Katika masuala ya uadilifu anatakiwa ajibu hoja za kuchafuliwa katika kipindi cha kampeni za kugombea nafasi ya kuwakilisha CCM kiti cha Urais. Kukaa kimya bila kujibu mapigo yale ambayo yalitangazwa waziwazi hadharani ina maanisha alihusika. La sivyo kama anajiona hakuhusika kwa nini asiwachukulie hatua waliomchafua wakati tuhuma hizo zilikuwa nzito kuhusu mauaji?
Wanafalsafa husema kukaa kimya dhiti ya tuhuma zinazomkabili mtu ni kweli zinamhusu na hivyo dhamiri inamwuma, aidha tuhuma si za kweli lakini hajiamini katika kujenga utetezi.
Iwapo anashindwa kujenga utetezi katika masuala yanayomhusu binafsi atawezaje katika mambo mazito ya kitaifa?
MWANDISHI UMEFANIKIWA KUONYESHA TOPE ZAKO ZA KICHWANI,TOFAUTI NA WENZIO AMBAO TOPE ZAO HUWA ZA MCHANGA,WEWE UMEONYESHA TOPE ZA MFINYANZI-Shame. On you! KWANI KAKWAMBIA ANATAKA URAIS,AU UNATAFUTA BWANA TUKUTOLEE POSA.
![]()
![]()
Dr. Salim Ahamed Salim (Tanzania) and Henry A. Kissinger (USA)
Dr. Salim Ahmed Salim ana jina kubwa nchini na kimataifa katika masuala ya kimataifa. He is a diplomatic figure. Naweza kumlinganisha na baadhi ya wanadipolamasia kama Henry Kissinger pamoja na umaarufu wao kimataifa hawakufaa kushika dola katika taifa.
Majukumu mazito aliyowahi kuyafanya kitaifa na kimataifa ni pamoja na:
Pamoja na umaarufu alioweza kuwa nao katika masuala ya kimataifa na kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania:
- Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Umoja wa Mataifa
- Katibu Mkuu Umoja wa nchi Za Afrika
- Mgombea Ukatibu Mkuu umoja wa Mataifa - hakupita
- Nafsi ya juu aliyowahi kuishika Tanzania ni kuwa Waziri Mkuu
- Hajaonyesha msimamo wake katika masuala ya kitaifa,
- Hayuko wazi
- Mkimya asiye weza kushirikisha aliyo nayo.
- Pamoja na kwamba ni mwana CCM sijawahi kuona ushirikishaji wa uongozi wake kwa CCM zaidi ya kuwa mhudhuriaji.
- Anaonekana kupokeleka zaidi kwa sura badala ya vitendo na fikra.
- Anaonekana kufaa shughuli za kiofisi zaidi kuliko siasa za majukwani.
Kwa mtazamo huu ana dira gani katika kuongoza Tanzania ya leo kama atagombea urais?
Je, Tanzania tuendelea kunadishwa majina makubwa ya wagombea urais pasipo kuonyesha uwezo wao?
Aaah Wapi,
Mmeshaanza siasa zenu za majitaka sasa,,
Hebu niambie wewe sasa.humpendi huyu kwa chuki zako binafsi au humpendi kwa kuwa yuko CCM??
Akisimama huyo 2015 hatuna budi kumpatia nchi hii,mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni..
Au kwa kuwa ni Muislam??
Kambi ya "mtaka urais maarufu" EDWARD LOWASSA @ WORK
Mnaweweseka sana wadau wa kambi ya mzee mzima,aliyewaambia salim anataka urais nani?yeye kaingizwa kamati kuu kwa lengo maalum,mtakuja kulikua huko mbele,ni mapema sana kwa sasa.
