Wasomi na kiingereza

Wasomi na kiingereza

siku mkiacha utegemezi,mtakuwa mmejikomboa sana.

kiingereza safi sio kielelezo cha usomi wa mtu,ndio sababu mnatapeliwa kizembe na wajanja wajanja,ukilazimishwa kukijua kiingereza katika mazingira yako utakijua tu utake usitake.

hiyo ni lugha tu,labda tuangalie output ya msomi husika sasa badala ya lugha ya kiingereza na bla bla zingine.
kiingereza sio lugha rasmi ya kusomea shule za msingi,inakuja kuwa lugha rasmi ya kusomea sekondary,ambako ni wazi sasa mtu wakati huu anachukua ujuzi,sijui nini cha ajabu hapa!!!
 
Lugha na uwezo wa kuwasiliana kwa ufasaha ni muhimu sana. Ndio njia pekee uwezo na ujuzi alionao mtu unaweza kudhihirika, kusambazwa na kutunzwa kwa ajili ya Watu wengine.

Lazima Utumie lugha kwa usahihi. Na sio kiingereza tu.. shida yetu leo hata kiswahili hatujui. Tunaandika mambo kama tuna mtindio wa ubongo.. funny enough hata Radio presenters (who once were the pinnacle for excellence) Kiswahili chao ni utumbo wa kiwango cha Lami ya Kibaha!

Hatuna tena namna sahihi ya kuucondition Umma maana kinacholetwa kwao kwa sasa ni majanga matupu, iwe Filamu, Makala, Hadithi, Hotuba, Nyimbo, Mashairi, Tenzi, Nk hakuna kinachoandikwa kwa weledi.. na kinachozingatia matumizi sahihi ya lugha kinaitwa "boring".

Matokeo yake kila kitu kwa sasa kinawalenga Watu wenye kiwango kikubwa cha ujinga. 🙂
 
Abigail.
Kama waziri wa elimu hajui kiingereza unategemea mwanafunzi au hata mwalimu kwenye shule zilizo chini ya huyo waziri ajue kiingereza?
Waziri ni kiunganisho kati ya Lumumba na serikali tu, kiingereza ni katibu mkuu ambaye ni mtendaji, huyu hafiki Lumumba.
 
Firstly, you choose one , either American, British or African English.

let's start. 😒
Haha hiyo African English imekuwa categorised kuanzia lini?😂😂
British, American and Autralian English languages.
 
Lugha na uwezo wa kuwasiliana kwa ufasaha ni muhimu sana. Ndio njia pekee uwezo na ujuzi alionao mtu unaweza kudhihirika, kusambazwa na kutunzwa kwa ajili ya Watu wengine.

Lazima Utumie lugha kwa usahihi. Na sio kiingereza tu.. shida yetu leo hata kiswahili hatujui. Tunaandika mambo kama tuna mtindio wa ubongo.. funny enough hata Radio presenters (who once were the pinnacle for excellence) Kiswahili chao ni utumbo wa kiwango cha Lami ya Kibaha!

Hatuna tena namna sahihi ya kuucondition Umma maana kinacholetwa kwao kwa sasa ni majanga matupu, iwe Filamu, Makala, Hadithi, Hotuba, Nyimbo, Mashairi, Tenzi, Nk hakuna kinachoandikwa kwa weledi.. na kinachozingatia matumizi sahihi ya lugha kinaitwa "boring".

Matokeo yake kila kitu kwa sasa kinawalenga Watu wenye kiwango kikubwa cha ujinga. 🙂
hivyo vitu havikwepeki,hasa muingiliano wa jamii mbali mbali unapokuwepo.
leo hii mmasai kutokea manyara huko ndani,anasafari ndefu sana ya kuongea au kuandika kiswahili fasaha,achana na kiingereza.

kiingereza imekuwa lugha rasmi kwa kipindi kirefu sasa,na ni muhimu lakini sio lazima.inachukua miaka mingapi mtu kujifunza kiingereza ili aishi mazingira yanayomlazimu kukijua???hata mwezi hauishi.

hatuwezi worship kiingereza mpaka kuamini ni chanzo cha matatizo tuliyo nayo,ni dalili za utegemezi,tena ni dhana mbovu kabisa, ni ile ile inayowafanya wazazi kutafuta shule za kiingereza kwa gharama yoyote ile,wakati soko la mtaani linataka uwasilishaji wa taaluma.
 
Abigail.
Kama waziri wa elimu hajui kiingereza unategemea mwanafunzi au hata mwalimu kwenye shule zilizo chini ya huyo waziri ajue kiingereza?
U waziri unasomewa ama ni nafasi itokanayo na siasa?
 
I knew it
How can you mention something that doesn't exist?
I've never seen it anywhere
So I had to hear it from you for the first time

Call it self trap
Naona unaendelea kujivua nguo.

Call it self trap ndio nini?
Ama ndio kusema nyani haoni...

Siku zote ukiona mtu anamcheka mwenzako kuwa hamjui kiimgereza wakati sio lugha mama, basi ujue huyo anashida.

