Nyundo_tz
JF-Expert Member
- Jul 14, 2009
- 640
- 21
WAZIRI Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais (mstaafu), Jaji Joseph Warioba, amesema kwamba hana tena ndoto za kuwania urais kama ilivyo kwa Waziri Mkuu mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim ambapo, kwa nyakati tofauti, wote waliwahi kujitokeza kuwania bila mafanikio.
Viongozi hao ambao bado ni wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kimya cha muda mrefu hivi karibuni walijitokeza na kutoa maoni yao kuhusu mwenendo wa nchi, wakikosoa baadhi ya maeneo ya kiutendaji na hata kutoa mapendekezo kwa lengo la kuboresha, walipozungumza na baadhi ya vyombo vya habari jijini Dar es Salaam.
"Mimi na Salim (Dk. Salim Ahmed Salim) hatuna tena mpango wowote wa kutaka urais," alisema Jaji Warioba, na alipoulizwa ni kwa nini wameamua hivyo, akaeleza kuwa ni kutokana na kigezo cha umri.
'‘Tumekaa madarakani na kuongoza wananchi, tumekuwa viongozi wa wananchi, tunajua pilikapilika za uongozi, na hasa kwa nchi masikini kama Tanzania, umri nao ni suala la kuzingatia sana. Tungeweza kufanya kazi hiyo vizuri kwa wakati ule tulipojitokeza kutaka urais na si wakati huu,'' alijibu Jaji Warioba wakati wa kuhitimisha maoni yake alipozungumza na waandishi wa habari, ofisini kwake jijini Dar es Salaam, hivi karibuni.
Katika majibu ya swali hilo la Raia Mwema lililoulizwa mbele ya waandishi wengine wa habari waliohudhuria mkutano huo, Jaji Warioba alikiri moja kwa moja kusikia mazungumzo hayo kutoka kwa watu mbalimbali wakiwamo baadhi ya viongozi kuwa amekuwa na lengo la kutaka kuwania tena urais.
'‘Hilo unaloniuliza ni kweli; nami nimesikia. Wanasema nataka urais ... nitagombea urais,'' alikiri kusikia Jaji Warioba ambaye aliwahi kuwa Waziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Rais wakati wa Serikali ya Awamu ya Pili, Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Serikali ya Awamu ya Kwanza chini ya Mwalimu Julius Nyerere na Waziri wa Sheria na Katiba.
Katika mazungumzo yake kwa waandishi wa habari, Jaji Warioba alielezea mtazamo wake kuhusu masuala mbalimbali yakiwamo yanayohusu uendeshaji nchi, kuzidi kutanuka kwa pengo kati ya matajiri na masikini kuanzia serikalini ambako mshahara wa kima cha chini umetofautiana kwa kiasi kikubwa na kima cha juu.
Pia aliweka bayana kuwa utawala umekuwa karibu mno na matajiri kuliko wananchi wa kawaida, akirejea baadhi ya mifano ukiwamo wa baadhi ya wafugaji kutoka eneo la Loliondo, nje ya mji wa Arusha kujikusanya nje ya lango la Ikulu, Dar es Salaam wakati walikotoka kuna viongozi wa serikali ambao kimsingi ni wawakilishi wa Rais.
Kwa mujibu wa Jaji Warioba, kitendo hicho kinaonyesha namna utawala unavyotofautiana na wananchi katika baadhi ya uamuzi, akionya kuwa ni hatari hali hiyo ambayo licha ya nchi kuwa na utawala wananchi wanaanza kujifanyia mambo kwa taratibu zao binafisi.
Katika ufafanuzi wake, alisema si vibaya kwa wananchi kutaka kuonana na Rais, lakini alitarajia ruksa hiyo wangeipata baada ya kufanyiwa mipango na viongozi wao wa huko walikotoka na si wao binafsi na kwamba huo ni ushahidi wa kuwapo kwa kile alichoeleza kuwa ni credibility gap katika uongozi wa nchi.
Hata hivyo, baada ya ukosoaji huo na mapendekezo yake, baadhi ya viongozi wa CCM walijitokeza kuzungumzia maoni hayo katika tafsiri zinazokinzana.
Wakati Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa akisema Jaji Warioba ana haki ya kutoa maoni yake hayo, Katibu wa Fedha na Uchumi wa chama hicho, Amos Makala, alimshambulia akionyesha dhahiri kutokukubaliana na kitendo cha Warioba kutumia fursa yake ya kutoa maoni hadharani, akisema angepaswa kuyatoa kupitia vikao vya chama hicho kwa kuwa yeye ni mwanachama.