Hatuhitaji Tx kwani wao wanasema zanzibar ni nchi. Pili kweli Ccm wamekosa mtu hadi wssimamishe kibabu cha miaka80???? Bye bye Ccm kama mmefika hapo.
viongozi wakuu wote serikalini walilaani kitendo hicho na nasikia hadi fbi wameletwa kwa uchunguzi wa kina. ulitaka na dkt salim nae aseme?
Aaah Wapi,
Mmeshaanza siasa zenu za majitaka sasa,,
Hebu niambie wewe sasa.humpendi huyu kwa chuki zako binafsi au humpendi kwa kuwa yuko CCM??
Akisimama huyo 2015 hatuna budi kumpatia nchi hii,mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni..
Au kwa kuwa ni Muislam??
SAFI SANA! jibu mujarab.Mbona Kikwete alipewa,au naye si mwislam? BTW, Jemedali Mwislam Kikwete alimfanyia Zengwe na Fitna Mwislam mwingine Dr Salim A Salim. Hivyo MBWA KALA MBWA. The rest ni chuki na upungufu wa hekima kichwani.
TubinafsisheMkuu nani sasa anafaa kuwa rais kwa mtazamo wako.
Kubwajinga,
..kwa uelewa wangu,wakati Mkapa alipoingia madarakani alikuwa msafi kuliko Salim Salim. now, look at what he did alipokuwa madarakani!! binafsi siwaamini hawa wanafunzi wa Nyerere. nadhani ni wasafi kwasababu ya kumuogopa Mwalimu.
..kuhusu uwezo wake wa kuongoza, pamoja na uelewa wake wa dunia vs mahitaji ya nchi, sidhani kama Salim Salim ana lolote jipya. binafsi rekodi yake ya OAU hainivutii kwasababu aliishia kuifanya kama kijiwe cha Muamar Gaddafi. wa-Liberia hawataki hata kumsikia huyu bwana. wakati wa mgogoro na mauaji ya DRC, OAU and Salim Salim were missing.
..mwisho, kwa hapa nyumbani Salim Salim ametumikia wizara ya mambo ya nje, pamoja na wizara ya ulinzi. sasa pamoja na umuhimu wa wizara hizo, I would rather consider mawaziri wenye uzoefu na waliofanya vizuri ktk wizara za sekta zinazogusa moja kwa moja maisha ya Mtanzania.
NB:
..Kibwajinga, kama tunataka Mtanzania na mwana CCM mwenye rekodi ya kimataifa, na aliyeipata kwa nguvu zake mwenyewe, on merit, basi ni Prof.Anna Tibaijuka[PhD].
Kiongozi yeyote shupavu asiyetoka ccm. Mtu kama Salim akitaka kuwa kiongozi mzuri hawezi. Ni mtu asiyeguswa kabisa na uongozi mbovu na uliokuwepo na matatizo ya wananchi hivyo hatofanya kitu tofauti. Bora hata Joseph Sinde Waryoba ambaye wanaendana na Salim japo yuko ccm lakini anakerwa na upuuzi wakati mwingine anaupigia kelele. Wote hawafai.Mkuu nani sasa anafaa kuwa rais kwa mtazamo wako.
Kiongozi yeyote shupavu asiyetoka ccm. Mtu kama Salim akitaka kuwa kiongozi mzuri hawezi. Ni mtu asiyeguswa kabisa na uongozi mbovu na uliokuwepo na matatizo ya wananchi hivyo hatofanya kitu tofauti. Bora hata Joseph Sinde Waryoba ambaye wanaendana na Salim japo yuko ccm lakini anakerwa na upuuzi wakati mwingine anaupigia kelele. Wote hawafai.
Salim kuwa rais ni sawasawa na rubani mzee ambaye siku nyingi hajaendesha ndege siku nyingi kupewa ndege lakini iliyoharibika matairi, imetoboka kioo cha mbele na vifaa vyake ni vibovu kabisa. Ndege ikiwa ccm. Hata angekuwa rubani kijana kabisa mwenye uwezo wote wa kuendesha ndege za hao abiria hawatafika salama.