaidi na nchi zitakazotumia bandari hiyo.

Je, sisi hatuna uwezo, hata kama utakuwa ni kukopa, kuanza ujenzi wa ghati chache hapo Bagamoyo, na wakati huo huo tukiiuza kwa wawekezaji, hata hao wachina waje kuwekeza, kama wanavyotaka kuwekeza sasa?

Mpangilio huu utakuwa na masharti tofauti na haya tunayokabiliana nayo wakati huu na huyu mwekezaji anayetaka bandari iwe ya kwake.

Nadhani katika hoja zinazotolewa kwenye mijadala hapa ukumbini, kuna mambo pia watu wanayasahau kwamba yapo.
Kwa mfano: Mchina hawekezi kwa asili mia katika mradi wa Bagamoyo, yeye anazo asili mia kadhaa atakazowekeza kwenye mradi huo, na yeye atatafuta wawekezaji wengine waje wawekeze chini ya himaya yake.

Mchina hatoi hiyo $30 bilioni, siku tutakayomkubalia kuwekeza hapo. Mu-Oman yeye za kwake zinajulikana ni asili mia kumi za mradi unaopangwa hapo, na hata sisi Tanzania tukisema tuwekeze zaidi ya hicho kiasi cha mchango wa ardhi kitakachohesabika kuwa ndizo hisa zetu katika uwekezaji, hilo pia linawezekana (sijaona popote linapokatazwa). Hata matajiri wetu hapa, akina Bakhresa, huenda watajitosa kuwekeza wakitaka, lakini kwa kwa hali ya sasa, uwekezaji huo utakuwa ni chini ya himaya ya mchina na siyo yetu (Tanzania).

Ninachoomba kujuwa, kuna tatizo lipi la kuufanya mradi huo uwe wetu? Bila shaka majibu mengi yatahusu hilo la uwezo wetu kujenga hizo ghati za mwanzo, lakini mbona Kenya wameweza?

Wengine watahoji tutawapataje wawekezaji ambao bado hawajaonekana Lamu - ukweli hapa ni kwamba Bagamoyo inauzika sana, ndiyo maana wachina hawabanduki kwenye mradi huo, vinginevyo ungekwishasikia wamekimbilia Lamu au kwingine.

Kama hatutaweza kupata mkataba wenye maslahi stahiki kwa nchi yetu, napendekeza, tuwe jasiri, tuuanzishe huu mradi wenyewe, halafu , kama tunavyofanya juhudi za kuwakaribisha wawekezaji nchini mwetu kwenye sekta hizi nyingine, tuweke jitihada kubwa za kutafuta wawekezaji kokote watakakopatikana, waje wawekeze kwenye eneo hilo kama ilivyopangiliwa katika uwekezaji wa sasa.
Na mchina lengo lake hasa ni hapo kwenye bandari, maana anajua atafanya ufirauni wote hapo bila mamlaka za nchi kujua kinachoendelea.......
 
Na mchina lengo lake hasa ni hapo kwenye bandari, maana anajua atafanya ufirauni wote hapo bila mamlaka za nchi kujua kinachoendelea.......
Kwa hiyo mkuu wangu 'nyumisi' unasemaje, hatuwezi kamwe tukaaanza kwa kujikongoja kuuanzisha mradi huu sisi wenyewe?
Kwa nini tusiwe jasiri kidogo, tuseme huu mradi ni wetu!
 
Swala la bandari ya Bagamoyo hilo halina ubishi lazima ijengwe; Dar aiwezi kuwa expanded anymore it’s reaching its saturation point.

So either Bagamoyo
anajenga mchina au Tanzania; upande wa serikali wao walilenga kulinda mapato yao yasipotee vile.

Icho ndio ilichokuwa inataka serikali iliyopita win win situation.
Tunayo nafasi ya Bandari ya Mwambani Tanga, pia ya Tanga Mjini na pia ya Mtwara , Bagamoyo ikawa ni ya "kutambika"
 
Sasa mkuu EPZ zote tax holidays lazima,kuleta miundombinu ni jukumu la serikali sio mwekezaji,kwa mfano unatoa tax holiday kwa viwanda vya mbolea na usindikaji Mazao ya kilimo ,hapo huoni umeongeza value kwenye mnyororo wa thamani?

Economic benefits sio Kodi tuu na ajira
Na hizo machine zake halipii kodi kuziingiza, wakati Kagera sugars mitambo yao ilikwama bandarini kisa kodi.

