Wapi Wanauza Power bank za uhakika?

Somi

JF-Expert Member
Feb 7, 2009
3,605
4,360
Kutokana na umeme kutokuwa wa uhakika ni vyema kuangalia plan B.

Ni wapi wanauza power bank za uhakika zisizo feki zenye guarantee?

Wadau wenye kujua tujulishane.
 
Kuhusu suala la Powerbank Wachina tuwape maua yao,

Ni kweli wanaweza wasiwe wazuri kwenye bidhaa nyingine lakini kwenye masuala ya Battery wachina wako juu kuliko wazungu...

Hata kampuni nyingi za Ulaya na Marekani zinapofikiria suala la battery za uhakika kwenye product zao wanatumia zaidi makampuni ya China

Chukua Oraimo au Xiaomi wako vizuri sana
Zaidi sana Oraimo. Hutojutia.
 
Upo sasa brother , Hata sasahivi wamegundua betri za magari ya umeme zenye kuhifanyi chaji kwa umbali mrefu zaidi wa safari kuliko betri zote za kipindi hiki .
 
Kutokana na umeme kutokuwa wa uhakika ni vyema kuangalia plan B.

Ni wapi wanauza power bank za uhakika zisizo feki zenye guarantee?

Wadau wenye kujua tujulishane.
Powerbank za Xiaomi huwa ni nzuri, around 80,000 hivi unaweza pata yenye Mah 20,000 na fast charging ya 50W ambayo ni multipurpose kusukuma vitu vingi tofauti na simu, Vitu vya kisasa vyenye usb C power delivery kama Laptop, Monitor, Feni etc utasukuma.

Kama budget ndogo hao hao Xiaomi wana powerbank hizo hizo za huo ukubwa ila bila fast charging features unakuta kawaida 10-18W nafikiri hizi around 50,000 hivi.
 
Kuhusu suala la Powerbank Wachina tuwape maua yao,

Ni kweli wanaweza wasiwe wazuri kwenye bidhaa nyingine lakini kwenye masuala ya Battery wachina wako juu kuliko wazungu...

Hata kampuni nyingi za Ulaya na Marekani zinapofikiria suala la battery za uhakika kwenye product zao wanatumia zaidi makampuni ya China

Chukua Oraimo au Xiaomi wako vizuri sana
Zaidi sana Oraimo. Hutojutia.
China sababu ya Bei, ila Japan hana mpinzani tech ya battery.
 
Kuhusu suala la Powerbank Wachina tuwape maua yao,

Ni kweli wanaweza wasiwe wazuri kwenye bidhaa nyingine lakini kwenye masuala ya Battery wachina wako juu kuliko wazungu...

Hata kampuni nyingi za Ulaya na Marekani zinapofikiria suala la battery za uhakika kwenye product zao wanatumia zaidi makampuni ya China

Chukua Oraimo au Xiaomi wako vizuri sana
Zaidi sana Oraimo. Hutojutia.
Yeah sure ni miaka 5 nilinunua oraimo enzi hizo niliku chaka tu chaka site ila bado ipo mpaka leo ina nisaidia kwa jinsi tanesco wanavyo tunyoosha na mgao.. bado ipo vizuri kama sikosei nilichukua elfu 45 au 55
 
Jamani hizo aina nzuri za power bank mnazozisema basi muambatanishe za picha zake ili tukienda dukani tukomae na hzohizo

Binafsi niko Mashambani Huku na umeme ni shida sana,, mwezi uliopita nilinunua power bank ya Samsung Mah 20800 Ila Cha kushangaza haijazi hata Simu Ndogo😥😥😥
 
Back
Top Bottom