JUAN MANUEL
JF-Expert Member
- Nov 26, 2010
- 8,497
- 18,298
Hizo tunaita PR stunts, wamefanya hivyo ili kuzuia watu wasiongee sana, kwamba Raisi anatumia Vifaa vya uraisi kwa shughuli za chama, kwanza hiyo gari ni armoured, hata upige bomu, anatoka salama,Jana zilisanbaa video zikionyesha Rais wetu akiwa kwenye gari lenye namba binafsi akikatiza mitaa ya Dodoma akiwa na ulinzi hafifu sana, katika kile kilichoelezwa ni kutenganisha kazi za chama na urais
Rais ni Rais tu muda wowote, akiwa Chato, au hata Kisiwandui, katiba inamtambua kama Rais
Kitendo cha kumuondolea gari lake maalum na msafara, wake naweza kuita kama jaribio la kuhatarisha maisha ya Rais na na kuiweka nchi katika hali ya taharuki
Tupo kwenye vita kali ya uchumi inayoongozwa na Rais wetu, maadui wapo macho kuangalia jinsi gani wanaweza kuishinda vita hii kwa njia za mkato, wasaidizi wa Rais kama mmelala amkeni
Imenitisha sana kuona V8 imekaa upande wa kulia ikiwa spidi kali, bila tahadhari yoyote, je ingetokea fuso ya vitunguu toka Singida dereva kalewa na yupo kwenye mwendo kasi ingekuaje?
Usalama wa Rais ni kipaumbele cha kwanza, msiogope kuambiwa mnatumia vibaya rasilimali za serikali,katiba haimbani Rais,MSIRUDIE JAMANI
Pia, hiyo njia yote aliyokuwa anapita lazima ilikuwa imejaa presidential guards, hata kama walikuwa wamevaa kiraia, mfagizi wa barabara, dereva tex, bodaboda, mtembea kwa miguu, aliyekuwepo maeneo hayo, baadhi yao walikuwa, TISS