Warioba: Mimi na Salim urais basi

Si tu hafai kuwa Rais wa nchi hii bali, kitendo cha Vurugu za Kidini zinawakosesha baadhi ya Watarajiwa uhalali wa kuliongoza taifa hili linajinasibu kutokuwa na Dini....Je kama CCM watamteau kugombea na ikatokea kwa BAHATI MBAYA akawa rais hataweza kutuliza mukari na hasira za kundi la dini linalodai linaonewa na kukandamizwa.

Maana kwa sasa Viongozi walioko madarakani wanatoka upande huo na mambo ndio haya.. Je yeye akibahatika kuunyaka Urais je anayomikakati gani ya Kuyalinda makundi ya dini zote......Tumechoka sana kuona pande hizi mbili zinanyanyasana, hasa upande mmoja unaonekana kuwa na jazba na kusababisha madhara makubwa kwa upande wa pili...."

Watanzania bado tuna wasiwasi na wagombea wengi toka CCM, vinginevyo watamke waziwazi ni mbinu gani watazitumia kuondoa kirusi hiki cha Udini kilichotamaraki kwa sasa..Vinginevyo tuwajaribu wapinzani kwani kwao pana uwezekano wa kukiua kirusi cha udini, na labda tutapambana na swala na rushwa na ukabila ambao kwa nchi kama Tanzania si tatizo kuukemea na kuuzika kabisa... Udini ni noma...
 
Aaah Wapi,

Mmeshaanza siasa zenu za majitaka sasa,,

Hebu niambie wewe sasa.humpendi huyu kwa chuki zako binafsi au humpendi kwa kuwa yuko CCM??

....
Au kwa kuwa ni Muislam??

Lakini mleta mada hajagusia suala la dini wala Uislamu wa Dk Salim.
Wewe, kwa inferiority uliyo nayo, kutojiamini uliko nako, na udini ulionao umechomeka Uislamu na Udini!
Nilikuwa sijui kama Dk Salim ni Muislam, au unaswali naye Msikiti mmoja?
 
Aaah Wapi,

Mmeshaanza siasa zenu za majitaka sasa,,

Hebu niambie wewe sasa.humpendi huyu kwa chuki zako binafsi au humpendi kwa kuwa yuko CCM??

Akisimama huyo 2015 hatuna budi kumpatia nchi hii,mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni..

Au kwa kuwa ni Muislam??

kwenye nyekundu hapo ndo alipotufikisha bwana maendeleo, mtu akipigwa au kukubalika huwa mnaanza kuangalia dini ya anayemkubali na anayekubalika, hili tatizo kubwa sana kwa sasa!
 
Mbona Kikwete alipewa,au naye si mwislam? BTW, Jemedali Mwislam Kikwete alimfanyia Zengwe na Fitna Mwislam mwingine Dr Salim A Salim. Hivyo MBWA KALA MBWA. The rest ni chuki na upungufu wa hekima kichwani.

Umenikumbusha lile andiko; " mjibu mpumbavu kwa kadiri ya upumbavu wake."
Kwa kuwa hekima ya Dulla na Njiwa zinalingana, watakuwa wamepata majibu mujarab.
 
Mleta mada ameweka hoja zake, jaribu kuleta hoja za utetezi badala ya kujibu kimipasho. Hapa hatujadiri mambo mengine katika mada hii zaidi ya kupima uwezo wa presidential candidates, tunahaki ya kupima uwezo wao mapema badala ya kutumbukiza tu kura sandukuni baadaye tuje kulalamikia uwezo wao kuwa mdogo kuongoza watanzania.

Candid Scope ni Mtazamo tuuh,usijenge chuki..

Unaweza kuuchukua au kuupuzia..

Jukwaa huru hili..
 
Lakini mleta mada hajagusia suala la dini wala Uislamu wa Dk Salim.
Wewe, kwa inferiority uliyo nayo, kutojiamini uliko nako, na udini ulionao umechomeka Uislamu na Udini!
Nilikuwa sijui kama Dk Salim ni Muislam, au unaswali naye Msikiti mmoja?

Jamaa yuko imara sana,tuache ubishi katika hilo..
 
Lakini mleta mada hajagusia suala la dini wala Uislamu wa Dk Salim.
Wewe, kwa inferiority uliyo nayo, kutojiamini uliko nako, na udini ulionao umechomeka Uislamu na Udini!
Nilikuwa sijui kama Dk Salim ni Muislam, au unaswali naye Msikiti mmoja?

Tunatamani tuwe na rais mwenye kudhubutu bila kuuma uma maneno pale inapotokea maswala nyeti yanayotishia ustawi wa taifa letu... kwani swala la kuchinjana na kuchoma nyumba za ibada wewe unaliona ni zuri. Ni vema tuwe wazi kwani udini kwa sasa siyo jambo la kuficha, na madahara yake yako wazi kabisa......
 
