Warioba: Mimi na Salim urais basi

Warioba: Mimi na Salim urais basi

Aaah Wapi,

Mmeshaanza siasa zenu za majitaka sasa,,

Hebu niambie wewe sasa.humpendi huyu kwa chuki zako binafsi au humpendi kwa kuwa yuko CCM??

Akisimama huyo 2015 hatuna budi kumpatia nchi hii,mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni..
Au kwa kuwa ni Muislam??
Angalia ulovyotutaka mjinga wewe umeanza safi badaye unachomeka mambo yako ya udini. Shetani mkubwa wewe. Kwa hiyo wewe unamkubali kwa kuwa ni muislamu? Dini yenu inaruhusu kutungatunga hoja tena bila kuwa na ubaki kwa nazo? Kwa taarifa yako watanzania wanahohitaji kwa sasa ni kiuongozi bora siyo dini ya mtu. Kwani Kikwete muislamu amekusaidia nini wewe?
 
Punguza jazba kidogo..
 
Mkuu nani sasa anafaa kuwa rais kwa mtazamo wako.

Anayefaa kuwa raisi kwa mtazamo wa wengi ni Mabugando a.k.a mkulima wa mapalachichi/nyanya kwani atatujengea mabugando mengi na atatufundisha kulima mapalachichi ili yakauzwe ulaya yawe mbadala wa horse meat
 
Hatuwezi kukubali kuiharibu nchi kwa miaka 20 mfululizo. Inatosha 10 atakayokuwa ameharibu fastjet.
Alipokea nchi ingali bidhaa zikiwa na bei ndogo. Mf:sukar ilikuwa 600-900/= leo hii had 2000../=
dolar 1@600/= leo hii dolar 1@1600/=
hiyo ni mifano michache tu.
Hatuhitaji tena viongozi wa majaribio. Wazee wa kuharibu nchi pumziken kwanza. Hamna uchungu na nchi, hamna msimamo, ni fuata upepo,fuata bendera. Tulien kwanza tuwaoneshe jinsi wenzenu tunavyorekebisha mambo.
 
Kwa siasa zilivyo sasa, ccm kutoa mgombea urais kutoka Zanzibar, ilihali tunaaminishwa kuwa Zanzibar ni nchi, ni janga lingine, Yaani kuleta mtu wa nchi nyingine KUTAWALA NCHI NYINGINE!! Nitawashangaa sana WATANGANYIKA ambao watampigia kura Mzanzibari kuwa rais wa JMT. Kwa Katiba ya Zanzibar ilivyo, ni kama vile hakuna Muungano, hivyo kuleta Mgombea kutoka Nchi ya Zanzibar kugombea urais wa JMT, ni sawa na KUTAWALA NCHI NYINGINE, na huo utakuwa UKOLONI KABISA. Sina hakika kama Watangayika bado wanahitaji ukoloni wa Wazanzibari.

Ndio maana mimi suluhu yangu siku zote ni KUWA NA SERIKALI MOJA YA JMT, ambayo itaongozwa kutokana na weledi na sifa stahiki za mtu, siyo kwa zamu, OTHERWISE, HATUWEZI KUFIKA.
 
Mkuu CANDID:Hoja yako ina mantiki, lakini turejee nyuma kidogo;
1. Kwenye uchaguzi wa mwaka 2005 Dr. Salim alichafuliwa sana (Siasa za matope),ungetegemea jukwaa gani Dr. SAS angesimama na ku-demonstrate hoja ulizozitoa.
2. Dr. SAS alikwisha kuwa vetted kabla ya mwaka 2005.kwanini usilete hiyo hoja yako wakati ule?.
Please be Candid as per your name.

Sidhani aliyoambiwa kama si ya kweli angetafuta haki ya kurudisha jina lake safi kwa waliomchafua. Zipo njia nyingi, na hata kama wakati ule aliamua kutuliza kichwa kwanza, kwa sasa ni muda mrefu angekuwa ameshapata namna bara ya kurudisha jina lake lililochafuliwa. Siwezi kukubali mtu anituhumu mauaji jambo ambalo ni kesi ya jinai, nitahitaji uthibitishi na vyombo vya dola vithibitishe tuhuma zangu hadi Mahakamani, vinginevyo hapatakalika.

Lowasa alichafuka pengine zaidi ya Salim, hadi kutangazwa kukufukwa uanachama. Lakini alipotulia aliamua kujitutumua na kwamba ye yote mwenye kumharibia jina na tuhuma zisizo na ushahiti atamfikisha mahakamani. Huyo sasa katulia na kuendesha siasa zake.

