Kenya ya 3 kwa Umeme wa uhakika wakati Tanzania umeme ni anasa

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,547
41,060
Kati ya vigezo vya kupima maendeleo ya nchi ni pamoja na kiwango cha nishati ambacho kwa wastani, kila mwananchi hutumia.

Huwezi kuwa na maendeleo kama huna nishati ya uhakika, inayotosheleza na inayoaminika.

Nchi 10 zinazoongoza kwa ubora wa upatikanaji wa nishati ya umeme Afrika, majirani zetu Kenya ni nchi ya tatu:

According to energycapitalenergy.com, below are the African countries with stable power supply.

1. Ghana
Ghana, who got electricity supply from Nigeria, is one of the African countries with a stable power supply. Her electricity mix is ruled by hydropower, thermal energy and gas. This country is endowed with natural gas reserves which aids a proper power supply. Currently, this country has a high national electricity access of 85%.

2. Egypt

Egypt has 100% electricity access rate for both the rural and urban areas. The country has plans to supply electricity to other countries.

3. Kenya

According to energycapitalpower, Kenya has the highest access rate in East Africa. It imports power from Uganda and Ethiopia. Over 80% of Kenya’s electricity is generated from renewable energy sources with. Kenya has 62.7% electricity access for rural areas and 94% for urban areas. Hivi karibuni umeme Kenya ulikatika kwa siku moja, wakuu wawili wa shirika la umeme walifikishwa mahakamani kwa kuisababishia nchi hasara. Tanzania umeme unakatwa kila siku, hakuna anayefikishwa hata kwenye baraza la kata. Leo nipo Mwanza, jana nimefika saa 2 usiku kulikuwa hakuna umeme mpaka naenda kulala. Sijui ulirudishwa saa ngapi, lakini saa 2 asubuhi leo ukakatwa tena, mpaka muda huu haupo. Sijui kama ni mji mzima au eneo hili nililopo pekee.

4. South Africa
This is the only African country that allows nuclear energy for power. South Africa has 80% power supply and is ranked one of the best African countries with stable power supply.

5. Gabon

Gabon has a stable power supply with 91.6% electricity access rate. According to energypedia.info, about 91% of Gabon’s population has access to electricity. The country’s main source of energy is through fossil fuels and hydropower.

6. Tunisia
Tunisia is one of the African countries that has 100% electricity access to both the urban and rural areas. This country generates its energy from natural gas and is also investing in renewable energy

7. Algeria

Algeria has a 99.8% electricity access rate with 99.6% in the rural areas and 99.9% in the urban areas.

8. Morocco

According to moroccoworldnews, electricity penetration in Morocco remains the highest amongst the list of countries with 100% electricity penetration. Morocco represents a high potential renewable energy market, particularly regarding solar.

9. Senegal

Senegal has 70.4% electricity access generating its electricity from solar, wind and natural gas. The urban area has 95.2% access to electricity while the rural area has 47.4% access.

10. Botswana
This country generates its power from coal, wood and petroleum.

Tanzania tumepewa kila kitu, tulichokikosa ni uongozi wenye maono. Ukikosa uongozi wenye maono, regardless una kitu gani, ukweli ni kwamba unakuwa umekosa kila kitu.

Ndiyo maana, licha ya Tanzania kujaliwa mali asilia nyingi sana, lakini huwezi kuiona Tanzania ikiiongoza kwenye jambo lolote lililo zuri.

1. Hutaiona kwenye orodha ya nchi zenye elimu bora.

2. Hutaiona kwenye orodha ya nchi zenye huduma bora ya afya

3) Hutaiona kwenye orodha ya nchi zenye mipangilio mizuri ya miji na makazi

4) Hutaiona kwenye orodha ya nchi zenye huduma bora ya maji

5) Hutaiona katika orodha ya nchi zenye barabara bora

6) Hutaiona kwenye orodha ya nchi zenye bandari bora Africa.

7) Hutaiona kwenye orodha ya nchi zenye maendeleo makubwa ya tekinolojia Africa.