Si tu hafai kuwa Rais wa nchi hii bali, kitendo cha Vurugu za Kidini zinawakosesha baadhi ya Watarajiwa uhalali wa kuliongoza taifa hili linajinasibu kutokuwa na Dini....Je kama CCM watamteau kugombea na ikatokea kwa BAHATI MBAYA akawa rais hataweza kutuliza mukari na hasira za kundi la dini linalodai linaonewa na kukandamizwa. Maana kwa sasa Viongozi walioko madarakani wanatoka upande huo na mambo ndio haya.. Je yeye akibahatika kuunyaka Urais je anayomikakati gani ya Kuyalinda makundi ya dini zote......Tumechoka sana kuona pande hizi mbili zinanyanyasana, hasa upande mmoja unaonekana kuwa na jazba na kusababisha madhara makubwa kwa upande wa pili...." Watanzania bado tuna wasiwasi na wagombea wengi toka CCM, vinginevyo watamke waziwazi ni mbinu gani watazitumia kuondoa kirusi hiki cha Udini kilichotamaraki kwa sasa..Vinginevyo tuwajaribu wapinzani kwani kwao pana uwezekano wa kukiua kirusi cha udini, na labda tutapambana na swala na rushwa na ukabila ambao kwa nchi kama Tanzania si tatizo kuukemea na kuuzika kabisa... Udini ni noma...
Hakuna vurugu za kidini Tanzania.Unachokiona ni 'mbojo' tu -kimetengenezwa. Watanzania hatuwezi kugawanywa kwa ukabila kwa kuwa makabila yako mengi.Tunaweza kugawanywa kwa udini kwa vile dini kubwa zipo mbili tu.Inabidi tuwe makini. 'Media' nazo zimekuwa 'compromised'..
 
Mbona Kikwete alipewa,au naye si mwislam? BTW, Jemedali Mwislam Kikwete alimfanyia Zengwe na Fitna Mwislam mwingine Dr Salim A Salim. Hivyo MBWA KALA MBWA. The rest ni chuki na upungufu wa hekima kichwani.

sijakuelewa bado .... point yako ni nini hasa ..?
 
kuwa kimya ni hekima kutoka kwa mungu. by edward n lowassa

Sikupingi kwamba wenye falsafa ya hali ya juu si wazungumzaji sana, lakini ni watu wenye kutoa mada na ukweli unaofikirisha na wenye hekima. Lakini kukaa kimya tu hata kutoonyesha msimamo wake katika mambo mazito yatokeayo nchini, ni dalili ya kwamba uwezo wake mdogo, amezoea mambo ya ofisini zaidi si majukwaani.

Akiwa mkuu wa nchi ataongoza kwa kukaa kimya?
 
Hz sio siasa za majitaka wakuu. Binafsi sijawahi kumsikia huyu ndugu akijadili au kutoa kauli yeyote kupinga, kukubali au kusisitiza jambo. Kwa ujumla haeleweki. Penye ukweli tuzungumze jamani. Inaonyesha hana msimo.
 
sijakuelewa bado .... point yako ni nini hasa ..?
Kwamba Mleta uzi alitaka kuleta chuki za kumkataa SAS kwa Uislam wake,kama ulivyompongeza Dula .. Bila kukumbuka kwamba Pamoja na Uislam wake huyu SAS alipigwa zengwe ambalo kama ningekuwa mimi hata koti lenye rangi ya kijani ningetia Moto.!
 
L.Col_Members_SalimSalim.jpg
images

Dr. Salim Ahamed Salim (Tanzania) and Henry A. Kissinger (USA)

Dr. Salim Ahmed Salim ana jina kubwa nchini na kimataifa katika masuala ya kimataifa. He is a diplomatic figure. Naweza kumlinganisha na baadhi ya wanadipolamasia kama Henry Kissinger pamoja na umaarufu wao kimataifa hawakufaa kushika dola katika taifa.

Majukumu mazito aliyowahi kuyafanya kitaifa na kimataifa ni pamoja na:
  • Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Umoja wa Mataifa
  • Katibu Mkuu Umoja wa nchi Za Afrika
  • Mgombea Ukatibu Mkuu umoja wa Mataifa - hakupita
  • Nafsi ya juu aliyowahi kuishika Tanzania ni kuwa Waziri Mkuu
Pamoja na umaarufu alioweza kuwa nao katika masuala ya kimataifa na kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania:

  1. Hajaonyesha msimamo wake katika masuala ya kitaifa,
  2. Hayuko wazi
  3. Mkimya asiye weza kushirikisha aliyo nayo.
  4. Pamoja na kwamba ni mwana CCM sijawahi kuona ushirikishaji wa uongozi wake kwa CCM zaidi ya kuwa mhudhuriaji.
  5. Anaonekana kupokeleka zaidi kwa sura badala ya vitendo na fikra.
  6. Anaonekana kufaa shughuli za kiofisi zaidi kuliko siasa za majukwani.

