Kigarama
JF-Expert Member
- Apr 23, 2007
- 2,492
- 1,230
Mod naomba uvumilie maana najua kuna vichwa maji wataijadili hii mada kwa mlengo wa ukabila. Lengo langu kujadili fumbo la haya makabila matatu kuonekana ni hatari kuongoza nchi hii,ni kuondoa dhana za kijinga tulizojipandikizia vichwani mwetu.
Watu wengi wanadai kwamba Mwalimu alishawahi kusema haya makabila hayafai kupewa nafasi ya kuwa Rais wa Tanzania. Lakini wengi wao ukiwauliza kuwa Mwalimu aliyasema maneno hayo akiwa wapi wanatangatanga nyikani kutafuta majibu.
Lakini kuna nini cha ajabu kwa makabila haya hadi wenzao wa makabila mengine waaminishwe kwamba ni hatari kuongoza nchi yetu. Ni nini kilitokea hadi haya makabila yawe hatari?
Mbona makabila makubwa ni wasukuma na wanyamwezi lakini hawaogopwi kama makabila haya yanavyoogopwa?