8) Hutaiona kwenye nchi zenye mifumo bora ya demokrasia Africa.
Here are the top 10 African countries leading in the Democracy Index:

1. Mauritius 8.14
2. Botswana 7.81
3. Cape Verde 7.67
4. Namibia 7.20
5. Ghana 6.95
6. Senegal 6.88
7. South Africa 6.83
8. Tunisia 6.67
9. Kenya 6.55
10. Madagascar 5.70

9) Hutaiona kwenye orodha ya nchi zenye mifumo bora ya utawala wa sheria

10) Hutaiona kwenye orodha ya nchi zenye maendeleo makubwa Africa:

Top 10 Most Developed Countries in Africa in 2023
1) Mauritius – 0.802 (Very High)
2) Seychelles – 0.785 (High)
3) Algeria – 0.745 (High)
4) Egypt – 0.731 (High)
5) Tunisia – 0.731 (High)
6) Libya – 0.718 (High)
7) South Africa – 0.713 (High)
8) Gabon – 0.706 (High)
9) Botswana – 0.693 (High)
10) Morocco – .683 (Medium)

NB: Tanzania bila kufanya mabadiliko makubwa kwenye mifumo ya utawala wa nchi, hata ipite miaka mingapi, sisi tutakuwa ni watu wa kuongelea na kustaajabia maendeleo ya mataifa mengine.

Tukitaka kuondoka mahali tulipo ni lazima twende kwenye root cause, ambayo ni mifumo mibaya ya uongozi na namna viongozi wanavyopatikana. Viongozi wamewafunga watanzania wote, wao wapo mbele wakiwakokota Watanzania wote, kuwapeleka mahali ambako hata wao wenyewe hawajui. Ndiyo maana Kikwete alipoulizwa kwa nini nchi hii ni maskini, alisema hata yeye hajui.
 
Tanzania ndiyo nchi pekee ambayo utakutana na mgawo mara sjui umeme umeangalia kushoto.

Longolongo nyingi sana.

Kwa kauli ya rais kusema baada ya miezi 6 ndiyo umeme utakaa sawa.

Hiyo ina maanisha nchi itakuwa kwenye mgawo +gizani kwa kipindi hicho cha miezi 6.

Na hata hiyo miezi 6 ikifika watakujana songi lingine

Ova
 
Kifupi tu nchi hii ina uduwanzi mwingi saana.
Lakini mkuu hapo kwenye hiyo listi vigezo gani vimetumika, kuna nchi zina access ya umeme 100% kama Egypt, wengine wana 91% huko, kwanini ghana imeweka nambari uno, nae ana 85%?
 
Hizi takwimu sio za kuamini toka mwaka jana South Africa wana mgao Tanzania ikasome. Labda ni takwimu za kua na miundombinu bora ya umeme ila sio kua na umeme wa uhakika.
 
Ndio sababu Shujaa Magufuli amejenga Bwawa la Nyerere
Huyu bwana atakumbukwa vizazi na vizazi vijavyo.

Walamba asali walijaribu kutaka kuchafua jina lake, wakapewa wizara miaka 2 imewashinda, hawajaacha legacy yoyote, wameondolewa kwa aibu ya mwaka.

Miaka 2 wako pale ni media coverage na publicity tu, hakuna kitu chochote wamefanya.
 
Hizi takwimu sio za kuamini toka mwaka jana South Africa wana mgao Tanzania ikasome. Labda ni takwimu za kua na miundombinu bora ya umeme ila sio kua na umeme wa uhakika.
South Afrika inazalisha umeme megawati 60,000+, sawa na nusu ya umeme wote unaozalishwa Afrika nzima huku Tanzania ikizalisha megawati 1,600.

South kinachosababisha mgao ni mahitaji na matumizi makubwa ya viwanda. Wao wana manufacturing plants ambazo ni heavy industries.
 
Kati ya vigezo vya kupima maendeleo ya nchi ni pamoja na kiwango cha nishati ambacho kwa wastani, kila mwananchi hutumia...
Mkuu 'Bams', unajua wazi siwezi kamwe kuwatetea TANESCO kwa jambo lolote wanalofanya kuhusu umeme wetu; lakini kuamini ujinga huo ulioonyeshwa katika kijarida hicho ni upumbavu mkubwa kabisa; kuwa Kenya inafanya vizuri kwenye mambo ya umeme?

Jameni, watu tunasoma ili tuwze kutumia akili zetu vizuri kutambua uhalisia wa mambo

Hali ya umeme Kenya ni mbovu zaidi, siyo katika vyanzo vyao pekee, lakini hata katika mfumo wa biashara yao katika sekta hiyo.

Kenya wanapenda sana kujiuza kwa uongo mwingi kwa mambo ambayo hawana, na watu hutokea kuamini uongo huo; na naona hata wewe mkuu 'Bams' unajiweka katika kundi la watu wanaoamini uongo.
 