Imagine sasa kama mchina nae anajenga kiwanda cha sukari huyo Mtibwa na Kagera sugars watashindana na kiwanda ambacho mitambo yao wameingiza bila ya kulipia ushuru na wanapata capital allowance and before we forget wana tax holiday.

Now put that scenario kwa kila kitu kitakacho zalishwa hapo kuna kiwanda cha Tanzania kitashindana nao kwenye bei sokoni? Bado ujaweka low production costs za umeme, maji, ardhi wamepata bure na wala awataki kulipa land fees.

We unadhani wao wajinga kutaka hiyo industrial park iwe sehemu ya mkataba wa bandari.
 
Tunayo nafasi ya Bandari ya Mwambani Tanga, pia ya Tanga Mjini na pia ya Mtwara , Bagamoyo ikawa ni ya "kutambika"
Critics might argue unreability ya miundombinu kufanya hizo sehemu kuwa easily accessible na nchi kama Congo, Uganda, Rwanda na Burundi
 
Ata wale waliopo bungeni wanaushadsdia kwasababu walienda ziara siku 21 huko nje na wapo kwenye kamati ya miundombinu wakalishwa presentation ya nusu saa hivi then wakapitishiwa mlungula ndiyo waliporudi kila mtu anantaka uendelee ule mradi alafu wanasema Wachina wanataka kuisadia nchi yetu!

Sent using Jamii Forums mobile app

Mambo mengine bwana... Kama mradi ni kwa faida yetu waTZ, sasa kwanini waChina ndio wawaite nchini kwao na kuwa convince kuwa mradi ni kwa faida ya TZ. Ideailikuwa ya kwao au yakwetu? Kwanini msingeibua mradi nyie waTZ na kuu present kwao na kuwahakikishia kuwa ni winwin situation, wote tutafaidika?
 
Kwa hiyo mkuu wangu 'nyumisi' unasemaje, hatuwezi kamwe tukaaanza kwa kujikongoja kuuanzisha mradi huu sisi wenyewe?
Kwa nini tusiwe jasiri kidogo, tuseme huu mradi ni wetu!
Na mimi ndo ulikuwa mtazamo wangu, kwa sababu kwa sasa hatuna pressure kubwa kwenye swala la bandari. Bandari za Dar, Tanga, Mtwara zimeshapewa pesa kwa ajili ya expansion, Ya Dar tayari imepiga hatua kubwa kwa kuongeza gati hadi zitafika 13. Kwa hiyo nilitegemea nchi ingeanza uwekezaji kwenye bandari ya bagamoyo kwa pesa zake yenyewe na mikopo ili ipate starting point kabla wawekezaji wengine hawajaja....
 
Na hizo machine zake halipii kodi kuziingiza, wakati Kagera sugars mitambo yao ilikwama bandarini kisa.

Imagine sasa kama mchina nae anajenga kiwanda cha sukari huyo Mtibwa na Kagera sugars watashindana na kiwanda ambacho mitambo yao wameingiza bila ya kulipia ushuru na wanapata capital allowance and before we forget wana tax holiday.

Now put that scenario kwa kila kitu kitakacho zalishwa hapo kuna kiwanda cha Tanzania kitashindana nao kwenye bei sokoni? Bado ujaweka low production costs za umeme, maji, ardhi wamepata bure na wala awataki kulipa fees.

We unadhani wao wajinga kutaka hiyo industrial park iwe sehemu ya mkataba wa bandari.
Hayo ya kodi yanajadilika ,Kuhusu ushindani hayo ni mambo ya biashara,afu sijui kama unajua uchumi,Rostam alienda kuwekeza Kenya no way out Tzn itanufaika isipokuwa host country kwa hiyo Mchina akiwekeza still wanufaika ni sisi sio China.

Wao faida yao ni kutafutia watu wao ajira na ile volume ya biashara baina ya Nchi ndio nchi itanufaika kwenye external trade
 
Kuna watu wanajiona wajanja kwenye hili kisa wametanguliza maslahi yao, hii inaweza kuleta political crisis ambayo haijawahi kushuhudiwa......hapo mchina amedinda na mkataba wake wa miaka 99 hasikii la mtu.
Kiasi flani akili ya waTZ na uelewa kuhusu matumizi ya kodi zao umefunguka. Asipokuwa makini atakuja kuwa infamous leader (sipendi kutumia neno hili). Anatakiwa ajue, wananchi wanam banchmark na leaders waliopita, hasa yule aliyemrithi.
 
