Wanyakyusa, Wachaga na wahaya kuna nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanyakyusa, Wachaga na wahaya kuna nini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kigarama, Nov 12, 2010.

 1. Kigarama

  Kigarama JF-Expert Member

  #1
  Nov 12, 2010
  Joined: Apr 23, 2007
  Messages: 2,479
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mod naomba uvumilie maana najua kuna vichwa maji wataijadili hii mada kwa mlengo wa ukabila. Lengo langu kujadili fumbo la haya makabila matatu kuonekana ni hatari kuongoza nchi hii,ni kuondoa dhana za kijinga tulizojipandikizia vichwani mwetu.

  Watu wengi wanadai kwamba Mwalimu alishawahi kusema haya makabila hayafai kupewa nafasi ya kuwa Rais wa Tanzania. Lakini wengi wao ukiwauliza kuwa Mwalimu aliyasema maneno hayo akiwa wapi wanatangatanga nyikani kutafuta majibu.

  Lakini kuna nini cha ajabu kwa makabila haya hadi wenzao wa makabila mengine waaminishwe kwamba ni hatari kuongoza nchi yetu. Ni nini kilitokea hadi haya makabila yawe hatari?

  Mbona makabila makubwa ni wasukuma na wanyamwezi lakini hawaogopwi kama makabila haya yanavyoogopwa?
   
 2. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #2
  Nov 12, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,469
  Likes Received: 5,847
  Trophy Points: 280
  Kuna NDIZI na KAHAWA........na ELIMU(UAMKO)....vitu amabavyo sisi WAKWERE hatuna

  [​IMG]
   
 3. H

  Hardwood JF-Expert Member

  #3
  Nov 12, 2010
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 853
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 80


  Makubwa katika mambo gani???? Ukubwa wa mtu ni kichwa mkuu sio idadi yao!!! Ukweli ni kwamba makabila haya ndio yenye wasomi wengi zaidi...that's it, nothing more!!!!

  As for Mwl. Nyerere comments regarding these tribes not to lead the nation.... hio haina ukweli wowote... ni conspiracy fulani tu hivi ambayo imeasisiwa na wapuuzi fulani ndani ya serikali.... One amasing thing is that Vyama vingi vya upinzani vina viongozi waandamizi wengi wanaotoka katika makabila haya....so, vilaza wa CCM wanatumia upuuzi huu kwa kuwaambia wa-tz wasiwachague wapinzani!!!
   
 4. Buswelu

  Buswelu JF-Expert Member

  #4
  Nov 12, 2010
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 1,989
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Eti kwa sababu wasomi ni wengi kwenye makabila hayo...na wametangulia kimaendeleo(which is benefit for country like this)kupata mtu mwenye mtizamo mkuuu wa maendeleo toka kwako/kwake.
   
 5. manenge

  manenge JF-Expert Member

  #5
  Nov 12, 2010
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 280
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ni dhana potofu iliyojengeka miongoni mwa jamii ikichanganika na kawivu kwa mbali dhi ya makabila hayo kutokana na mwamko walio uliochangiwa na elimu
   
 6. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #6
  Nov 12, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Hao watu ni noma kwa kupendeleana na kubebana!
   
 7. Sokomoko

  Sokomoko JF-Expert Member

  #7
  Nov 12, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  You are vere vere true si unawaona kwenye kile chama chetu? wakwe watoto na pengine 2015 wajukuu watakuwa tayari wamefikisha miaka 18 watapata kula ndani ya chama hehehehe nawapenda sana wachagga zea vere smati.....
   
 8. D

  DoubleOSeven JF-Expert Member

  #8
  Nov 12, 2010
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 661
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  ... kwi kwi kwi!!! niongeze ... LONGO LONGO siyo utamaduni wao. Yapo makabila mengine mengi tu ambayo USANII na LONGOLONGO siyo JADI yao. Hapa nataja mOJA tu...WAMBULU
   
 9. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #9
  Nov 12, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mimi nasema ndo maana Tanzania haiendelei! Yaani mtu alizusha hii zana tu ili iwe mtaji wa kuendelea kutafunwa kwa mali ya nchi na wachache. Maana ndani ya Haya makabila kunawasomi wengi ambao huwezi kiwadanganya kitu ndio maaana walizusha hii hoja ili kwamba haya Makabila yasishike hatamu kuwafumbua watanzania macho!!!!!!!!!!!
   
