dkt salim ni muungwana. muungwana ni vitendo. kwa bahati mbaya kizazi cha sasa hawaelewi utendaji wake. alifanya mambo mengi lakini ikumbukwe kuwa MWL NYERERE HUKUPENDA JINA LA MTU MMOJA MMOJA LIPANDE. ALIPENDA SANA KUTUKUZWA YEYE. HAKUWAPA MAWAZIRI WAKE FURSA YA KUAMUA NA KUTENDA KAMA WANAVYO FANYA AKINA MAGUFULI NA MWAKYEMBE hivi sasa. nilipokua chuoni, profesa mmoja aliwahi kutuambia kuwa mwalimu amelifanyia taifa letu mengi lkn hakupenda mawaziri wake wasifiwe au waonekane kuwa wanatenda. alipenda mipango ypte apelekewe yeye ili yeye ndiyo aitekeleze. marehemu sokoine aliwahi kukwamishwa na mwalimu katika kasi yake ya kuirekebisha nchi yetu. hii ni kutokana na kumuonea wivu. vilevile alimuona kama HATARI kwa utawala wake. mwalimu alipenda anaeharibu ahamishiwe sehemu nyingine lkn sokoine aliaumuru anaeharibu afukuzwe. hiyo siyo mada ya leo tuachane nayo.
dkt salim ni mtu makini azungumzapo na atendapo. hotuba aliyoitoa chimwaga mwaka 2005 wakati anaomba kuchaguliwa kugombea urais kwa tiketi ya ccm ni kielelezo kuwa uwezo na dira anavyo. hana asili ya kupayuka. kuna watu wanadhani kupayuka ndiyo utendaji. la hasha. kuna mabadiliko makubwa ambayo wakurugenzi wa nsssf na nhc wameyafanya lkn licha ya utendaji wao mzuri, siyo watu wa kujitokeza kujisifu ili waonekane.
dkt salim aliongoza oau ktk mazingira magumu. viongozi wengi walisema kuwa oau haifai kuwepo kwa sababu nchi nyingi zimeshapata uhuru. dkt salim alijitahidi kuzihamasisha kuwa chombo hicho ni muhimu na lazima nchi zichangie ili kukifanya kiwepo. baadaye aka andaa dira ya kubadilisha oau kuwa AU. yakaundwa malengo mapya ya au. LA MSINGI ZAIDI SALIM NI MTU SAFI. HANA KASHFA YA RUSHWA KATIKA UTENDAJI WAKE. mwl nyerere aliwahi kusema kuwa "kimataifa mtanzania namba moja ambaye ameifanya TZ ijulikane na kuheshimika ni dkt salim. alijenga hoja UN akifafanua self reliance (kujitegemea) ambayo tanzania inaifuata. aliiongoza oau na kuifanya kiwe chombo cha kuaminika".
kwa ccm ya sasa, salim ni chaguo bora kwa sababu hayumo katika makundi yanayo chafuana. amekua kimya kwa miaka 8 kwa sababu alichafuliwa sana mwaka 2005 na JK. aliona kuwa njia salama ya kumfanya awe na amani, ni kukaa kimya. alichafuliwa sana!
akipitishwa lowassa lazima akina sitta, membe nk..... hawatomuunga mkono. na kinyume chake ni sahihi. akipitishwa salim, wote watamuunga mkono kwa sababu amepewa mtu ambaye hayumo vitani. kinacho onesha kuwa hapendi rushwa, mwaka juzi kamati anayoiongoza ya MO IBRAHIM iliamua kuwa hakuna kiongozi mstaafu mwenye sifa ya kupewa tuzo. salim alisema wasubiri hadi miaka 2-3 ijayo.
kiafya salim bado ana nguvu na anaonekana vizuri. lowassa sasa hivi ni dhaifu kiafya. slaa ana nguvu lkn mkono naona umeshalemaa! lipumba amechokwa, mrema hoi na mbatia amekiua chama. tukiweka uzalendo pembeni, salim is the right choice to be the fifth president of TZ