Salmu kuna tatizo fulani tangu enzi za Nyerere alishaoona, na wazanzibar wanajua zaidi yetu. Hajaribu kuchukua form ya kugombea Zanj, wabara ndo hatujui ati.
 
Sioni sababu ya ukimya kama inamantink.....

Bora raisi akawa mtu ambaye si maarufu kwan anaweza fanya makubwa zaidi....chukulia mfano mwakyembe hakuwa anajulikana lakin baada ya report ya richmond watu walifahamu utendaji wake wa kazi

Afu tuchukulie mfano wa Ben alikuwa kimya sana na hakuwa maarufu wa jukwaan lakin alifanya makubwa....

Kwan ww mtoa thread hii unadhan umaarufu wa kisiasa jukwaan unaweza ukamfanya mtu awe bora kiutendaji???????

Chukulia mfano sugu na Dr salim nan maarufu jukwaan??? Je unaweza kuwalinganisha kiutendaji????

Tunataka raisi mpiga kazi si maarufu wa majukwaaaa????

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums

Salim anafaa kuwa katibu mkuu ofisi ya rais lakini urais hapana.
 
dkt salim ni muungwana. muungwana ni vitendo. kwa bahati mbaya kizazi cha sasa hawaelewi utendaji wake. alifanya mambo mengi lakini ikumbukwe kuwa MWL NYERERE HUKUPENDA JINA LA MTU MMOJA MMOJA LIPANDE. ALIPENDA SANA KUTUKUZWA YEYE. HAKUWAPA MAWAZIRI WAKE FURSA YA KUAMUA NA KUTENDA KAMA WANAVYO FANYA AKINA MAGUFULI NA MWAKYEMBE hivi sasa. nilipokua chuoni, profesa mmoja aliwahi kutuambia kuwa mwalimu amelifanyia taifa letu mengi lkn hakupenda mawaziri wake wasifiwe au waonekane kuwa wanatenda. alipenda mipango ypte apelekewe yeye ili yeye ndiyo aitekeleze. marehemu sokoine aliwahi kukwamishwa na mwalimu katika kasi yake ya kuirekebisha nchi yetu. hii ni kutokana na kumuonea wivu. vilevile alimuona kama HATARI kwa utawala wake. mwalimu alipenda anaeharibu ahamishiwe sehemu nyingine lkn sokoine aliaumuru anaeharibu afukuzwe. hiyo siyo mada ya leo tuachane nayo.

dkt salim ni mtu makini azungumzapo na atendapo. hotuba aliyoitoa chimwaga mwaka 2005 wakati anaomba kuchaguliwa kugombea urais kwa tiketi ya ccm ni kielelezo kuwa uwezo na dira anavyo. hana asili ya kupayuka. kuna watu wanadhani kupayuka ndiyo utendaji. la hasha. kuna mabadiliko makubwa ambayo wakurugenzi wa nsssf na nhc wameyafanya lkn licha ya utendaji wao mzuri, siyo watu wa kujitokeza kujisifu ili waonekane.

dkt salim aliongoza oau ktk mazingira magumu. viongozi wengi walisema kuwa oau haifai kuwepo kwa sababu nchi nyingi zimeshapata uhuru. dkt salim alijitahidi kuzihamasisha kuwa chombo hicho ni muhimu na lazima nchi zichangie ili kukifanya kiwepo. baadaye aka andaa dira ya kubadilisha oau kuwa AU. yakaundwa malengo mapya ya au. LA MSINGI ZAIDI SALIM NI MTU SAFI. HANA KASHFA YA RUSHWA KATIKA UTENDAJI WAKE. mwl nyerere aliwahi kusema kuwa "kimataifa mtanzania namba moja ambaye ameifanya TZ ijulikane na kuheshimika ni dkt salim. alijenga hoja UN akifafanua self reliance (kujitegemea) ambayo tanzania inaifuata. aliiongoza oau na kuifanya kiwe chombo cha kuaminika".

kwa ccm ya sasa, salim ni chaguo bora kwa sababu hayumo katika makundi yanayo chafuana. amekua kimya kwa miaka 8 kwa sababu alichafuliwa sana mwaka 2005 na JK. aliona kuwa njia salama ya kumfanya awe na amani, ni kukaa kimya. alichafuliwa sana!

