Wasaidizi wa Rais msirudie kosa hili

Wasaidizi wa Rais msirudie kosa hili

Wewe nyamaza usijifanye wewe unajua sana kuliko walinzi wa rais!!!Wako wenye kazi hiyo wanajua wanafanya nini acha kutafuta kuganga njaa kupitia rais!!!
Ni mawazo yangu tu kama ulivyotoa ya kwako
Walinzi nao ni binadamu, na siku zote makosa ya kibinadamu huambatana na gharama kubwa sana
 
Jana zilisanbaa video zikionyesha Rais wetu akiwa kwenye gari lenye namba.binafsi akikatiza mitaa ya dodoma.akiwa na ulinzi hafifu sana,katika kile kilichoelezwa ni kutenganisha kazi za chama.na urais

Rais ni Rais tu muda wowote, akiwa Chato, au hata Kisiwandui, katiba inamtambua kama Rais

Kitendo cha kumuondolea gari lake maalum na msafara,wake naweza kuita kama jaribio la kuhatarisha maisha ya Rais na na kuiweka nchi katika hali ya taharuki

Tupo kwenye vita kali ya uchumi inayoongozwa na Rais wetu, maadui wapo macho kuangalia jinsi gani wanaweza kuishinda vita hii kwa njia za mkato, wasaidizi wa Rais kama mmelala amkeni

Imenitisha sana kuona V8 imekaa upande wa kulia ikiwa spidi kali, bila tahadhari yoyote, je ingetokea fuso ya vitunguu toka Singida dereva kalewa na yupo kwenye mwendo kasi ingekuaje?

Usalama wa Rais ni kipaumbele cha kwanza, msiogope kuambiwa mnatumia vibaya rasilimali za serikali, katiba haimbani Rais, MSIRUDIE JAMANI

Labda wanatekeleza Katiba ya Jamhuri kuwa Rais akivunja Bunge kiti ki wazi, ingawaje kwingine kwenye katiba hiyo hiyo inasema ki wazi mara mwingine anapoapishwa!!!
 
Vipanya vya usalama wa taifa vile kwahiyo usiogope, halafu hii vita ya kiuchumi anapigana na wakina nani?
Usalama hauna vipanya bana
Vita tunapigana na mabeberu, wamekasirika sana kuthubutu kujitegemea kwa umeme kwa pesa yetu
 
Atakaye Mrithi ni nani tuwe Serious na Maisha. Nchi tuwape akina Faru John, Tundu, Msigwa, Zitto 🤣🤣🤣🤣🤣🤣. Tuache tabia chafu za kujaribu.
Chadema kila Mtu anaogopa kurudi Jimboni kugombea maana anajua itakuwa Fedheha kwake na Familia yake. Na Chadema atakayerudi Bungeni sijui maana lichamaa lao lipo kama la Hashim
Kushindwa uchaguzi ni fedheha? Huyo Mbowe kawa mbunge kwa miaka mingapi labda hadi leo hii aogope kushindwa? Kuna watu wamekuwa marais huko visiwani na wote tunajua wameupataje huo urais, kwenye maisha kuna kushinda na kushindwa mzee
 
Labda wanatekeleza Katiba ya Jamhuri kuwa Rais akivunja Bunge kiti ki wazi, ingawaje kwingine kwenye katiba hiyo hiyo inasema ki wazi mara mwingine anapoapishwa!!!
Weka hiko kifungu hapa
 
kabombe ondoa hilo neno Ulinzi hafifu kwani kwa taarifa yako tu hilo Tukio zima lilikuwa Well Coordinated and Monitored Kiulinzi tena kwa 100%.
Nimeweka video ku substaintiate hofu yangu
Weka ushahidi kuimarisha hoja yako hii
 
Mabeberu hawahawa ambao wanatusaidia kwenye bajeti yetu kila leo? Mbona watu vichwa panzi nyie
Tehehe lazima watusaidie, wametunyonya sana na kupora rasilimali walipotutawala
Kwa sasa ile omba omba na kulia imepungua kuliko kipindi chochote kile, yaani wasipotusaidia hatulii tena
 
Kila mtanzania kuanzia miaka 18 anatakiwa kuwa na katiba, nenda kasome kwenye nakala yako.
Ya kwangu mimi haina hicho kifungu, naomba nisaidie ya kwako mkuu nipate ilmu
 
Usalama hauna vipanya bana
Vita tunapigana na mabeberu,wamekasirika sana kuthubutu kujitegemea kwa umeme kwa pesa yetu
Yaani wewe ni mbuzi kweli! Akili itwawarudia lini nyie pimbi?
Unapigana na mabeberu vita ya uchumi wakati ndio wanaokusaidia kujenga huo uchumi? Pambaf kabisa nyie msio nashukurani na mkono unaokulisheni.

More than 40% ya budget yenu hamuwezi kuitekeleza hadi mpewe support, kisha huyohuyo anaye kusupport unamwita beberu na eti anakupiga vita usiendelee. Utakuwa una kichaa wewe! Viongozi wenu wanawalisha unafiki nanyi mnapokea kama mazuzu vile!
Hivi hata kama huna elimu, kukaa kwako JF kwa muda wote umeshindwa kuelimika na kulitambua hilo?

Sasa naamini kuwa upumbavu wa wanaccm hata ukiutwanga na mpunga au mahindi utashindwa kukoboka Ila mahindi yatatakata
 
Ni mawazo yangu tu kama ulivyotoa ya kwako
Walinzi nao ni binadamu,na siku zote makosa ya kibinadamu huambatana na gharama kubwa sana
Elewa hao ni taaluma yao mpaka wakaruhusu hayo jua walishachukua tahadhari zote ndiyo wakaamua hivyo!!! Hata kama kutatokea tatizo wao wanayo Plan B. Hao jamaa hawafanyi kazi kienyeji kama unavyofikiri!!
 
Kivipi wakati kila kitu kipo wazi?
Kivipi vipi mbona unakuwa mjinga utadhani umetokea Kantalamba huko vijijini juzi, politics ni game na hiyo ni game imechezwa ili mtu wa aina yako aone huo ndio uhalisia???
 
Nimeweka video ku substaintiate hofu yangu
Weka ushahidi kuimarisha hoja yako hii

Sina muda huo wa kuendelea Kujibizana na Wewe katika hili, ila ninaendelea Kusisitiza Tukio zima lilizingatia taratibu zote za Kiusalama kwa Rais.
 
ha ha ukiangalia hio video ni maigizo matupu, kwanza gari ni ile ile (BP) sema tu wameivisha private number, ukicheki kwa makini hizo gari zote za upande wa kulia zilikua zimesimamishwa na pia kuna mlinzi alishuka kwenda kuzuia gari za upande wa kushoto!, ukija kwa hio barabara kubwa ya kwenda dar unaona kabisa iko clear kwa vyovyote itakua ilisha safishwa!

Ila kwa haya maigizo yalio fanyika bado kuna somo lipo kuna hakuna haja ya kusimamishana njiani masaa mawili ili mtu apite kuna uwezekano wa magari ya kawaida kukaa pembeni kwa muda mchache ili hao wakubwa wapite kama inavyofanyika huko kwa wenzetu.
 
Back
Top Bottom