 10. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #10
  Nov 12, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,469
  Likes Received: 5,847
  Trophy Points: 280
  Advantage tulionayo Watanzania ni kuwa unaweza kuzamia kabila lingine...unajifunza lugha na utamaduni wao halafu unaowa ndugu yao...tayari ushakuwa mwenzao...KENYA...huwezi kuzamia Ukikuyuni kama wewe ni Mjaluo
   
 11. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #11
  Nov 12, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  kwani kinachayafanya hayo makabila mengine yasiige hayo makabila 3 ni nn tuache uvivu tujitume kila mtu ni bora
   
 12. N

  Nyaturu Member

  #12
  Nov 12, 2010
  Joined: Feb 26, 2010
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watu wa makabila hayo walibahatika tu kupata elimu enzi ya ukoloni kabla ya watu wa makabila mengine. Ingekuwa ni Waha, Wanyaturu, Wakwere, na wengine walio elimika kuliko makabila mengine enzi hiyo, wangekuwa wanasemwa hivyo pia.

  Ni wivu mtupu kuyalaumu makabila hayo.

  Hata mimi niliwahi kusikia mara nyingi enzi ya Nyerere na baada ya Mwalimu kuondoka madarakani kwamba aliwazuia watu wa makabila hayo kupata nafasi ya uraisi na sehemu zingine za uongozi nchini. Hakuna uthibitisho Mwalimu alifanya hivyo.

  Hakuwaamini kuongoza nchi lakini aliwaamini na maisha yake? Mnamkumbuka yule mlinzi wake mrefu, Mwangota kutoka Kyela, kwa miaka mingi? Tusimsahau daktari wake, Msokile mwingine - samahani Myakyusa - Mwakyusa.

  Hili halina uhusiano na usalama wa Mwalimu au wa taifa lakini kati ya wakwe zake ni Mnyakyusa mwingine, Mwamakula. Sidhani hakumwamini kwa sababu alikuwa ni Mnyakyusa. Halafu kulikuwa na Wachaga, Wayakyusa, na Wahaya wengi katika usalama wa taifa enzi ya Mwalimu. Jeshini pia, kulikuwa na maofisa wengi kutoka makabila hayo. Alikuwa na wasi wasi kwamba watampindua? Sikuwahi kusikia.

  Na yule aliyegusia hapo juu kuhusu chama kikubwa cha upinzani, si kweli kwamba ni cha Kichaga au ni cha Wachaga. Kimeshinda uchaguzi sehemu zote za Tanzania, pamoja na washindi wake walioibiwa kura katika uchaguzi mkuu uliopita. Pia kuna viongozi katika chama hicho kutoka watu wa makabila mbali mbali. Siyo Wachaga tu.

  Ikiwa hatuaminiani kwa sababu ya makabila yetu, nchi yetu itapotea. Mhaya ana haki kuwa raisi wa Tanzania kama Mnyaturu; Mchaga ana haki kuwa raisi wa Jamhuri hii kama Mmakonde; Mnyakyusa ana haki kuwa raisi wa nchi yetu kama Mdigo, Mmatengo, Mzaramo, Mkinga, Mkurya, Mzanaki, Mluguru na kadhalika.
   
 13. October

  October JF-Expert Member

  #13
  Nov 12, 2010
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 2,147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kila ,mtu ana haki sawa ya kuwa RAISI hapa tanzania mradi tu asichakachue kura kama alivyofanya huyu Mkwere na timu yake.

  Tanzania hakuna chuki ya ukabila kama wanavyotaka tufikiri, ndio maana makabila tofauti yanachumbiana na kuoana bila kujali kabila la mtu. Ni watu wangapi huanza kuuliza kabila la mtu kabla hawajaanza mahusiano? Au ni nani kati yetu ambae hajawahi ku-date mtu wa kabila tofauti na lake? Nadhani hakuna!!

  Hii dhana ya ukabila katika Tanzania ni mchezo mchafu tu uliopikwa na CCM ili ku-distract attention ya watanzania kuhusu maovu yanayofanywa na CCM.

  Watanzania tuwe macho na mchezo mchafu wa CCM, Walianza kutumia ukabila kutugawa, na baadae wakaanza kutumia udini,Next time sijui watatumia nini. Lets wait and see....Nionavyo hii yote ni kutapatapa kwa CCM ili watanzania wabakie kujadili upuuzi kama huu na wao waendelee kupora mali ya nchi. Ni sawa na kuwadunga watanzania sindono (nusu kaputi) ili waendelee kuwabaka.....

  Tusikubali kuingia kwenye hii sokomoko ya CCM. Watanzania ni wamoja na wote wana haki sawa.

  Mfano. Ukiwa unaumwa unahitaji kufanyiwa upasuaji, halafu wakawepo madaktari wawili. Daktari mmoja ni daktari wa ukweli mwenye ujuzi na kazi yake na rekodi bora katika utendaji wake lakini si wa kabila lako, Wapili ni Daktari wa uongo, asiye serious na kazi yake, Msanii na mwenye rekodi ya kusahau mikasi tumboni mwa wagonjwa wake, Lakini ni wa kabila lako. Ni yupi utakayemchagua akufanyie Upasuaji?

  Kama unaweza kutoa uamuzi mzuri katika swala linalohusu maisha yako, kwanini ushindwe toa uamuzi sahihi kama huu katika swala la uongozi wa nchi yako?


  Swala si Kabila bali uwezo wa mtu katika kuikwamua nchi yetu katika umaskini.
   
 14. JOYCE PAUL

  JOYCE PAUL JF-Expert Member

  #14
  Nov 12, 2010
  Joined: Jan 8, 2010
  Messages: 1,007
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Suala la siasa naweka pembeni na me maoni yangu ni kama ifuatavyo
  swala la makabila haya sio kupendeleana aua nini sasa kama hamjui nia ya nyerere effect yake ndio hii hapa mnayoiona sasa hivi.haya makabila nafikiri mnaona wenyewe yalivyo na msimamo na nyerere hakupenda mtu anayemchalenge hivyo aliamua kuyakandamiza makabila haya kwa visingizio mbali mbali lakini ile mbegu sasa mnaiona watu hawataki mabadiliko hata ukweli wakiambiwa..unafikiri ongezeko la mafisadi unatokana na nini kama sio watu kutopenda kufikiri wakiambiwa kitu nao wanakubali..nyerere alikuwa anajua akili za watu wengine wa tanzania wakijazwa maneno wanayabeba kama yalivyo ndo maana watu wanapewa tshet.wali,alfu kumi yakula siku moja wanampa kura fisadi hiyo yotee ni matokeoo ya mbegu iliyopandwa na mwl.i love this man angekuwepo najua angebadili usemi wake ila ndo hivo ena hayupo na mbegu inaota watu hawana msimamo wanapelekwa pelekwa tu.
   
 15. 1

  1954 JF-Expert Member

  #15
  Nov 12, 2010
  Joined: Nov 14, 2006
  Messages: 4,293
  Likes Received: 2,185
  Trophy Points: 280
  Hii mada haifai kuletwa katika mjadala ingawa ina namna ya umuhimu.

  Ukweli ni kuwa hakuna mahali popote ambapo Mwalimu alitamka maneno hayo. Hii ni 'conspiracy' ambayo ililetwa kwa bahati nzuri na wala siyo bahati mbaya.

  Uongozi wa nchi ni jambo nyeti na mtu anayeongoza taifa au nchi kwa ujumla wake ni lazima awe mtu mwadilifu asiye na upendeleo na asiye mbinafsi.
  Hofu iliyopo ni kuwa watu wa makabila ya kichaga, wahaya na wanyakyusa wana ubinafsi mkubwa mno. Angalia kwa mfano hali iliyokuwepo katika shirika la Bima enzi za Mwaikambo. Wanyakyusa walikuwa kibao. Inawezekana kosa ni la mtu mmoja ambaye ni Mwaikambo lakini katika masuala haya huwezi kumtenganisha Mwaikambo na Unyakyusa.

  Angalia hali ilivyo sasa huko HAZINA, TRA na vyombo vya fedha. Wachagaa wamejaa. Inawezekana ni kweli hao ndio waliosoma. lakin i ukweli ni kuwa huwezi kutenganisha uchaga na harufu ya upendeleo.

  Wahaya wanajulikana kwa ubinafsi walio nao na tabia ya kuongea ki-lugha kila 'mahali'. Hii ndio inayoleta hisia mbaya dhidi yalo.

  Hivi sasa Wahaya na Wanyakyusa na hata Wachagaa baadhi yao kwenye CV zao au majina yao kwa ujumla wameondoa majina ya ukoo ili wasijulikane makabila yao. Kama mtu fulani anaitwa Fred na ukoo wake ni Mushi au Mutayoba kamwe, baadhi yalo, hawaweki majina ya koo zao bali watachukua majina ya baba zao kwa mfano ataiwa Fred Max kama baba yake ni Max.

  Kwa hiyo tunachokiona hivi sasa ni hofu ya jamii kuwa Wachagga, Wanyakyusa na hata Wahaya wana ubinafsi na upendeleo wa kikabila ndio maana hofu hiyo ipo.

  Lakini swali la kujiuliza ni kuwa hali hiyo ya ubinafsi na upendeleo kwa makabila haya kweli bado ipo? Huu ndio mjadala unaopaswa kujadiliwa, kwani inawezekana makabila haya yanaonewa tu kwa sasa.
   
 16. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #16
  Nov 12, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  hawakutumikishwa na wakoloni wa kiarabu kwa kuwa ni makabila ya watu makini sana
  na wanaojitambua, huku wakijitawala kifikra, vile vile haya makabira hayana dhana
  ya ndiyo mzee, hata kwenye ujinga so mwalimu alipata upinzzani sana kutoka
  kwa watu wa haya makabila, ukizingatia pia mfano Wanyakyusa walipata muamko
  wa elimu mapema sana ukilinganisha na wayao, wamakua, wazaramo, wakwere,
  wangindo, n.k

  nawasilisha
   
 17. S

  Shwari Senior Member

  #17
  Nov 12, 2010
  Joined: Jan 12, 2008
  Messages: 189
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Msimuongopee Mwalimu. Leta ushahidi kuonyesha aliwabagua Wachaga, Wanyakyusa na Wahaya. Ni yeye aliyewapa wengi wao kazi za juu sana serikalini na katika mashirika mbali mbali.

  Mfano mmoja ni Amon Nsekela. Kulikuwa na malalamiko mwanzoni wa miaka ya sabini na baada ya hapo miongoni mwa watu mbali mbali kwamba Nyerere alikuwa anampendelea Nsekela. Nakumbuka alikuwa na vyeo vya juu sana sehemu mbali pamoja na National Insurance Corporation, National Bank of Commerce, University of Dar es Salaam, na mahali pengine. Aliteuliwa na Nyerere. Kuna wakati watu mbali mbali walikuwa wanasema ana vyeo kumi na mbili - either as director, chairman au mmoja wa members of board of directors. Walikuwa wanauliza, kwa nini mtu mmoja tu apewe vyeo vyote hivyo? Wangemuuliza Nyerere anayelaumiwa kuwa alikuwa anawabagua Wanyakyusa, Wachaga na Wahaya. Ndiye aliyemteua Nsekela.