akipitishwa lowassa lazima akina sitta, membe nk..... hawatomuunga mkono. na kinyume chake ni sahihi. akipitishwa salim, wote watamuunga mkono kwa sababu amepewa mtu ambaye hayumo vitani. kinacho onesha kuwa hapendi rushwa, mwaka juzi kamati anayoiongoza ya MO IBRAHIM iliamua kuwa hakuna kiongozi mstaafu mwenye sifa ya kupewa tuzo. salim alisema wasubiri hadi miaka 2-3 ijayo.

kiafya salim bado ana nguvu na anaonekana vizuri. lowassa sasa hivi ni dhaifu kiafya. slaa ana nguvu lkn mkono naona umeshalemaa! lipumba amechokwa, mrema hoi na mbatia amekiua chama. tukiweka uzalendo pembeni, salim is the right choice to be the fifth president of TZ
th
th
th

Katika masuala ya uadilifu anatakiwa ajibu hoja za kuchafuliwa katika kipindi cha kampeni za kugombea nafasi ya kuwakilisha CCM kiti cha Urais. Kukaa kimya bila kujibu mapigo yale ambayo yalitangazwa waziwazi hadharani ina maanisha alihusika. La sivyo kama anajiona hakuhusika kwa nini asiwachukulie hatua waliomchafua wakati tuhuma hizo zilikuwa nzito kuhusu mauaji?

Wanafalsafa husema kukaa kimya dhiti ya tuhuma zinazomkabili mtu ni kweli zinamhusu na hivyo dhamiri inamwuma, aidha tuhuma si za kweli lakini hajiamini katika kujenga utetezi.

Iwapo anashindwa kujenga utetezi katika masuala yanayomhusu binafsi atawezaje katika mambo mazito ya kitaifa?
 
Candid Scope, DULLAH MSAVIVOR,

..hatujamsikia Dr.Salim akipinga ufisadi.

..hatujamsikia akikemea na kupinga udini na ukabila.

..hatujamsikia akikemea ubaguzi wa waZNZ dhidi ya wa-TGK.

..hatujamsikia akitetea muungano, au akipendekeza muundo bora na wa haki wa muungano.

..hatujamsikia akipinga sera za uuzwaji holela na umilikishwaji wa mali za umma.

..inasemekana ni mwanafunzi nambari wani wa Mwalimu Nyerere lakini hatetei siasa za ujamaa, wala hahubiri sera ya kujitegemea.

..hatujamsikia akitetea nafasi ya Tanzania ktk jumuiya ya Afrika Mashariki.

..hata wakati wa harakati za KATIBA MPYA hatukumsikia akieleza msimamo wako.

..the man is just silent and indifferent kwa mambo yote yanayomkaibili nchi yetu na mwananchi wa kawaida.

..inasemekana anajiweza, lakini sijawahi kusikia amechangia msikiti, kanisa, shule, kisima cha maji, timu ya mpira, popote pale nchini.

cc: Kubwajinga, Nguruvi3, Ritz, njiwa

Umefanikiwa mdau kuweka kitoweo maana niliandaa mezani ugali na kipwagu bila kitoweo. Thanks
 
Ndugu wana JF naandika haya ili kuweza kumfahamu vyema Dr salim kwani ukimya wake unatutia mashaka juu ya uwezo wake wa kuongoza nchi endapo kutatokea muujiza akaukwaa urais. Wengi hatujui msimamo wake juu ya mambo kadha wa kadha yanayomhusu yeye mwenyewe na taifa kwa ujumla. Maswali yangu ni haya hapa naomba atupe majibu. Wanajamvi mwaweza kuongezea:
1. Ni yapi maoni yako kuhusu suala la ushoga na ndoa za jinsia moja kama tunavyoshinikizwa na nchi za magharibi?
2. Ni mfumo upi wa muungano ambao wewe kwa maoni yako unadhani utaondoa/kupunguza matatizo ya muungano?
3. Je? Unasemaje juu ya tuhuma zilizotolewa na wana CCM wenzako kuwa ulishiriki kumuua aliyekuwa rais wa Zanzibar hayati Karume?
4. Je? Unafahamu kuwa kuna ufisadi wa kutisha nchini? Kama ndivyo, nini maoni yako juu ya kashfa za Richmond, fedha zilizofichwa Uswis, kashfa ya EPA, kashfa ya RADA nk?
5. Je? Unaweza kutueleza jambo kubwa na la kukumbukwa uliloifanyia Tanzania wakati ulipokuwa waziri mkuu wakati wa awamu ya kwanza?
6. Je, Huoni kuwa umri umekutupa mkono na kwamba ni wakati wa kupumzika na kuwa mshauri wa rais ajaye kuliko wewe mwenyewe kugombea?
7. Kama wana ccm waliona hufai mwaka 2005, ni jambo gani litamfanya aone kwamba sasa unafaa?
8. Je, huoni kwamba ni busara kuacha watanganyika ambao ni zaidi ya millioni 43 wajichagulie rais wao na wewe kwenda kugombea kwenu Zanzibar ambao idadi yenu ni chini ya mil moja na nusu?
9. Nini maoni yako kuhusu kuporomoka kwa kiwango cha elimu nchini na ni nini kifanyike?
10. Nini maoni yako kuhusu uendeshaji wa shughuli za bunge la jamhuri ya muungano wa tz?