Mambo mengine bwana... Kama mradi ni kwa faida yetu waTZ, sasa kwanini waChina ndio wawaite nchini kwao na kuwa convince kuwa mradi ni kwa faida ya TZ. Ideailikuwa ya kwao au yakwetu? Kwanini msingeibua mradi nyie waTZ na kuu present kwao na kuwahakikishia kuwa ni winwin situation, wote tutafaidika?

China ni ndugu zetu wanatujali sana
 
Mkataba uwekwe wazi wote (warts and all terms and conditions and small prints). Hakuna mkataba mzuri wenye manufaa kwa Mtanzania, utakao pingwa na Majority ya Watanzania.

Switzeland wana utaratibu wa kupiga kura kwa mambo yote makubwa, ya msingi ya taifa. Hili ni jambo kubwa, la msingi sana.

Ni muhimu kujua kama usimamizi, ukaguzi, kodi, Bandari za Dar, Tanga, Mtwara zitaathirika kufaidika vipi? Zitakufa?

Miaka mingapi wanapewa kuimiliki, ajira ngapi zitakuwa kwa Watanzania, deni (kama litakuwepo), upande mmoja ukikiuka, ukivunja masharti / makubaliano nani atakuwa msuluhishi, adhabu gani zitahusika. Who is going to enforce those penalties.

Rushwa, mikataba mibovu inazibitiwa vipi? Miradi yote mikubwa huwa kuna risks kubwa sana rushwa kukithiri.

Kukiwa na uwazi unaweza kupunguza Rushwa.
Mwanga (uwazi) hufukuza giza ( rushwa, mikataba mibovu, upigaji).

Hii issue iangaliwe kwa maslahi mapana ya Taifa, na vizazi vijavyo.
Idea nzuri bro,,lakini kweli unipange mm Waiter kwenye foleni ya kupigia kura bandari yenye viwanda 190,obviously kura yangu nitaipigia ndio....ndo maana tukachagua wabunge,kama hawajielewi nchi itapotea
 
Hayo ya kodi yanajadilika ,Kuhusu ushindani hayo ni mambo ya biashara,afu sijui kama unajua uchumi,Rostam alienda kuwekeza Kenya no way out Tzn itanufaika isipokuwa host country kwa hiyo Mchina akiwekeza still wanufaika ni sisi sio China.

Wao faida yao ni kutafutia watu wao ajira na ile volume ya biashara baina ya Nchi ndio nchi itanufaika kwenye external trade
Kuhusu kodi laxima wachukue tax holiday kwa miaka nenda rudi! Nukk Sri Lanka wachina hawatalipà kodi kwa miàka 32!! Ajira watakazotengewa watanzania ni ukuli yaani wabeba mizigo bandarini. Nafasi muhimu watashika wachina!!
.
 
Kuna watu wanajiona wajanja kwenye hili kisa wametanguliza maslahi yao, hii inaweza kuleta political crisis ambayo haijawahi kushuhudiwa......hapo mchina amedinda na mkataba wake wa miaka 99 hasikii la mtu.
Political crisis utaifanya wewe labda.

Tena utaifanyia humu JF.
 
Mradi wa Hambatota ni mkopo tofauti namradi wa Bagamoyo Special Economic Zone ambao ni uwekezaji wa pamoja kati ya China, Oman na Tanzania ambapo sisi tunatoa ardhi. Kwa vyovyote vile hata mradi ukiwa na hasara sisi hatuhusiki kwenye hiyo hasara.

Mada kama hizi ndio zinasababisha wengine tuamini mnaopinga mradi huu hamna akili ya kuchanganua mambo makubwa kama haya ila mnalazimisha msikilizwe japo hamna nguvu ya hoja.

hamuhusiki kwenye hio hasara? ujinga mzigo sana
 
Hujasikia plan ya SGR Tanga kuelekea huko unakosema, maana hata Bwagamoyo hawa hiyo miundo mbinu
Hiyo kwakweli sijasikia, kama kuna hiyo mipango inaongeza kesi ya Tanga kudai bandari kubwa. Either way Bagamoyo kwa mazingira ya sasa ina supporting infrastructures so kuna strong case kwa mazingira ya leo.
 
Back
Top Bottom