Wewe mleta uzi hivi unajua Kuna wazungu wamezaliwa UK lakini akiongea kizungu unaweza kushangaa
 
hivyo vitu havikwepeki,hasa muingiliano wa jamii mbali mbali unapokuwepo.
leo hii mmasai kutokea manyara huko ndani,anasafari ndefu sana ya kuongea au kuandika kiswahili fasaha,achana na kiingereza.

kiingereza imekuwa lugha rasmi kwa kipindi kirefu sasa,na ni muhimu lakini sio lazima.inachukua miaka mingapi mtu kujifunza kiingereza ili aishi mazingira yanayomlazimu kukijua???hata mwezi hauishi.

hatuwezi worship kiingereza mpaka kuamini ni chanzo cha matatizo tuliyo nayo,ni dalili za utegemezi,tena ni dhana mbovu kabisa, ni ile ile inayowafanya wazazi kutafuta shule za kiingereza kwa gharama yoyote ile,wakati soko la mtaani linataka uwasilishaji wa taaluma.
Mimi niko against shule za mitaala ya Kizungu. Kabisa.. shida shule zilizoko maeneo ninayoishi za serikali ziko underfunded na hazikidhi kutoa elimu inayofaa kwa mtoto.

Watoto wetu mazingira wanayoishi ni mazingira ya Utamaduni wa kiswahili, wanahitaji kuuelewa Uswahili ili waweze kuyatawala mazingira yao.. Nakubaliana na wewe kama taifa tunahitaji mabadiliko.

Lakini kabla ya yote ni kujifunza utunzaji. Ukikaa nyumba ya kupanga na ukaiabuse usitegemee ukihamia kwako ndio utageuka mtunzaji.

Haya haya tuliyoyarithi ama hatuwezi kuyatunza kwa maana ya kuyatumia kwa ufasaha.. hata tungepewa kitu chetu na bora bado tusingeweza.

Kwa kifupi Taifa hili halina Nidhamu... Na hilo unaweza kuliona katika mambo madogo madogo kabisa... Matumizi ya barabara, Matumizi ya Ardhi, Ujenzi, Matumizi ya Lugha... Kote utaona jinsi gani nidhamu imetoweka..

Kwa hoja ya muingiliano wa Lugha mbalimbali sio kesi.. maana ukifika london wewe/mimi na uswahili wetu Tutaongea Kiingereza sanifu kama kweli tunataka kuhudumiwa.. kiswahili na upya wake hakina sababu ya kuacha kuwa halisi na chenye maana..
 
Kwa bahati mbaya sana, vijana wa sasa hapa Tz sio tu wanashindwa kuzungumza au kuandika Kiingereza:- Hata Kiswahili wanachoandika au kukiongea mara nyingi sana kina makosa. Ukitaka kujua tatizo ni lugha (iwe Kiswahili au Kiingereza), pitia tu mambo watu wanayoandika wanapochangia mada kwenye mitandao.

a) WENGI SANA hawawezi kutofautisha kati ya herufi L na R. Unamsikia mtu anasema "nilipokuwa nachumbia mahari ambapo mahali ilipelekwa ni kwa mjomba"

b) Ni Watanzania wengi (hata baadhi ya viongozi wanasiasa) wanasema:- "Tangia sasa...." wakimaanisha kuanzia sasa. Hawajui wangepaswa kusema "Tangu sasa", au "kuanzia sasa"

c) Wapo pia watu wengi ambao hawajui the difference between a subject and a predicate (samahani kwa kuchanganya kimombo ndani maana hata mimi yapo maneno ya Kiswahili siyajui - kwa mfano subject and predicate). Nilitaka kusema kwamba watu wengi "wanachanganya mambo" wakati wanazumgumzia mambo mawili tofuati.

Kwa mfano mtangazaji wa habari anasema:- 'Lile gari lilimgonga mtu na kufa" Maana ya mstari huu ni kwamba gari ndio lilikufa. Angetaka kusema mtu ndie kafa angesema "lori lilimgonga mtu akafa"

d) Makosa yapo mengi tu kwenye Kiswahili kinachozungumwa na baadhi ya wasomi wa Tanzania. Kosa lingine ni pale mtoa habari anaposema:- "Alipigwa risasi akaweza kufa" badala ya kusema alipigwa risasi akafa. Unaposema mtu ameweza kitu fulani una maana hicho ni kitu ambacho alikuwa anataka akipate na akajitahidi mpaka akakipata. Hivyo sio sawa kusema mtu aliyepigwa risasi aliweza kufa maana hakuwa anajitahidi kufa.

So, my question to your dear readers is this:- If we can make SO MANYA MISTAKES in Kiswahili which is our mother tongue, do you expect us to be proficient, and efficient in making utterences in a foreign language? No way ! CIAO !
Big up mkuu,i salute you kwa hii comment.
 
We subiri siku akukamate
Atanitandika viboko?
15678901.jpg
 
Hivi wanafunzi waliomaliza vyuo vikuu Afrika mashariki ya zamani Tz, Kenya Uganda wakifanyiwa interview ya kufa mtu ili kuajiriwa Watanzania wataajiriwa kweli? Utasikia wanapendelea Kenya na Uganda! Kumbe lugha ya malkia ndio tatizo!
 
Back
Top Bottom