Tafadhali Dr ukijibu haya walau tutaanza kukufahamu kuliko hivi unavyotaka kutubabatiza kama alivyofanya mwenyekiti wako jk. Usitumie ukimya kama silaa ya kuchukua ikulu. Ikulu panahitaji mtu ambae ana msimamo na muwazi.
 
Tope kichwani at work-hili ni tope la mfinyanzi lime-replace ubongo wa mtu,-shame on you.
 
JESHI LITAPEWA UNIFORM KUTOKAS KUWAIT
mabrigadia watapewa landcruser kutoka iraq.
halafu palestina day itarudi!
 
Mleta mada ameweka hoja zake, jaribu kuleta hoja za utetezi badala ya kujibu kimipasho. Hapa hatujadiri mambo mengine katika mada hii zaidi ya kupima uwezo wa presidential candidates, tunahaki ya kupima uwezo wao mapema badala ya kutumbukiza tu kura sandukuni baadaye tuje kulalamikia uwezo wao kuwa mdogo kuongoza watanzania.

nimeipenda hoja, mi binafsi namkubali sana jamaa na labda niseme hivi; pengine alivunjwa moyo na waliopiga propaganda juu yake last time wakimtuhumu na uarabu. lakini kama anataka, bado tunampenda.
na wewe unayekimbilia kumtuhumu mleta mada kuhusu uislam uache kabisa, ni lini watu kama wewe mtajiamini, kwani unafikiri uislam ni weakness! kila kikisemwa kitu mkihusishe na kwa kuwa ni mwislam, loh, mnafanya ambao sio waislam wasiseme chochote au wasishiriki kumchambua kiongozi hususan akiwa mwislam, acheni hizo
 
Ndugu wana JF naandika haya ili kuweza kumfahamu vyema Dr salim kwani ukimya wake unatutia mashaka juu ya uwezo wake wa kuongoza nchi endapo kutatokea muujiza akaukwaa urais. Wengi hatujui msimamo wake juu ya mambo kadha wa kadha yanayomhusu yeye mwenyewe na taifa kwa ujumla. Maswali yangu ni haya hapa naomba atupe majibu. Wanajamvi mwaweza kuongezea:
1. Ni yapi maoni yako kuhusu suala la ushoga na ndoa za jinsia moja kama tunavyoshinikizwa na nchi za magharibi?
2. Ni mfumo upi wa muungano ambao wewe kwa maoni yako unadhani utaondoa/kupunguza matatizo ya muungano?
3. Je? Unasemaje juu ya tuhuma zilizotolewa na wana CCM wenzako kuwa ulishiriki kumuua aliyekuwa rais wa Zanzibar hayati Karume?
4. Je? Unafahamu kuwa kuna ufisadi wa kutisha nchini? Kama ndivyo, nini maoni yako juu ya kashfa za Richmond, fedha zilizofichwa Uswis, kashfa ya EPA, kashfa ya RADA nk?
5. Je? Unaweza kutueleza jambo kubwa na la kukumbukwa uliloifanyia Tanzania wakati ulipokuwa waziri mkuu wakati wa awamu ya kwanza?
6. Je, Huoni kuwa umri umekutupa mkono na kwamba ni wakati wa kupumzika na kuwa mshauri wa rais ajaye kuliko wewe mwenyewe kugombea?
7. Kama wana ccm waliona hufai mwaka 2005, ni jambo gani litamfanya aone kwamba sasa unafaa?
8. Je, huoni kwamba ni busara kuacha watanganyika ambao ni zaidi ya millioni 43 wajichagulie rais wao na wewe kwenda kugombea kwenu Zanzibar ambao idadi yenu ni chini ya mil moja na nusu?
9. Nini maoni yako kuhusu kuporomoka kwa kiwango cha elimu nchini na ni nini kifanyike?
10. Nini maoni yako kuhusu uendeshaji wa shughuli za bunge la jamhuri ya muungano wa tz?

Tafadhali Dr ukijibu haya walau tutaanza kukufahamu kuliko hivi unavyotaka kutubabatiza kama alivyofanya mwenyekiti wako jk. Usitumie ukimya kama silaa ya kuchukua ikulu. Ikulu panahitaji mtu ambae ana msimamo na muwazi.

Umeleta mambo muhimu ambayo tungependa avunje ukimya tumwelewe vema, na si kwa sababu ya uwezekana wa kugombea urais tu, ila kama mtu mashuhuri ana mtazamo gani kwa masuala uliyoorodhesha.
 
nimeipenda hoja, mi binafsi namkubali sana jamaa na labda niseme hivi; pengine alivunjwa moyo na waliopiga propaganda juu yake last time wakimtuhumu na uarabu. lakini kama anataka, bado tunampenda.
na wewe unayekimbilia kumtuhumu mleta mada kuhusu uislam uache kabisa, ni lini watu kama wewe mtajiamini, kwani unafikiri uislam ni weakness! kila kikisemwa kitu mkihusishe na kwa kuwa ni mwislam, loh, mnafanya ambao sio waislam wasiseme chochote au wasishiriki kumchambua kiongozi hususan akiwa mwislam, acheni hizo

Tatizo la kukimbilia kwenye pazia la udini ni la wale wenye kushindwa kujibu hoja au kuelemewa na ukweli au uzito wa hoja. Haya ni mambo ya kawaida watu kujadili kuhusu matazamio yao kwa candidates watarajiwa na kwa mitazamo hiyo tunawapa nafasi ya kutafakari na kufanya kile tunachotazamia.

Tuhuma alizohusishwa kuhusu mauaji ya Karume miaka 8-9 iliyopita, kama kiongozi mwadilifu, mwaminifu na shupavu mwenye kutaka kulinda heshima yake anatakiwa kutolea ufafanuzi na kuwaondolea watanzania shaka kama kilichoelezwa ni kwali au la. Vinginevyo kauli ile inabaki bado utata.
 
Katika masuala ya uadilifu anatakiwa ajibu hoja za kuchafuliwa katika kipindi cha kampeni za kugombea nafasi ya kuwakilisha CCM kiti cha Urais. Kukaa kimya bila kujibu mapigo yale ambayo yalitangazwa waziwazi hadharani ina maanisha alihusika. La sivyo kama anajiona hakuhusika kwa nini asiwachukulie hatua waliomchafua wakati tuhuma hizo zilikuwa nzito kuhusu mauaji?

Wanafalsafa husema kukaa kimya dhiti ya tuhuma zinazomkabili mtu ni kweli zinamhusu na hivyo dhamiri inamwuma, aidha tuhuma si za kweli lakini hajiamini katika kujenga utetezi.

Iwapo anashindwa kujenga utetezi katika masuala yanayomhusu binafsi atawezaje katika mambo mazito ya kitaifa?

Mkuu CANDID: Ni kweli tuhma zozote za uchafuzi binafsi (character assassination) ni vyema kuzijibu, kwa lengo la kujisafisha ikitegemea na hali ya mtoa tuhma hizo. Je? Chizi; Mtoto;Muhuni akikutuhumu utamjibu?
Kwa busara ya kawaida kama aliyoichukuwa Dr. SAS ni sawa (nature will take it's own course,and time will sort out for every thing). Pumba/Mchele/Mawe vitajulikana, kama tunavyo anza kushuhudia. IMEDHIHIRI!!!!!
 
Tuhuma alizotupiwa Salim zilitolewa na watu makini, maarufu, wenye akili timamu na hata wakishtakiwa wanasimamishwa mahakamani kama wenye akili timamu tena viongozi waaandamizi serikalini. Kutolewa tuhuma hizo waziwazi jukwani na yeye kunyamaa tu kwa miaka yote hii inatia shaka fulani ambalo umma ungependa kupata ufafanuzi au kauli yake mwenyewe.
 
Back
Top Bottom