Wanyakyusa, Wachaga na wahaya kuna nini?

Ni uoga tu kwa sababu haya makabila yanamsimamo yangependa kusimamia haki bila kuogopa, hawadanganyiki hawa watu!
Si rahisi kuwanunua..
 
Nyerere alichokiongea ni kweli,hawa jamaa zetu wana ukabila sana alafu umewasahau na wahaya,kama ndo wahaya wanaonekana wamesoma kuliko wote kumbe ni sababu ya expose iliyopo sababu ya kubebana,akiwa waziri utakuta hata mfagizi ni kabila lao. Naunga mkono asilimia zote.wanyakyusa,wachaga na wahaya mliopo humu jf mtusamehe lakini ndivyo mlivyo,ukweli utabaki palepale. Badilikeni.
 
Pole sana usiwe kama JUHA
 
Wala sio siri hawa jamaa ni wakabila sana. Ni kweli ki elimu wako juu kutokana na kuwa wa missionary wa kwanza waliingilia kwao kwahivyo elimu ilikuwa ni kipaumbele chao sasa hili la ubinafsi sijui linatoka wapi sijui tupate wachunguzi watuchunguzie kwenye NDIZI kuna nini maana haya ni Makabila yanayofanya kilimo cha NDIZI sana...................
 
Kuna NDIZI na KAHAWA........na ELIMU(UAMKO)....vitu amabavyo sisi WAKWERE hatuna

IMG_0139-coffee-tree-banana-tree.jpg

Tehe teheeeeeeeee tih...........
 
Ukweli ni kuwa haya makabila yanabebana sana sana.

Hapa Sikonge, alikuwepo Abeid Katikaza kama MD wa NBC kama sikosei. Hakufanya lolote la maana huku Sikonge na kwa Wanyamwezi kwa ujumla. Baada ya yeye kuuguwa na kuachishwa kazi, ndipo akaingia Nsekela.

Amon Nsekela, aliwabeba Wanyakyusa si kawaida. Kazi zote za ujenzi akawa anapewa baba yake Dr. Mponjoli. NBC ikawa ikihema Kinyakyusa na Kinyakyusa ikawa kama lugha ya Taifa ndani ya NBC. Yule Boss wa Kipare pale Muhimbili na yeye alijaza Wapare kibao pale na siku aliondoka, Wapare walianza kunyanyaswa sana pale. Wachaga nafikiri tatizo lao si kubebana sana kama Wahaya ila wao wakifika sehemu, wanakomba pesa kama hawana akili nzuri. Ona Mramba na watu kama yeye.

Wahaya wengi story ni kama hizo hapo juu. Wakishajazana ofinisi, ndipo zinapoanza "usinigambire Shut up kuru-public lwa watu" yaani hapo itabidi tu ujifunze Kihaya ili uweze kufanya nao kazi.

Wanyamwezi/Wasukuma ni kabila ambalo lilikuwa limelala ila wako wengi sana. Mnyamwezi akishika kazi sehemu, basi Wanyamwezi wengine anawapishia mbali. Anaona hadi kinyaa kukaa nao kuongelea mambo ya kwao au kilugha. Atashirikiana na makabila mengine huku akiwakimbia wa kwake kama ukoma. Muone mtu kama Chenge na usomi wake. Jamaa alikuwa kwenye position ya kuwa hata Rais wa Tanzania ila ndiyo hivyo tena, akaanza KUFISADI na akina Lowassa na ndiyo mwisho wake.

Hili kabila Nyerere alilitakia kila la kheri katika usingizi wake. Usingizi wa hili kabila imekuwa heri ya CCM kwa miaka mingi sana. Tangu waanze kuamka, mabadiliko mengi sana Tanzania yanaanza kuonekana. Kwa sasa ni Mwanza imeamka ikifuatiwa na Shinyanga na nina imani siku Tabora nayo ikiamka, basi patakuwa hapatoshi.

Haya Makabila mengine kama Wachaga na Wanyakyusa, idadi yao si kubwa na hivyo hata kama wamesoma (zamani) kwa sasa hiyo haionekani sana. Sanasana wako mbele kipesa. Wengi wao sasa hivi wanajenga pwani au mbali na mikoa yao. Wanyamwezi/Wasukuma ndiyo kwanza wanaanza kurudi nyumbani maana sasa hivi wamechoka kuishi mbali na kwao wakishazeeka. Mtu kama Jaji Mfwalila ni mmoja ya mifano kuwa alipozeeka, karudi hapa Sikonge.