Huyu bwana atakumbukwa vizazi na vizazi vijavyo.

Walamba asali walijaribu kutaka kuchafua jina lake, wakapewa wizara miaka 2 imewashinda, hawajaacha legacy yoyote, wameondolewa kwa aibu ya mwaka.

Miaka 2 wako pale ni media coverage na publicity tu, hakuna kitu chochote wamefanya.
Wameondolewa pale kwa kazi iliyowashinda, ikiwa ni mkakati wa kulinda hadhi yao isichafuke zaidi. Hiyo ndiyo CCM ya "Hawa ni Wenzetu."
Kulindana hata wakati wenzetu hao wakiharibu.
 
Hivi kwa nini Botswana inawekwa kwenye orodha ya nchi ambazo raia hawana furaha kila mwaka?

Wamewafanya nini "mabeberu"?
 
Kama kungefanyika study kuzipanga nchi zinazoongozwa kwa longolongo na uwongo, bila shaka Tanzania ingeibuka kuwa ya kwanza.
Na Kenya wasingekuwa mbali sana na hiyo namba itakayokuwa imeshikiliwa na Tanzania; pamoja na kwamba mbinu zinazotumiwa katika nchi zote mbili ni tofauti.

Hapa Tanzania viongozi wanatumia njia za kijinga jinga tu, kwa sababu hawana 'sophistication' yoyote ya kutunga "longolongo" ya kufikirisha watu wenye uwezo wa kufikiri.
 
Kwa kauli ya rais kusema baada ya miezi 6 ndiyo umeme utakaa sawa
Hiyo ina maanisha nchi itakuwa kwenye mgawo +gizani kwa kipindi hicho cha miezi 6....
Na hata hiyo miezi 6 ikifika watakujana songi lingine
Na mtu anayesema maneno hayo ni Rais wa nchi!

Miezi sita ya umeme wa kubahatisha, yeye akilini mwake hajiulizi miezi sita uchumi wa nchi utakuwa vipi?

Yeye anauza mipasho tu, kwa jambo la msingi sana kama hilo.
 
Mkuu 'Bams', unajua wazi siwezi kamwe kuwatetea TANESCO kwa jambo lolote wanalofanya kuhusu umeme wetu; lakini kuamini ujinga huo ulioonyeshwa katika kijarida hicho ni upumbavu mkubwa kabisa; kuwa Kenya inafanya ...
Wewe umeweka hadithi. Mimi nimezingatia taarifa za utafiti wa kisekta, tena toka taasisi 3 tofauti.


 
NB: Tanzania bila kufanya mabadiliko makubwa kwenye mifumo ya utawala wa nchi, hata ipite miaka mingapi, sisi tutakuwa ni watu wa kuongelea na kustaajabia maendeleo ya mataifa mengine.
Ili kuunga mkono hoja yako hii sahihi kabisa, ngoja nikupe mifano halisi:

Haiti (wanakopelekewa polisi toka Kenya, kulinda usalama wao) imekuwa nchi huru zaidi ya miaka mia mbili sasa hivi.

China, ambako wana umri wa miaka 74 tokea mageuzi yao, sasa hivi ni super power, ndani ya miaka tu hiyo 74.
Na mifano ya aina hiyo ipo mingi sana.

Kwa hali tunayokwenda nayo sisi (Tanzania) sasa hivi, hatuna tofauti yoyote na Haiti. Kama utawala wa aina hii tulio nao utaendelea hivi hivi, miaka 60 mingine ijayo hatutakuwa mbali sana na tulipo sasa.
 
Wewe umeweka hadithi. Mimi nimezingatia taarifa za utafiti wa kisekta, tena toka taasisi 3 tofauti.
Mkuu, huo unauita utafiti, kweli?

Mimi nazungumzia ninayoyajua kwa kufuatilia hali halisi ya nchi hiyo, na wala siyo hadithi.

Sihitaji kuwekewa hicho unachokiita wewe "utafiti" ili niamini ninachokijua.

Huko vijijini nyumba ikiwekewa swichi ya umeme tu, kwa msaada ya pesa toka Benki ya dunia, na nyumba hiyo ikawa hata siku moja haijawasha taa, huo unaouita "utafiti" unahesabu nchi kuwa na "umeme wa uhakika". Kweli?

Mkuu, 'Bams', ni hivi, sote tunakubaliana juu ya uduni wa uongozi wa nchi yetu, lakini hiyo haina maana tusifie hata kusikokuwa na sifa ya kusifia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom