Wasaidizi wa Rais msirudie kosa hili

Wasaidizi wa Rais msirudie kosa hili

Nani ambae uhai wake sio muhimu?
Hivi walinzi wa Nkurunzinza walishindwa nini?
 
Nitaamini kuwa hakuwa na ulinzi iwapo nitaona mabasi ya abiria kwenye ile clip
 
Mkuu nyumba yako haijaisha nini, unaogopa asipokuwa rais yeye nyumba yako haitaisha?
Kwa magufuli ukitaka kujenga lazima ukope benki,mie nimeshajenga bwashee
 
Nani kakuambia kuwa lile li-V8 ni gari binafsi la JPM? Ni kuwahadaa watu tu na kunogesha show. Lile ni gari la ikulu lililopachikwa plate number bandia ya kiraia. System ilikuwa kazini Kama kawaida. Walifanya hivyo kupunguza kelele za wapinzani.
Kelele gani sasa?
 
Kwa taarifa yako mbele kule kuna v8 jeupe moja na nyuma kuna jingine la mshoot video na walinzi juu pembeni boda boda na dalala kulijaa abiria walinzi.
Naomba niishie hapo tafadhali.
Matumizi mabaya ya fedha sasa walinzi daladala kumlinda yesu duh!
 
Jana zilisanbaa video zikionyesha Rais wetu akiwa kwenye gari lenye namba binafsi akikatiza mitaa ya Dodoma akiwa na ulinzi hafifu sana,katika kile kilichoelezwa ni kutenganisha kazi za chama na urais

Rais ni Rais tu muda wowote, akiwa Chato au hata Kisiwandui katiba inamtambua kama Rais

Kitendo cha kumuondolea gari lake maalum na msafara wake naweza kuita kama jaribio la kuhatarisha maisha ya Rais na na kuiweka nchi katika hali ya taharuki

Tupo kwenye vita kali ya uchumi inayoongozwa na Rais wetu, maadui wapo macho kuangalia jinsi gani wanaweza kuishinda vita hii kwa njia za mkato, wasaidizi wa Rais kama mmelala amkeni

Imenitisha sana kuona V8 imekaa upande wa kulia ikiwa spidi kali, bila tahadhari yoyote, je ingetokea fuso ya vitunguu toka Singida dereva kalewa na yupo kwenye mwendo kasi ingekuaje?

Usalama wa Rais ni kipaumbele cha kwanza, msiogope kuambiwa mnatumia vibaya rasilimali za Serikali, katiba haimbani Rais, MSIRUDIE JAMANI

View attachment 1482030
Yaani hayo ya usalama wa Rais umewaza wewe tu. Unafikiri kabisa hii nchi ina watu wazembe kiasi hicho. Licha ya usalama wetu kama nchi, Idara zetu za masuala ya usalama zipo makini sana mkuu.
 
Mbowe alikuwa bar usiku na gari ya KUB ya serikali unataka kusema pale alikuwa anatekeleza kazi za kibunge
MATAGA ndivyo mmefunzwa hivyo na Lijulikali na Mlinga? na Kaka ndugai "mzee wakupiga wenzake marungu ya kichwa"?
Mmejuaje alikuwa bar? Gesti, chooni kama mmengoa CCTV the same mlivyofanya kwa Lissu?
 
Dunia imebadilika!zama za baba wa Taifa si hizi

Ni hatari sana kumtembeza Rais bila kusafisha njia, haswa kwa jiji la Dodoma barabara kuu ni moja tu, wanaoenda Mwanza, Singida, Kigoma, Shinyanga, Tabora, Kagera, Geita, Simiyu na Mara wote wanapita njia hiyo
Kwa hiyo wewe ndio una akili saaaaana kuliko wenye dhamana ya kumlinda? Mi ningekushauri ubakie na kazi ya kupiga makofi kwenye hotuba, haya ya ulinzi tuwaachie walinzi
 
Back
Top Bottom