Kuamka kwa Kabila hili, inaweza kuwa ni habari njema na habari nzuri. Kutokana na ukubwa wake kihistoria, utakuta kuwa siku zote mikoa kama Mara na Bukoba huwa inaingia kwenye kundi hili na pia mkoa wa Rukwa huwa unaingia Tabora na hapo kulifanya hili kundi kuwa kubwa zaidi. Mji wa Mwanza ni kama vile umejengwa na makabila ya hiyo mikoa ya Mara, Mwanza na Bukoba na hii imejenga ushirikiano na ujirani mwema wa makabila ya hao watu.

Wingi wa watu wa mikoa hii Mitano, siku wakiungana, nina wasiwasi itatokea kama inavyotokea nchi kama Senegal ambako kuna kundi moja kubwa sana (Mouride brotherhood -Senegal's richest and most powerful Islamic brotherhood ) ambalo liko well organised na ndiyo wamempeleka jamaa yao hadi akawa Rais.

Kwa mawazo yangu mie, kuna haja ya kuwa na kitu kiitwacho MADARAKA MIKOANI. Hii itafanya hii mikoa iwe ikishindana kwa maendeleo na siyo kama sasa hivi kuwa na Central Government. Kwa hali ilivyo sasa, ni rahisi sana siku moja akaja Mnyamwezi/Msukuma mwenye uwezo wa kuwaunganisha kama Mirambo, na akajenga kundi moja kubwa na lenye nguvu sana Tanzania na hapo kuanza kukandamiza makabila mengine ambayo kwa uchache wake, hawatakuwa na nguvu sana. Hii mikoa kwa kutumia madini yake, inaweza kuwa tajiri na kuanza kutawala wengine kwa nguvu hadi ikapelekea makabila mengine kutaka kujitenga na mwisho vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Ni jambo zuri kuliongelea na kuanza kutafuta solution mapema. Wachina wanasema "jasho jingi wakati wa amani, damu kidogo wakati wa vita". Tusiwe waoga kujadili tipic ngumu maana hali ikibadilika, tunakuwa tumejiandaa na tusiwe kama Mbuni kwa kuficha kichwa kwenye mchanga.

Please: Usiniite mie Mkabila. Maishani nimesaidiwa na watu wa makabila mengi sana na namba moja Wahaya.
 
You are vere vere true si unawaona kwenye kile chama chetu? wakwe watoto na pengine 2015 wajukuu watakuwa tayari wamefikisha miaka 18 watapata kula ndani ya chama hehehehe nawapenda sana wachagga zea vere smati.....

Karibu tule Machalari ndugu yangu, lakini tumeweka na kisusio cha KM kwa pembeni sijui unatumiagaaaa.
Na kata yako ya mbege nimeshakuwekea, karibu sana.

Lakini pia aiseeee? we serikali yetu huijui nini? tangu ensi sa Nyerere, mtaji wa CCM ni ujinga wa Watansania, Hakya nani wakiambiwa ukimhagua Mchaga fita itatokea, wakioneshwa na vita vya Idd Aminn unafikiri watamchagua. Halafu mchaga sio mwoga kwa hiyo humpeleki peleki hofyo, hifi wewe unaleta kesi sako za ajabu ajabu kama sa Rada unadhani utapona.

Hifi hujajifunsa hata kwa Pesambili, ooh sijui panga la samani, sijui kaiba kaleta nyumbani, wiiiii nani amchague sasa, sisi tutakunywa mbege na hela sake, na hiso kanga faeni tu, tena mama Aika chukua kanga tatu, moja ya kufagia mbolea, nyingine yakwenda shambani/mtemeni na ingine tukasugie pale klabuni badae tupate bohora moja leo si ndio anakuja kwene kampeni? Wale jamaa sake lasima watoe mbege leo.
Chaaaaaaa! eti kaleta lami, uwiiiiiiii hiso ni kodi setu aiseee wala asitudanganye.
 
Hao watu ni noma kwa kupendeleana na kubebana!
Hiii hoja pia nakumbuka ilitumiwa sana kumwangamiza Mwandosya, Pia inatumiwa dhidi ya Mbowe na CHADEMA. Lakini ukichunguza sana inatumiwa dhidi ya Kikwete na Uislamu wake.

Kwa maoni yangu watu wengi wenye matatizo ya ubaguzi wa aina yoyote ile wana sifa moja. Sifa yao kuu ni kuishi kwenye eneo moja lenye watu wenye sifa ya aina moja. Kama mtu amezaliwa Unguja au Pemba yeye ataamini kwamba wasio waislamu ni watu wa kujihadhari nao na ni lazima wasilimishwe. kwa sababu yeye maisha yake yote ameishi katikati ya eneo lenye waislamu kwa asilimia 99!

Na ukikutana na Mlokole kutoka Tukuyu au Kiraracha basi ujue yeye anajua watu wasio Wakristo ni wana wa shetani au wapinga Kristo. Hata kwa makabila ni hivyohivyo.

Kwa wale waliozaliwa Mijini hali yao ya Ukabila na Udini ni ndogo sana ukilinganisha na wale waliozaliwa vijijini na kwenye maeneo yeye aina moja ya kabila au dini. Nafikiri suluhisho ya tatizo hili ni kuendeleza maeneo ya vijijini ili watu wa maeneo mengine waweze kupata hamu ya kwenda kuishi huko na kuleta mchagamano utakaondoa dhana ya ukabila ambayo kwa sasa ingawa haina maana lakini imeanza kuchipuka tena.
 
[/B][/COLOR]Makubwa katika mambo gani???? Ukubwa wa mtu ni kichwa mkuu sio idadi yao!!! Ukweli ni kwamba makabila haya ndio yenye wasomi wengi zaidi...that's it, nothing more!!!!

QUOTE]

Uoongo! Ni imani tu kwamba wasomi wengi wanatoka makabila haya! Leta takwimu!! Hii ni hofu ya kihistoria maana hawa ndio walianza na shule za misheni, lakni since then ni kama makabila mengine kama hawajapitwa
 
wanawekana maofisini.. nenda katika chuo cha kariuki pale! hesabu idadi ya wahaya
 
Ukweli ni kuwa haya makabila yanabebana sana sana.

Hapa Sikonge, alikuwepo Abeid Katikaza kama MD wa NBC kama sikosei. Hakufanya lolote la maana huku Sikonge na kwa Wanyamwezi kwa ujumla. Baada ya yeye kuuguwa na kuachishwa kazi, ndipo akaingia Nsekela.

Amon Nsekela, aliwabeba Wanyakyusa si kawaida. Kazi zote za ujenzi akawa anapewa baba yake Dr. Mponjoli. NBC ikawa ikihema Kinyakyusa na Kinyakyusa ikawa kama lugha ya Taifa ndani ya NBC. Yule Boss wa Kipare pale Muhimbili na yeye alijaza Wapare kibao pale na siku aliondoka, Wapare walianza kunyanyaswa sana pale. Wachaga nafikiri tatizo lao si kubebana sana kama Wahaya ila wao wakifika sehemu, wanakomba pesa kama hawana akili nzuri. Ona Mramba na watu kama yeye.

Wahaya wengi story ni kama hizo hapo juu. Wakishajazana ofinisi, ndipo zinapoanza "usinigambire Shut up kuru-public lwa watu" yaani hapo itabidi tu ujifunze Kihaya ili uweze kufanya nao kazi.

Wanyamwezi/Wasukuma ni kabila ambalo lilikuwa limelala ila wako wengi sana. Mnyamwezi akishika kazi sehemu, basi Wanyamwezi wengine anawapishia mbali. Anaona hadi kinyaa kukaa nao kuongelea mambo ya kwao au kilugha. Atashirikiana na makabila mengine huku akiwakimbia wa kwake kama ukoma. Muone mtu kama Chenge na usomi wake. Jamaa alikuwa kwenye position ya kuwa hata Rais wa Tanzania ila ndiyo hivyo tena, akaanza KUFISADI na akina Lowassa na ndiyo mwisho wake.

Hili kabila Nyerere alilitakia kila la kheri katika usingizi wake. Usingizi wa hili kabila imekuwa heri ya CCM kwa miaka mingi sana. Tangu waanze kuamka, mabadiliko mengi sana Tanzania yanaanza kuonekana. Kwa sasa ni Mwanza imeamka ikifuatiwa na Shinyanga na nina imani siku Tabora nayo ikiamka, basi patakuwa hapatoshi.

Haya Makabila mengine kama Wachaga na Wanyakyusa, idadi yao si kubwa na hivyo hata kama wamesoma (zamani) kwa sasa hiyo haionekani sana. Sanasana wako mbele kipesa. Wengi wao sasa hivi wanajenga pwani au mbali na mikoa yao. Wanyamwezi/Wasukuma ndiyo kwanza wanaanza kurudi nyumbani maana sasa hivi wamechoka kuishi mbali na kwao wakishazeeka. Mtu kama Jaji Mfwalila ni mmoja ya mifano kuwa alipozeeka, karudi hapa Sikonge.

Kuamka kwa Kabila hili, inaweza kuwa ni habari njema na habari nzuri. Kutokana na ukubwa wake kihistoria, utakuta kuwa siku zote mikoa kama Mara na Bukoba huwa inaingia kwenye kundi hili na pia mkoa wa Rukwa huwa unaingia Tabora na hapo kulifanya hili kundi kuwa kubwa zaidi. Mji wa Mwanza ni kama vile umejengwa na makabila ya hiyo mikoa ya Mara, Mwanza na Bukoba na hii imejenga ushirikiano na ujirani mwema wa makabila ya hao watu.

Wingi wa watu wa mikoa hii Mitano, siku wakiungana, nina wasiwasi itatokea kama inavyotokea nchi kama Senegal ambako kuna kundi moja kubwa sana (Mouride brotherhood -Senegal's richest and most powerful Islamic brotherhood ) ambalo liko well organised na ndiyo wamempeleka jamaa yao hadi akawa Rais.

Kwa mawazo yangu mie, kuna haja ya kuwa na kitu kiitwacho MADARAKA MIKOANI. Hii itafanya hii mikoa iwe ikishindana kwa maendeleo na siyo kama sasa hivi kuwa na Central Government. Kwa hali ilivyo sasa, ni rahisi sana siku moja akaja Mnyamwezi/Msukuma mwenye uwezo wa kuwaunganisha kama Mirambo, na akajenga kundi moja kubwa na lenye nguvu sana Tanzania na hapo kuanza kukandamiza makabila mengine ambayo kwa uchache wake, hawatakuwa na nguvu sana. Hii mikoa kwa kutumia madini yake, inaweza kuwa tajiri na kuanza kutawala wengine kwa nguvu hadi ikapelekea makabila mengine kutaka kujitenga na mwisho vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Ni jambo zuri kuliongelea na kuanza kutafuta solution mapema. Wachina wanasema "jasho jingi wakati wa amani, damu kidogo wakati wa vita". Tusiwe waoga kujadili tipic ngumu maana hali ikibadilika, tunakuwa tumejiandaa na tusiwe kama Mbuni kwa kuficha kichwa kwenye mchanga.

Please: Usiniite mie Mkabila. Maishani nimesaidiwa na watu wa makabila mengi sana na namba moja Wahaya.

MKUU Sikonge,

Alikuwepo IGP Pundugu, mara baada ya kuteuliwa aliwapandisha askari Wanyamwezi wenzake kwakasi ya kutisha.

Kwa hiyo upendeleo ni tabia ya mtu, na kwa maelezo yako hapo juu ni wazi kwamba ukipata nafasi nawe ni wa tabia hiyo.
 
Watu wa makabila hayo walibahatika tu kupata elimu enzi ya ukoloni kabla ya watu wa makabila mengine. Ingekuwa ni Waha, Wanyaturu, Wakwere, na wengine walio elimika kuliko makabila mengine enzi hiyo, wangekuwa wanasemwa hivyo pia.

Ni wivu mtupu kuyalaumu makabila hayo.

Hata mimi niliwahi kusikia mara nyingi enzi ya Nyerere na baada ya Mwalimu kuondoka madarakani kwamba aliwazuia watu wa makabila hayo kupata nafasi ya uraisi na sehemu zingine za uongozi nchini. Hakuna uthibitisho Mwalimu alifanya hivyo.

Hakuwaamini kuongoza nchi lakini aliwaamini na maisha yake? Mnamkumbuka yule mlinzi wake mrefu, Mwangota kutoka Kyela, kwa miaka mingi? Tusimsahau daktari wake, Msokile mwingine - samahani Myakyusa - Mwakyusa.

Hili halina uhusiano na usalama wa Mwalimu au wa taifa lakini kati ya wakwe zake ni Mnyakyusa mwingine, Mwamakula. Sidhani hakumwamini kwa sababu alikuwa ni Mnyakyusa. Halafu kulikuwa na Wachaga, Wayakyusa, na Wahaya wengi katika usalama wa taifa enzi ya Mwalimu. Jeshini pia, kulikuwa na maofisa wengi kutoka makabila hayo. Alikuwa na wasi wasi kwamba watampindua? Sikuwahi kusikia.

Na yule aliyegusia hapo juu kuhusu chama kikubwa cha upinzani, si kweli kwamba ni cha Kichaga au ni cha Wachaga. Kimeshinda uchaguzi sehemu zote za Tanzania, pamoja na washindi wake walioibiwa kura katika uchaguzi mkuu uliopita. Pia kuna viongozi katika chama hicho kutoka watu wa makabila mbali mbali. Siyo Wachaga tu.

Ikiwa hatuaminiani kwa sababu ya makabila yetu, nchi yetu itapotea. Mhaya ana haki kuwa raisi wa Tanzania kama Mnyaturu; Mchaga ana haki kuwa raisi wa Jamhuri hii kama Mmakonde; Mnyakyusa ana haki kuwa raisi wa nchi yetu kama Mdigo, Mmatengo, Mzaramo, Mkinga, Mkurya, Mzanaki, Mluguru na kadhalika.

Nyaturu,

Kwa nyongeza tu, kabla ya Prof Mwakyusa alikuwepo Dr Mwakosya ambaye ndiye daktari wake wa kwanza. Kwa maana hiyo madaktari wake hadi anakufa ni Wanyakyusa.

Haya mawazo ya ukabila au kuyatenga makabila hayo na uongozi wa nchi hii ni kuwaonea. Lazima tukubaliana na ukweli kwamba walibahatika kupata elimu mapema, hivyo ni miongoni mwa Watanganyika wachache walioelimika wakati tunapata uhuru na Nyerere hakuwa na jinsi aliwatumia hao hao.

Lakini hata leo hii hawa jamaa wanawekeza sana kwenye elimu ya watoto wao. Kwa mfano Wahaya waliunda taasisi iliyoitwa BALIMI, hii ili sponsar watoto wao na hadi leo wanasomeshana hadi chuo kikuu kwa kuchangiana wakati wengine tumekazana na michango ya harusi na tunaona ufahari kwa hilo.
 
Nyerere hakuwahi kusema hayo, mbona hamtupi ilikua hotuba gani.
ama aliyasema hayo maneno akiwa na Mkewe Maria, majungu matupu.
 
[/B][/COLOR]Makubwa katika mambo gani???? Ukubwa wa mtu ni kichwa mkuu sio idadi yao!!! Ukweli ni kwamba makabila haya ndio yenye wasomi wengi zaidi...that's it, nothing more!!!!

QUOTE]

Uoongo! Ni imani tu kwamba wasomi wengi wanatoka makabila haya! Leta takwimu!! Hii ni hofu ya kihistoria maana hawa ndio walianza na shule za misheni, lakni since then ni kama makabila mengine kama hawajapitwa

Nenda chuo kikuu chochote Tanzania ratio itakuwa Chagga>Haya>Nyakusya>upupu wa pwani na wengine

Wahaya, wachaga na wanyakusya wakisusa kwenda ofisini nchi hii inacollapse
 
You are vere vere true si unawaona kwenye kile chama chetu? wakwe watoto na pengine 2015 wajukuu watakuwa tayari wamefikisha miaka 18 watapata kula ndani ya chama hehehehe nawapenda sana wachagga zea vere smati.....

Huu sasa ni ukabila na upo kila mahali hauchagui baadhi ya makabila tu ila kwa vile weng wamezaliwa na kuishi mijini matatizo haya yanaananza kupungua............
 
waTZ ukisema hiki ki2 alisema nyerere unawagusa kiukweli... so kuna wapuuzi/mpuuzi aliamua kutumia hiyo hali kuupotosha umma!
 
Back
Top Bottom