Wasaidizi wa Rais msirudie kosa hili

Wasaidizi wa Rais msirudie kosa hili

Kule kuna magofu tu
IMG_20200216_141001.jpg
 
Jana zilisanbaa video zikionyesha Rais wetu akiwa kwenye gari lenye namba.binafsi akikatiza mitaa ya dodoma.akiwa na ulinzi hafifu sana,katika kile kilichoelezwa ni kutenganisha kazi za chama.na urais

Rais ni Rais tu muda wowote, akiwa Chato, au hata Kisiwandui, katiba inamtambua kama Rais

Kitendo cha kumuondolea gari lake maalum na msafara,wake naweza kuita kama jaribio la kuhatarisha maisha ya Rais na na kuiweka nchi katika hali ya taharuki

Tupo kwenye vita kali ya uchumi inayoongozwa na Rais wetu, maadui wapo macho kuangalia jinsi gani wanaweza kuishinda vita hii kwa njia za mkato, wasaidizi wa Rais kama mmelala amkeni

Imenitisha sana kuona V8 imekaa upande wa kulia ikiwa spidi kali, bila tahadhari yoyote, je ingetokea fuso ya vitunguu toka Singida dereva kalewa na yupo kwenye mwendo kasi ingekuaje?

Usalama wa Rais ni kipaumbele cha kwanza, msiogope kuambiwa mnatumia vibaya rasilimali za serikali, katiba haimbani Rais, MSIRUDIE JAMANI

Naona unataka ukurugenzi mzee baba.! Yule alikuwa na ulinzi wake wa kutosha sana kabisa
 
humo ndani ya mafuso na vipanya waliomo huwezi amini .Msafara wa raisi huwa na advance team waweza kuwa kwenye daladala, bodaboda, lori, trekta na chochote

mleta mada usijifanye ujuaji kazi za ullinzi ni fani tena watu wanasomea kufa mtu
Mwaka juzi, huko Kenya walikufa watu 6, kutoka katika kikosi cha ulinzi wa Rais wa Kenya
Walikua wakitoka kumsindikiza kiongozi airport, wakati wanarudisha magari wakawa wanapita kulia kukwepa foleni, kumbe mbele kuna ajali ya lori la mafuta, ile wanalifikia tu lori, likalipuka, sita waliaga papo hapo bahati hawakuwa na kiongozi
Mnatuambia sijui boda boda kwenye vipanya kuna watu, usalama wa Rais hauwezi kulindwa na watu wanaotumia boda boda, acheni utani
 
Pumbavu kabisa, yani hii nchi ina wanafiki wengi, yani uoga umebadirika umekuwa unafiki.....
 
Wacha njaa zako wewe chumia tumbo, yaani unajifanya kufahamu protocol za ulinzi wa Rais wa nchi kuliko watu wa idara ya usalama wa Rais?

Wacheni kutafuta uteuzi kwa njia za mkato
Jana zilisanbaa video zikionyesha Rais wetu akiwa kwenye gari lenye namba.binafsi akikatiza mitaa ya dodoma.akiwa na ulinzi hafifu sana,katika kile kilichoelezwa ni kutenganisha kazi za chama.na urais

Rais ni Rais tu muda wowote, akiwa Chato, au hata Kisiwandui, katiba inamtambua kama Rais

Kitendo cha kumuondolea gari lake maalum na msafara,wake naweza kuita kama jaribio la kuhatarisha maisha ya Rais na na kuiweka nchi katika hali ya taharuki

Tupo kwenye vita kali ya uchumi inayoongozwa na Rais wetu, maadui wapo macho kuangalia jinsi gani wanaweza kuishinda vita hii kwa njia za mkato, wasaidizi wa Rais kama mmelala amkeni

Imenitisha sana kuona V8 imekaa upande wa kulia ikiwa spidi kali, bila tahadhari yoyote, je ingetokea fuso ya vitunguu toka Singida dereva kalewa na yupo kwenye mwendo kasi ingekuaje?

Usalama wa Rais ni kipaumbele cha kwanza, msiogope kuambiwa mnatumia vibaya rasilimali za serikali, katiba haimbani Rais, MSIRUDIE JAMANI
 
Kwa hiyo na wewe uliamini kabisa jamaa yupo mwenyewe, ungejua eneo zima lilikuwa na undercover wala usingeongelea habari ya roli la vitunguu.....
Mkuu hao ndiyo watu wanao tucheleweshea kupata maendeleo hapa nchini
 
Maana hao ni mabingwa wa madrama.
Simple tu aliyekuwa akifatilia kwa nyuma na kupiga picha ni Nani?Hizi drama za kitoto toto
Kwa hiyo angeweza kuzuia ajali na kikamera chake?
 
Nchi yetu ni ya amani hakuna shida,
Na kujiamini pia, cheki Assad anavyojiendesha mwenyewe mitaani, wakati nchi iko vitani.
Ni kujiamini tu
Wewe ni mwalimu wangu lakini hapo umechapia Assad hawezi kufanya hivyo bila kuwa na ulinzi pembeni
 
Yote 9, 10 ni alikuwa hawezi kumuagiza Bashiru amletee fomu Ikulu. Kama vikao vya ccm vimefanyiwa Ikulu alishindwa nini kuletewa form Ikulu?
 
kabombe,
Absolutely right to the point. Pamoja na kwamba Dodoma ni salama I was not impressed. Hawa mabeberu wana njia nyingi sana hivi sasa adui yao mkubwa ni Tanzania na JPM. Hata majirani zetu ni wakati wa kuwaangalia kwa macho mawili tusibweteke haya yanayotokea Tanzania hawayapendi wanayafuatila kwa karibu sana kuliko sisi tunavyofikiri.
 
Wacha njaa zako wewe chumia tumbo, yaani unajifanya kufahamu protocol za ulinzi wa rais wa nchi kuliko watu wa idara ya usalama wa rais?

Wacheni kutafuta uteuzi kwa njia za mkato
Sihitaji uteuzi, nitaharibu tuu, najijua, lakini natoa mawazo yangu, sio lazima uyakubali
 
Elewa hao ni taaluma yao mpaka wakaruhusu hayo jua walishachukua tahadhari zote ndiyo wakaamua hivyo!!! Hata kama kutatokea tatizo wao wanayo Plan B. Hao jamaa hawafanyi kazi kienyeji kama unavyofikiri!!

Kwani marehemu Moringe Sokoine kama waziri mkuu hakuwa na security detail? Acheni kuwalisha watu matango Pori!
 
Back
Top Bottom