Wasomi na kiingereza

Wasomi na kiingereza

11 Apr 2020
Dr. Mwakyembe - "Tukifundisha Kiingereza vizuri kama lugha ya kigeni, Kiswahili kitakuwa na Kiingereza tutakimudu zaidi"

Kuna wanaositasita kwamba tukitumia #Kiswahili katika mfumo wote wa elimu, tutaua Kiingereza. Kiingereza kipi? Kiingereza kibovu? Tukifundisha Kiingereza vizuri kama lugha ya kigeni, Kiswahili kitakuwa na Kiingereza tutakimudu zaidi. Tutaondoa kukariri. – Waziri Mwakyembe
Source : Durusu Kiswahili
 
21 Feb 2020
“Huwezi kujifunza utamaduni bila kufahamu lugha”, Carly Lucas.

Mbali na kwamba alitoka Marekani hajui hata neno moja la Kiswahili, sasa amebobea katika Kiswahili na Kimaasai. Msikilize.

Source : Durusu Kiswahili
 
Kama lugha ya wenyewe wanaisomea nini
Kiingereza ni lugha ya dunia
Ulishawahi funua vitabu vya aanafunzi sekondari na chuo?
Kuisomea haimanishi tuiongee!!! Mbona Kuna nchi nyingi hawatumii hiyo lugha na mambo yanaenda ni ujinga tu kuamini kuongea kingereza ndo kusoma
 
12 Oct 2019

Makosa ya tafsiri: Kufunguka, kwenda kwa jina, zoezi la

  • Kufunguka juu ya...
  • Anakwenda kwa jina...
  • Zoezi la kujiandikisha...
  • Sakafu ya moyo...
  • Kesi ya kwanza ya Ebola..
  • Kimbiza mgonjwa hospitalini...
  • Chukua tahadhari...
  • Siku zako zimehesabiwa....
  • Simama ufanye mazoezi ....
Je, wajua kwamba kauli hizo si sahihi na ni kutokana na tasfiri chapwa ya Kiingereza? [At the end of the day, open up, goes by the name na exercise] Msomi wa tafsiri Prof. Hermas J.M Mwansoko anaelezea makosa mengine yaliyoshamiri na kuhimizi kuwe na tungo asili za Kiswahili zisizoegemea muundo wa Kiingereza.

Source : Durusu Kiswahili
 
Nakisitikia kichwa chako kilichobeba ubongo wako,hakuna kitu, ni mzigo tu.
Few Tanzanian citizens

Huu ndio uwezo wako wa Kuandika, Wewe huna uwezo wa kuongea Kiingereza, Kwa uandishi huu umesoma shule za kata

Unatafsiri kiswahili kwenda Kiingereza sio sahihi

ukisema Mtanzania au Raia wa Tanzania hakuna utofauti

ukisema huyu mkenya au Raia wa Kenya hakuna utofauti

wewe ulisikia wapi "Noun na Noun" zikafuatana

Mimi kwa kuishi kwangu kote nje lugha ya Kiingereza inapishana kwa kila mtu

Kuna wazungu wa Irish wanatamka lugha ya Kiingereza kama neno linavyoandikwa kwa mfano Food wao wanasema Foooood, Huku watu wa mjini London wanasema Fud

Hata kiswahili hakuna anayeongea kwa ufasaha hapa Tanzania, Wakenya wanatuona sisi hatuna uwezo wa kufundisha kiswahili kwa wageni au mataifa na vyuo vikubwa kwani hatujui kiswahili fasaha cha darasani

Je wewe lugha umefundishwa na mtu wa nchi gani Australia, Ireland, America au Britain

Wazungu kutoka Britain nao hawaongei lugha sahihi

Marehamu Benjamin Mkapa hakuwa mzungu lakini alikuwa anaongea lugha kwa ufasaha kwa kufuata kanuni za muundo na miundo kuliko wazungu

Mfuatilie Ben Mkapa ndio unaweza ukajifunza lugha toka kwake

Wazungu wenyewe wanaongea lugha za mitaani mfano hiyo is you coming ni kawaida sana ukiwa London kama sisi neno mambo
 
Kutoiongea sio tatizo, tatizo ni kulazimisha kuiongea huku tukiwa tunaiongea hovyo sana. Bora tusingekuwa tunaiongea kabisa.
Kuisomea haimanishi tuiongee!!! Mbona Kuna nchi nyingi hawatumii hiyo lugha na mambo yanaenda ni ujinga tu kuamini kuongea kingereza ndo kusoma
 
Kiungereza sio kachumbari Tanzania, ni lugha ya kufundishia ambayo kwa mtu aliyefika angalau kiwango cha digree atakuwa ameitumia kwa miaka 10. Kama kilikushinda miaka hiyo yote ulikuwa unasomaje na utawezeje kazini? Hembu tumia akili zako.
Tanzania lugha ya Kiingereza ni mojawapo ya lugha ya taifa kiofisi sambamba na Kiswahili...
 