Amos Makala, ambaye naye hakutumia vikao kuwasilisha maoni yake kupinga mtazamo wa Jaji Warioba na badala yake alitumia moja kwa moja vyombo vya habari, katika mashambulizi yake alirejea kinyang'anyiro cha Uchaguzi Mkuu wa 2005, ndani ya CCM, wakati wa kumtafuta mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho.
Kwa mujibu wa maelezo ya Makala, katika kinyang'anyiro hicho, Jaji Warioba alikuwa akimuunga mkono mgombea Dk. Salim aliyekuwa akichuana na wagombea wengine, akiwamo Rais Jakaya Kikwete ambaye aliibuka na ushindi akifuatiwa na Dk. Salim, pamoja na Waziri wa sasa wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya.
Wagombea wengine kwa wakati huo ni pamoja na aliyewahi kuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais, Dk. John Malecela ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Mtera, mkoani Dodoma, aliyekuwa Waziri Mkuu, Frederick Sumaye, waliowahi kuwa mawaziri ambao ni Iddi Simba, Dk. Abdallah Kigoda, Dk. William Shija. Wengine ni John Shibuda ambaye ni Mbunge wa Maswa, Balozi Patrick Chokala na Balozi Ali Karume.
Mashambulizi hayo ya Makala yaliweka bayana kuwa katika kinyang'anyiro hicho cha 2005, kama Dk. Salim angefanikiwa kuteuliwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya CCM, basi Jaji Warioba angekuwa mgombea mwenza (Makamu wa Rais) wake, kwa kuwa Dk. Salim anatoka Zanzibar na taratibu zinaelekeza kuwa, kama Rais anatokana Tanzania Bara, Makamu lazima atoke Zanzibar au kinyume chake.
Alidai kuwa ukosoaji wa Jaji Warioba umejaa kisasi cha kushindwa katika kinyang'anyiro hicho cha urais. Katika majibu yake, Jaji Warioba alieleza kuwa ametoa ushauri tu na kwamba ni jukumu la walioko madarakani kuzingatia au vinginevyo na zaidi, hakuzungumzia watu binafsi, bali alizungumzia masuala yanayohusu mustakabali wa taifa.
Suala la ukosoaji wa serikali au viongozi walioko madarakani kutoka kwa viongozi wastaafu ni utamaduni wa muda mrefu ambao mwasisi wake ni Mwalimu Julius Nyerere, ambaye wakati wa utawala wa Serikali ya Awamu ya Pili iliyokuwa ikiongozwa na Ali Hassan Mwinyi, aliikosoa tena akiwalenga moja kwa moja viongozi waandamizi waliokuwa serikalini, akiwamo Waziri Mkuu wa wakati huo, Dk. John Samuel Malecela.
Malecela alipata kukosolewa wazi wazi na Mwalimu Nyerere ambaye alikuwa mstaafu kwa wakati huo, kuhusu kile kilichoelezwa kuwa kuruhusu au kuunga mkono wazo la kuundwa kwa serikali tatu, ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hoja hiyo ya Serikali tatu, ambazo ni Tanganyika, Zanzibar na Serikali ya Muungano, chimbuko lake ni kundi la wabunge lililojitambulisha kwa jina la G55.
Hoja hiyo iliibuka wakati Zanzibar kwa ridhaa ya aliyekuwa Rais wa visiwa hivyo, Dk. Salmini Amour ilipotaka kujiunga na Jumuiya ya Nchi za Kiislamu Duniani (OIC) bila ya kuwa na hadhi hiyo kama nchi, na kwamba kujiunga au kutojiunga kulipaswa kufanywe na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na si Zanzibar.
Nyerere alimlaumu Malecela wazi wazi, tena hadharani kwa wakati huo akiwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais, kwamba ameshindwa kumshauri vizuri Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu namna ya kudhibiti suala hilo na mahsusi hoja ya serikali tatu.
Aidha, Mwalimu Nyerere pia aliwahi kumkosoa hadharani aliyekuwa Mwinyi na serikali yake kwamba haikuwa ikikusanya kodi kutoka kwa wafanyabiashara wakubwa na badala yake ‘inakimbizana' na wafanyabiashara wadogo mitaani, akiweka bayana kuwa hiyo ni sifa ya ‘viji-serikali corrupt.'
Mwalimu Nyerere ambaye pia alikuwa miongoni mwa wasisi wa chama cha TANU ambacho baadaye kiliungana na ASP na kuwa CCM na kuwa mwenyekiti wa kwanza wa CCM, alikuwa akifanya ukosoaji huo hadharani na wakati mwingine katika baadhi ya maeneo serikali ilizingatia ukosoaji wake na wakati fulani kupuuza.
Source: Raia Mwema