  Nsekela alikuwa na maadui wengi kwa sababu hiyo. Kuna wana usalama wa taifa miaka ile waliomuongopea kwa nia ya kumuangamiza na walipeleka ripoti mbali mbali kwa Mwalimu lakini Mwalimu alizikataa ripoti hizo kwa sababu alijua wanaongopa. Mwalimu alimkingia kifua Nsekela.

  Kuna watu, kwa sababu ya wivu na chuki yao ya Wachaga, waliokuwa wanasema Edwin Mtei haifai kuwa mkuu wa benki kwa sababu hakusomea uchumi. Aliteuliwa na Nyerere. Hata baada ya kutofautiana, - policy not personal differences - Mwalimu aliona Mtei anafaa kuwa mwakilishi wa bara letu World Bank.

  Wakumbukeni Wachaga, Wahaya na Wanyakyusa wengi sana waliopewa kazi za juu na vyeo vikubwa na Nyerere anayelaumiwa alikuwa anayachukia makabila hayo. Msipotoshe ukweli. Ni sawa na chuki na uongo kutoka kwa watu mbali mbali wanaosema Chadema ni chama cha Wachaga ingawa kuna ushahidi wa kila aina kuonyesha kwamba ni chama ambacho kina viongozi na wafuasi wengi sana kutoka makabila mbali mbali sehemu zote za Tanzania.
   
 18. mgt software

  mgt software JF-Expert Member

  #18
  Nov 12, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 10,725
  Likes Received: 1,631
  Trophy Points: 280
  Topiki hii imenigusa sana na naandaa kitabu kuhus makabila haya yalivyoangushwa kuchumi na kiutamaduni kwa makusudi ili yatawalike kiurahisi na kulazimisha kukumbatia ujinga, sio kwamba makabila haya wabaguzi hila husuda, chuki binafsi , kwa mfano watu wengi wamekuja mjini kutafuat liziki na wakafikia kwa Zaramo na wandengereko , lakini walipewa vyumba wakaaqnza kupanga na kujiendeleza kimasomo lakini mwenyeji wao aliendelea kuamini chuma ulete baada ya hawa watu kuweka bidii na kujikomboa kuwa na nyumba nzuri na kutafuta maali pazuri , mra utasikia wahay noma wachawi, nyakyusa usiseme , chaga wezi wanajifanya wanbrash viatu kumbe usiku wezi kumbe ni juhudi binasfi wenyeji ujipamba kusubir wapewe (Uvivu) ndio maana wapiganaji wanawabagua
   
 19. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #19
  Nov 12, 2010
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Sokomoko [​IMG] [​IMG]
  JF Senior Expert Member [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] [​IMG] Join
  DateSat Mar 2008LocationKijijiniPosts875Thanks25
  Thanked 70 Times in 51 Posts Rep Power24


  Avatar yako tu ya kutangaza utalii.:evil:
   
 20. k

  kajembe JF-Expert Member

  #20
  Nov 12, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 756
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  on his annual radio broadcast to the nation on the seventh of independence anniversary on December 9, 1968, Mwalimu Nyerere said,
  I have begun to hear whisper about tribalism. just after indepence we got complains that people were being appointed to the government positions on the basis of tribalism, and we immediatly appointed the commission to look into the allegations. The commission proved without any doubt tha there was no tribalism in the allocation of jobs in government.

  But just recently, I have began to hear this complains again. I did not treat it lightly .We called some of this people who were saying there is tribalism,and told them to give evidence either to me or to the Ombudsman.we promised to investigate immediately. But they have not given us one shred of evidence.

  Tanzanians who had the most opportunity for higher education during colonial rule were mostly Wahaya,Wachga an Wanyakusa. And because most of the education was provided by missionaries,most of these people are also christians.

  It is the job of the government to help ,even favor,the more backward parts of country ,especially regarding education.
  We are doing this and will continue to do so.But if a Mchaga,a Mhaya or a Mnyakyusa young man were denied a job because of his tribe when he is capable and there is no other Tanzanian with necessary qualifications then we would be practicing a very stupid and very evil kind of tribalism which led to the establishment of Biafra
  .
   
Loading...