Kwa bahati mbaya sana, vijana wa sasa hapa Tz sio tu wanashindwa kuzungumza au kuandika Kiingereza:- Hata Kiswahili wanachoandika au kukiongea mara nyingi sana kina makosa. Ukitaka kujua tatizo ni lugha (iwe Kiswahili au Kiingereza), pitia tu mambo watu wanayoandika wanapochangia mada kwenye mitandao.

a) WENGI SANA hawawezi kutofautisha kati ya herufi L na R. Unamsikia mtu anasema "nilipokuwa nachumbia mahari ambapo mahali ilipelekwa ni kwa mjomba"

b) Ni Watanzania wengi (hata baadhi ya viongozi wanasiasa) wanasema:- "Tangia sasa...." wakimaanisha kuanzia sasa. Hawajui wangepaswa kusema "Tangu sasa", au "kuanzia sasa"

c) Wapo pia watu wengi ambao hawajui the difference between a subject and a predicate (samahani kwa kuchanganya kimombo ndani maana hata mimi yapo maneno ya Kiswahili siyajui - kwa mfano subject and predicate). Nilitaka kusema kwamba watu wengi "wanachanganya mambo" wakati wanazumgumzia mambo mawili tofuati.

Kwa mfano mtangazaji wa habari anasema:- 'Lile gari lilimgonga mtu na kufa" Maana ya mstari huu ni kwamba gari ndio lilikufa. Angetaka kusema mtu ndie kafa angesema "lori lilimgonga mtu akafa"

d) Makosa yapo mengi tu kwenye Kiswahili kinachozungumwa na baadhi ya wasomi wa Tanzania. Kosa lingine ni pale mtoa habari anaposema:- "Alipigwa risasi akaweza kufa" badala ya kusema alipigwa risasi akafa. Unaposema mtu ameweza kitu fulani una maana hicho ni kitu ambacho alikuwa anataka akipate na akajitahidi mpaka akakipata. Hivyo sio sawa kusema mtu aliyepigwa risasi aliweza kufa maana hakuwa anajitahidi kufa.

So, my question to your dear readers is this:- If we can make SO MANYA MISTAKES in Kiswahili which is our mother tongue, do you expect us to be proficient, and efficient in making utterences in a foreign language? No way ! CIAO !
 
Kuna sababu nyingi watanzania hatujui kiingereza, pamoja na kukisoma kuanzia form one.

Kujua lugha yoyote ile inahitaji "practice". Sisi ukishatoka darasani/shule huko nyumbani ni kiswahili au lugha za asili kwenda mbele.

Hatuna utamaduni wa kujisomea vitabu si vya kiingereza wala kiswahili, movie nazo siku hizi zimetafsiriwa uongo na wanaojiita madj. Sababu ziko nyingi.

Lakini mtu kutokujua kiingereza haimaanishi kuwa hana akili wala ufahamu.
 
Kuna Technical English and Fluency English. Watu wanao soma sayansi wanatumia Technical English sana. Hivyo ukiwaingiza kwenye fluency hawatakuelewa. na wewe wakiungiza kwenye technical hutowaelewa. Watu wanaosoma arts ndio wanatumia fluency English, sana ila nao technical English holaaaa
Mawasiliano ni mawasiliano tuu.. hakuna technical way ya kuomba chumvi au kumsalimia mtu Barabarani kiongozi... 🙂 Ni kama kujaribu kutafuta sababu ili uvae chupi kichwani na blauzi kiunoni..

Iko namna sahihi inayokubalika generally ya kuwasiliana.. kwa matamshi au maandishi.. Japo sikatai pia tuna Technical Language ambayo ni tofauti kutokana na Taaluma moja hadi nyingine.

Tatizo letu hasa sisi watanzania ni wavivu sana.. ukisha fundishwa darasani hutaki kuendelea kujifunza na kukiboresha mwenyewe kile ulichojifunza. Kujua matumizi sahihi kulingana na maeneo na tamaduni.. tunaakomaa na kusoma kile cha kufanyia mitihani tuu...

Matokeo yake hata uwezo wa kusoma hadithi ya kiswahili(sio kizungu) na kuelewa general idea, na kupata tafsiri fupi ya maudhui na lengo inamshinda mtu wa chuo kikuu..(graduate)

Mtu anashindwa kusikiliza hotuba na kuchukua minutes zenye mashiko.. matokeo yake ufupisho wake unakuta amenakili kila kitu kilichosemwa na ameshindwa hata kung'amua context ya Msemaji na alilenga kuwaambia nini hadhira.

Na kikubwa kinachotukamata tukiwa shule utasikia mtu wa PCM anawaambia Watu ungwini peleka huko.. wana Lugha anacrash Sayansi na wa ECA anadharauliwa/kudharau wote..

Mwanasayansi na Mtunza fedha wanahitaji basic skills za Mawasiliano effective... Mtunza fedha na Mtu wa Lugha wanahitaji analytical skills, hata mwanasayansi na Mtu wa Lugha wao pia wanahitaji kujua mahesabu ya fedha.

