Kwa jinsi siku zinavyopita, Kuna hatari ya nchi kupata Rais 2015 ambaye ni bogus zaidi ya Marais waliopata kuliongoza Taifa tokea tupate uhuru. Jamii kwa sasa imeanza kuona Rais bora ni yule mwenye imani ya dini kama wao bila kujali uwezo wake. Taifa limeanza kuonyesha dalili zote za kuelekea Taifa Mfu. Kwa Watanzania wengine wenye upofu wa fikra, Mwanasiasa mahili ni yule anayepiga kelele majukwaani bila hata ya kujua mipaka ya matamshi yake. Unfortunate, Salim Ahmed Salim hayupo kwenye haya makundi na siyo ajabu, kwa sasa ameanza kuzodolewa kwa sababu kwao, anaonekana hana vazi la Urais.
SAS ni mwanadiplomasia, na msingi mkuu wa kuwa mwanadiplomasia mahili ni kuwa CALM, COLLECTED AND ON BALANCE.
Ni kitu cha kushangaza pale watu wanamtaka aende sokoni kujiuza kama wanaSiasa wengine wanavyofanya kwa sasa. Salim Ahmed Salim hahitaji kwenda sokoni kujiuza kwa sababu kazi hiyo aliisha ifanya siyo kwa Tanzania tu bali hata katika mataifa. Pale alipopewa kazi ya kufanya katika nchi au mataifa, aliifanya kwa uadilifu na ufanisi mkubwa. What more you want!!.
Please
Candid Scope , usichanganye bidhaa za kisiasa zinazojiuza kwa sasa na bidhaa iliyojipambanua tayari ndani ya soko la kisiasa.