I concur with you
Mungo Park.
Labda tu la kuongezea ni kwamba nionavyo mimi SAS hafai kuwa Rais ajaye wa Tanzania na sababu ni simple sana, nayo ni kwamba hatujui msimamo wake ukoje kwenye mambo mbalimbali pamoja na ya msingi yanayoikabili nchi yetu hasa katika kipindi hiki cha mpito chenye kushuhudia a great political and socio-economic transformation katika jamii yetu, mfano mzuri ni utungaji wa katiba mpya, uchumi kuwa determined na nguvu ya soko na kuendeshwa na sekta binafisi zaidi kuliko uchumi hodhi wa serikali/nchi.
Namuona SASA kama ni mkimya sana hata kwenye mambo ya msingi yanayotokea kila siku be political, social, economical ect.
Lakini pia na muhimu sana ni kwamba hatuna track record yake kwenye utendaji, ubunifu na usimamizi katika nafaso alizowahi kuzishika au hata kwenye maisha yake binafis. Zaidi tuu ya kupata pengine 'bahati' ya kushika nyadhifa nyingi za kidplomasia na labda ilitokea tu by chance au bahati sioni any other added advantage aliyo nayo.
Labda ili tumfahamu tujaribu kumulika kule alikokuwa katibu mkuu metendaji wa OAU. Je by then ni yepi atajivunia kama ni mchango wa ubunifu au utendaji wake? Anayefahamu anitajie....
Kiukweli kosa kubwa tutakalofanya watanzania this time ni kuchagua mtu kutokana na jina lake au umaarufu wake bila kuangalia track record yake katika utendaji, ubunifu na uadilifu. Rais Kikwete alipata kuwa rais kwa sababu watanzania hatukuwahi kuhoji hayo maswala ya msingi juu yake: utendaji, ubunifu na uadilifu. Tuliangalia zaidi jina na umaarufu wake bila kuangalia track record yake katika haya. Wote leo hii kwa namna mbalimbali you can attest this country is run in auto-pilot mode, wakati JK yupo bize anakata naga daily...
Lakini pia by 2015 Salim atakuwa na miaka 70 na nadhani umri pia utakuwa umemtupa mkono. Nafasi ya rais inahitaji nguvu ya kimwili na kiakili. kwa umri huo dementia, brain atrophy and degeneration zinamhusu.na hii huwapata kwa wingi sana watu wa umri huu. Hata yeye hayupo spared katika hilo. Lakini pia siasa ya dunia ya sasa tunashuhudia ilivyo na mikiki mikiki, nadhani inahitaji zaidi 'vijana'
Kwa ufupi SAS hatufai kuwa rais wetu. Tunamhitaji rais mwenye sifa tukuta katika hayo maeneo niliyoainisha: utendaji, ubunifu na uadilifu. Short of this we are doomed kwa miaka mingine na tutakuwa tunapiga mark time sana tu wakati wenzetu wanakimbia.
Kindly naomba tujadili kwa hoja na si udini wa mtu. Dini yake inamhusu yeye na Mungu wake. Siku ya hukumu kila mtu atapeleka hesabu yake yeye mwenyewe na atahukumiwa yeye mwenyewe kadri ya matendo yake bila kujali kikundi cha dini.
Asanteni