Wasomi na kiingereza

Miss Champagne

JF-Expert Member
Sep 2, 2020
2,155
6,303
Inakuwaje msomi ama graduate wa chuo kikuu aliespend miaka kama minne chuo kikuu na ana degree, masomo yake yote ni kiingereza tupu anafanikiwa kugraduate, lakini ukimwongelesha kiingereza haelewi

Akiamua yeye sasa Hata kuandika ujumbe kwa kiingereza anashusha broken ya hatari hadI unashangaa? Wengine wamefanikiwa kupata kazi kabisa unakuta bonge la engineer from ardhi university English mbovu mkichat yuko kwenye bonge la kampuni

Mbaya zaidi graduate kamaliza chuo few days anaambiwa andika barua ya kuomba internship anaweweseka..Mara nipe google..maelezo yake binafsi yanamshinda kujieleza kwa kiingereza anatafuta CV za wengine akopi.sasa najiuliza huyu mtu kafanikiwa kumaliza successful report zake aliandikaje?kama kiingereza cha kuandika anababaika presentation alihudhuriaje akapata marks
Research zake?

Au ndo wale wa kukariri? Sawa basi hata kama kukariri unashindwa kujifunzia hapo mpangilio wa grammar.

Boss mzima ananitext "is you coming or no"
Kiingereza nacho ni kipaji?
 
Kuna Technical English and General Fluency English. Watu wanao soma sayansi wanatumia Technical English sana. Hivyo ukiwaingiza kwenye General fluency hawatakuelewa. na wewe wakiungiza kwenye technical hutowaelewa. Watu wanaosoma arts ndio wanatumia General fluency English, sana ila nao technical English holaaaa
 
Kuna Technical English and Fluency English. Watu wanao soma sayansi wanatumia Technical English sana. Hivyo ukiwaingiza kwenye fluency hawatakuelewa. na wewe wakiungiza kwenye technical hutowaelewa. Watu wanaosoma arts ndio wanatumia fluency English, sana ila nao technical English holaaaa

Kwa kuonyesha msisitizo angeandika thread kwa kiingereza.

Humu watu wanaopiga NGELI baadhi ni Kiranga na Nyani Ngabu
 
Kuna Technical English and Fluency English. Watu wanao soma sayansi wanatumia Technical English sana. Hivyo ukiwaingiza kwenye fluency hawatakuelewa. na wewe wakiungiza kwenye technical hutowaelewa. Watu wanaosoma arts ndio wanatumia fluency English, sana ila nao technical English holaaaa
Nipe mfano wa technical English na fluency english
 
That's why wataalam wetu wengi uwezo ni mdogo na vijana hawaajiriki! hauwezi ukawa mbobezi wa jambo flani ilhali lugha uliyotumia kusomea jambo husika inakupiga chenga.
Ni kweli kabisa yani
Unakuta anaandika hata barua kwa kiingereza broken anaishia kulalamika ajira hamna
Watu wakicheki ulichoandika wanapata picha hata kichwani uko shallow kiasi gani..halafu hao ndo wakupe nafasi inayohitaji mtu kichwa kigumu kuingia kwenye competition na kampuni nyingine.hapana
 
Abigail.
Kama waziri wa elimu hajui kiingereza unategemea mwanafunzi au hata mwalimu kwenye shule zilizo chini ya huyo waziri ajue kiingereza?
Kwakweli..
Ila mbona Mimi nimepata kujua kiingereza fasaha kupitia shule ya msingi tena enzi za mkapa..na sio mhitimu chuo kikuu

Kuna uhusiano gani kati ya mtu Na mtu kwenye ubongo wake?
Waziri na mwalimu?
 
Back
Top Bottom