#Tusitafute sababu ya kutokuandika au kusema matamshi kwa ufasaha.. hiyo ni kosa tuu.. na lack.of Discipline for the general population# Lugha ni tools muhimu sana.. lazima zitunzwe na kuzitunza ni pamoja a kuzitumia kwa ufasaha
 
Kwa bahati mbaya sana, vijana wa sasa hapa Tz sio tu wanashindwa kuzungumza au kuandika Kiingereza:- Hata Kiswahili wanachoandika au kukiongea mara nyingi sana kina makosa. Ukitaka kujua tatizo ni lugha (iwe Kiswahili au Kiingereza), pitia tu mambo watu wanayoandika wanapochangia mada kwenye mitandao.

a) WENGI SANA hawawezi kutofautisha kati ya herufi L na R. Unamsikia mtu anasema "nilipokuwa nachumbia mahari ambapo mahali ilipelekwa ni kwa mjomba"

b) Ni Watanzania wengi (hata baadhi ya viongozi wanasiasa) wanasema:- "Tangia sasa...." wakimaanisha kuanzia sasa. Hawajui wangepaswa kusema "Tangu sasa", au "kuanzia sasa"

c) Wapo pia watu wengi ambao hawajui the difference between a subject and a predicate (samahani kwa kuchanganya kimombo ndani maana hata mimi yapo maneno ya Kiswahili siyajui - kwa mfano subject and predicate). Nilitaka kusema kwamba watu wengi "wanachanganya mambo" wakati wanazumgumzia mambo mawili tofuati.

Kwa mfano mtangazaji wa habari anasema:- 'Lile gari lilimgonga mtu na kufa" Maana ya mstari huu ni kwamba gari ndio lilikufa. Angetaka kusema mtu ndie kafa angesema "lori lilimgonga mtu akafa"

d) Makosa yapo mengi tu kwenye Kiswahili kinachozungumwa na baadhi ya wasomi wa Tanzania. Kosa lingine ni pale mtoa habari anaposema:- "Alipigwa risasi akaweza kufa" badala ya kusema alipigwa risasi akafa. Unaposema mtu ameweza kitu fulani una maana hicho ni kitu ambacho alikuwa anataka akipate na akajitahidi mpaka akakipata. Hivyo sio sawa kusema mtu aliyepigwa risasi aliweza kufa maana hakuwa anajitahidi kufa.

So, my question to your dear readers is this:- If we can make SO MANYA MISTAKES in Kiswahili which is our mother tongue, do you expect us to be proficient, and efficient in making utterences in a foreign language? No way ! CIAO !
Lack of Discipline.
Na kudhani Elimu is nothing so we can take failures for teachers...
 
Kuna Technical English and Fluency English. Watu wanao soma sayansi wanatumia Technical English sana. Hivyo ukiwaingiza kwenye fluency hawatakuelewa. na wewe wakiungiza kwenye technical hutowaelewa. Watu wanaosoma arts ndio wanatumia fluency English, sana ila nao technical English holaaaa
Acha kutetea ujinga, Kiingereza ni majanga kwa graduates...

Sent from my TECNO L9 Plus using JamiiForums mobile app
 
Inakuwaje msomi ama graduate wa chuo kikuu aliespend miaka kama minne chuo kikuu na ana degree,masomo yake yote ni kiingereza tupu anafanikiwa kugraduate, lakini ukimwongelesha kiingereza haelewi

Akiamua yeye sasa Hata kuandika ujumbe kwa kiingereza anashusha broken ya hatari hadI unashangaa?
Wengine wamefanikiwa kupata kazi kabisa unakuta bonge la engineer from ardhi university English mbovu mkichat yuko kwenye bonge la kampuni

Mbaya zaidi graduate kamaliza chuo few days anaambiwa andika barua ya kuomba internship anaweweseka..Mara nipe google..maelezo yake binafsi yanamshinda kujieleza kwa kiingereza anatafuta CV za wengine akopi.sasa najiuliza huyu mtu kafanikiwa kumaliza successful report zake aliandikaje?kama kiingereza cha kuandika anababaika presentation alihudhuriaje akapata marks
Research zake?

Au ndo wale wa kukariri? Sawa basi hata kama kukariri unashindwa kujifunzia hapo mpangilio wa grammar.

Boss mzima ananitext "is you coming or no"
Kiingereza nacho ni kipaji?
Sio kila mtu anaenda kusoma Semantic chuoni bro au English structure au Language morphology na phonology au phonetics.
 
Kwakweli..
Ila mbona Mimi nimepata kujua kiingereza fasaha kupitia shule ya msingi tena enzi za mkapa..na sio mhitimu chuo kikuu

Kuna uhusiano gani kati ya mtu Na mtu kwenye ubongo wake?
Waziri na mwalimu?
Unajia kizungu au unajifanya unajua?
 
Back
Top Bottom