Wasio waislamu msilete ujuaji katika mambo ya Uislamu

Wasio waislamu msilete ujuaji katika mambo ya Uislamu

Mkuu natambua mchango wako wa kuutetea uislamu Mungu akulipe kwa hilo ila sio vizuri kuchanganya dini na siasa, serikali inatambua kuwa kuna taasisi nyingine tofauti na bakwata na taarifa za kuandama kwa mwezi zimetoka alhamis kuanzia saa moja na nusu mpaka saa mbili kuwa kesho yake ijumaa kuna baadhi ya wananchi wa kiislamu wataswali swala ya idd hivyo kwa nini hakukua na tamko la kutokuwepo kwa kazi na shule ijumaa, kuna watu walikosa fadhila za swala ya idd sababu walikuwa shule na makazini, ila serikali huwasikliza hasa bakwata tu, unajua ni misikiti mingapi wananchi wamejichanga kujenga ila ikitokea mgogoro kidogo kwenye uongozi serikali inauchukua msikiti na kuweka chini ya uongozi wa bakwata, hivyo kama serikali inatambua taasisi zipo nyingi kwa nini ina wa favour sana bakwata.
Kwanza Asante kwa maoni yako,lakini pili una hoja ya msingi kuhusu kutengana kwa waislamu kwani tumeambiwa katika qur'an

“Na shikamaneni nyote kwa pamoja na kamba ya Mwenyezi Mungu, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu juu yenu, mlipokuwa maadui akaziunganisha nyoyo zenu mkawa kwa neema yake ndugu…”
(Surah Aal-Imran 3:103)

Hiyo no aya ambayo inasisitiza sana mshikamano wa waislamu duniani kote,sasa hapa tujiulize je wasomi na wanazuoni wa kiislamu hawaijui aya hii au fundisho au Agizo hili.

Swala la kujiuliza hapa,Je ni uongozi upi unatambulika hapa Tanzania na serikali??

Jibu ni Bakwata,sasa kama Bakwata inatambulika je ungetarajia serikali itambue taasisi nyingine tofauti na Bakwata?

Kwanza ingetakiwa uongozi wa Bakwata utambuliwe na kuheshimiwa na waislamu wote,kisha kama kuna hoja ,marekebisho au mabadiliko yafanyike miongoni mwa taasisi zote,ila huu ujinga wa kila taasisi kuwa na meno ndio unatugawa waislamu

Huko nyuma enzi za Afrika Mashariki, East Afrika ilikuwa na msemaji au chombo kimoja cha waislamu ambacho ndio msemaji wa mwandamo wa mwezi na hakukuwa na shida yoyote ile,swali la kujiuliza je,kimetupata nini sasa hivi.

Hao ambao hawafuati mamlaka ya Uislamu ambayo ndio inatambulika na Serikali wasilaumu kwa kushindwa kupata nafasi ya kula sikukuu kwasababu wameamua wenyewe kufuata mlengo mwingine ambao hautambuliki na serikali
 
You are an establishment shill
 
View attachment 3561352

Kumekuwa na ujinga mwingi sana wa watu ambao hawajui chochote kuhusu Uislamu na kuwa kimbelembele kutoa majibu ya Uislamu,ikiwa wao tu hawajui imani yao vizuri kumjua yupi ni Mungu na yupi ni nabii/mtume ndio wataweza kweli kuujua Uislamu?

Nimepitia post kadhaa kuhusiana na mwandamo wa mwezi,wengi ambao sio waislamu ndio wa kwanza kuiponda Bakwata kwamba ni chombo sijui cha Ccm au sijui cha Serikali,huu ujinga mmeutoa wapi?

Yani kwakuwa tu sikukuu haikuangukia Ijumaa basi ujinga wenu,upuuzi wenu wote mnaulekeza kwa Bakwata, je mnajua kuhusu elimu ya figh ya dini ya kiislamu?