Kwa mtazamo huu ana dira gani katika kuongoza Tanzania ya leo kama atagombea urais?
Je, Tanzania tuendelea kunadishwa majina makubwa ya wagombea urais pasipo kuonyesha uwezo wao?
Candid Scope , kwa kweli kumlaumu Salim Ahmed Salim katika siasa za maji taka za siku hizi ni kumwonea tu.
Huyu ni mmoja wa viongozi waadilifu na watiifu mno nchi hii.

Tumeona jinsi alivyoumizwa katika kinyang'anyiro cha urais wa mwaka 2005.
Lakini alivyo mstaarabu hkujibu neno, na yuko kimya kabisa.
Hii ni pamoja na ukweli kuwa alishafikiaa ngazi ya juu kabisa katika uongozi wa Tanzania -Uwaziri Mkuu.

Sasa kumtaka zaidi naona n kumwonea tu, na wala hajatamka kuutaka urais, maana hata kwa kutazama tu waliomuumiza mwaka 2005 ni mitandao ile ile iliyopo.
 
kuwa kimya ni hekima kutoka kwa mungu. by edward n lowassa

Hapana ukimya unategemea na mahali na mazingira. Sasa ukiwa kimya hata unapoona wananchi wanateseka au watanzania kuanza kuulizana dini hapo hekima inatoka wapi?
 
Hz sio siasa za majitaka wakuu. Binafsi sijawahi kumsikia huyu ndugu akijadili au kutoa kauli yeyote kupinga, kukubali au kusisitiza jambo. Kwa ujumla haeleweki. Penye ukweli tuzungumze jamani. Inaonyesha hana msimo.

Hilo ndilo ninaloliona mimi. Unaweza kuona akina Lowasa, Sitta na wengine hujaribu kuonyesha misimamo yao, lakini huyu Salim ni usindikizaji tu.
 
Candid Scope , kwa kweli kumlaumu Salim Ahmed Salim katika siasa za maji taka za siku hizi ni kumwonea tu.
Huyu ni mmoja wa viongozi waadilifu na watiifu mno nchi hii.

Tumeona jinsi alivyoumizwa katika kinyang'anyiro cha urais wa mwaka 2005.
Lakini alivyo mstaarabu hkujibu neno, na yuko kimya kabisa.
Hii ni pamoja na ukweli kuwa alishafikiaa ngazi ya juu kabisa katika uongozi wa Tanzania -Uwaziri Mkuu.

Sasa kumtaka zaidi naona n kumwonea tu, na wala hajatamka kuutaka urais, maana hata kwa kutazama tu waliomuumiza mwaka 2005 ni mitandao ile ile iliyopo.

Kuna wengi tu waliotendewa mabaya zaidi ya Salim kama Mwakiembe hadi kukimbizwa hospitalini India, lakini kwenye ukweli na kupinga maovu wanajitokeza. Kunyamaza huko hakuleti picha nzuri kama anataka kuwa kiogozi bora wa wananchi. Anatakiwa kuonyesha msimamo wake katika kuwatetea na kuwapigania wananchi. Vinginevyo uadilifu katika maisha si kigezo pekee cha kufaa kuingia magogoni. Tunao waadilifu wengi lakini wengi wao hawafai kuongoza nchi.
 
Kwamba Mleta uzi alitaka kuleta chuki za kumkataa SAS kwa Uislam wake,kama ulivyompongeza Dula .. Bila kukumbuka kwamba Pamoja na Uislam wake huyu SAS alipigwa zengwe ambalo kama ningekuwa mimi hata koti lenye rangi ya kijani ningetia Moto.!

sidhani kama ulinisoma sahihi.. hakuna sehemu niliyompongeza dula "kwa lile swali alilouliza" au kusema kwamba mleta uzi anamkataa salim kutokana na uislam wake...

nimempogeza dula kwa kusoma btw lines kuona kwamba hakuna lolote zaidi ya siasa za majitaka....

sijaingiza dini katika post zangu ndani ya hii thread :nono: naona umehamaki naku replay kwa hisia zaidi baada ya kuona aliyejibu ni njiwa , na kwa standard zenu JF njiwa ni mdini kwasababu anajiweka wazi yeye ni muislam humu JF
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom