Mkuu natambua mchango wako wa kuutetea uislamu Mungu akulipe kwa hilo ila sio vizuri kuchanganya dini na siasa, serikali inatambua kuwa kuna taasisi nyingine tofauti na bakwata na taarifa za kuandama kwa mwezi zimetoka alhamis kuanzia saa moja na nusu mpaka saa mbili kuwa kesho yake ijumaa kuna baadhi ya wananchi wa kiislamu wataswali swala ya idd hivyo kwa nini hakukua na tamko la kutokuwepo kwa kazi na shule ijumaa, kuna watu walikosa fadhila za swala ya idd sababu walikuwa shule na makazini, ila serikali huwasikliza hasa bakwata tu, unajua ni misikiti mingapi wananchi wamejichanga kujenga ila ikitokea mgogoro kidogo kwenye uongozi serikali inauchukua msikiti na kuweka chini ya uongozi wa bakwata, hivyo kama serikali inatambua taasisi zipo nyingi kwa nini ina wa favour sana bakwata.