Kama hamjui sasa mnapata wapi gut za kuzungumzia kitu ambacho hamkijui? Yani sawa sawa na Mimi leo kobazi nizungumzie kuhusu Naziri wanazo weka makatekitsi au mafaza au mabraza,though nilipata elimu kidogo kuhusu hili lakini sina gut ya kueleza kama wakatoliki wenyewe

Uislamu katika elimu ya figh/ Sheria ya dini kuhusiana na ibada mbali mbali,inasema kuelekeza njia mbili ambazo waislamu wanaweza kufunga au kufungua kutokana na muandamo wa mwezi

Kuna ile mkiona mwezi fungeni na ukionekana mwezi fungeni. Na hiyo ya kuona kutokana na zone ya nchi husika au ukanda husika ndio ambayo imekuwa ikitumika karne na karne,sasa Leo hii Bakwata wakitumia njia hiyo ndio mnawaona vibaraka wa CCM au Serikali?

Stay away from our business!!!

Ni hayo tu!
Dini ya, kishetani,
Ukihama dini, unauliwa, wa Islam wana mahaba makubwa na mtume mudy kuliko Allah wao,
Hawataji jina LA mtume wao bila kusema Amani iwe juu yake, "PBUH) Ila, allah wao, wanamtaja tu, dini isiyo taka critical thinking, bure kabisa,
 
Hawa jamaa wanataka watu wote wawe na mawazo ya aina moja? Mtu akiwa tofauti na wanavyofikiria wao anakua adui? Hii dunia ingekuwa na akili moja ingefika ilipofika au tungekuwa bado tunakula mizizi na matunda pori hadi leo tukiishi mapangoni, hata karatasi za kuchapisha kuruani yenyewe zingekuwepo?😛😛
Hapana unakosea ukisema hivyo,tunatambua mawazo na maoni ya kila watu,lakini kuna masuala hayana maoni wala mawazo binafsi,huwezi ukaleta maoni yako kwenye ibada

Mfano sijui kama ni sahihi kuwaambia au kutoa maoni yako kwa wakatoliki kwa kuwaambia kwanini wasiache tu kuweka alama ya msalaba kama wanavyofanya,hapo maoni yako na mawazo yako hayahitajiki,hivyo hivyo swala muandamo wa mwezi hatuhitaji mawazo yenu wala maoni yenu,period
 
Achaga ujinga kuufanya uislam ni hakimiliki yenu tu, labda ungekuwa mwarabu hapo ungeeleweka unalinda utamaduni wenu, mila na desturi zenu za huko mashariki ya kati. Na kama ni mbongo ukija na hoja hii basi utakuwa umechanganyikiwa na dini na huujui uislam ulianzishwa wapi. Kasome kitabu how they create islam
Wewe ni mpuuzi kama wapuuzi wengine tu,kitendo cha wewe kuaminishwa watu walitengeza Uislamu inatosha kujua kwamba ur not thinking by yourself,unalishwa tu mawazo na wengine bila hata kutafakari
 
BAKWATA ni taasisi ya kisiasa tu
Waislam wenyewe wanaipuuza BAKWATA
Mahakama ishatoa mwogozo kuwa BAKWATA asijipe kiherehere cha kujifanya taasisi ya waislam wote.

BAKWATA inakandamiza waislam wenyewe
Mamia ya mashehe wapo gerezani karibia miaka 20 taasisi Yao BAKWATA ipi kimya kila siku wanaenda ikulu kula tende na ubwabwa

Wanatumiwa na mafisadi kulinda mambo Yao.
Juzi hapa taasisi ya dini kubwa kama BAKWATA inatoka kutetea mauaji ya Watanganyika
Hakuna kitu kibaya kama kutoa tuhuma bila uhakika na kile unachokisema,umezungumzia kwamba Bakwata imeacha kuwatoa masheikh 20 huko kwenye kesi,je ulijua hiyo kesi ina uzito kiasi gani? Je ulitaka Bakwata iitishe maandamano ya waislamu wote kuandamana kudai masheikh watolewe,na lau ingefanya hivyo hapa mgekuja na nyuzi hapa kusema waislamu hawafuati sheria za nchi

Naweza sema mmefanikiwa pakubwa sana kuipa Bakwata jina baya hivyo kila jambo ambalo halipo sawa ni lawama kwa BAKWATA

Ndio natambua Bakwata kama taasisi nyingine ina mapungufu na makosa yake lkn si hekima wala busara kuitupia kila jambo baya
 
Back
Top Bottom