Tukiachana na wachaga, Kuna kabila lingine lina utamaduni wa kurudi na kujumuika kwenye vijiji vya mizizi yao nje ya misiba?

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,033
Ni utamaduni unaonishangaza sana, kila ikifika december wiki 2 za mwisho Wachaga wa nje ya mikoa na nje ya nchi hukusanyika pamoja kwenye sehemu za asili zao huko Kilimanjaro.

Kwa miaka kadhaa nishazoea kuona status za wachaga watatu wanaoishi nje ya nchi wanapost status wamerudi, Yupo anaeishi China jiji la Guangzou, Marekani jiji la San Fransisco na mwengine Australia jiji la Sydney.

Kurudi kwa pamoja hukutanisha kila mwaka ndugu, majirani mpaka marafiki wa utotoni, kwa wale watoto waliozaliwa huku mijini ama nje ya nchi nao wanapelekwa kuijua mizizi yao, nadhani hata kama ulikopa duka la mangi mwaka jana basi hii December utadakwa tu.

Tukija huku makabila mengine ni nadra sana, achilia mbali kabila yani hata ndugu kurudi kwa pamoja kwenye mizizi yao ni suala zito, Labda itokee kuna msiba wa babu huko kijijini watazika na kutawanyika.

Binafsi upande wa baba ni mtu wa kanda ya ziwa, Yeye alikulia kijijini huwa anarudi kila mwaka lakini mimi nilienda mara 2 tu nikiwa darasa la sita na la saba shughuli ikaishia hapo !! kwakweli ni kipindi kirefu sana kimepita, connection za kijijini zimepotea kabisa hata watoto wakiulizia kijijini kwao nawaambia ni mtaa wa mjini niliozaliwa, naowahesabia ni ndugu ni wale tunaokutana mjini ila kule kwenye mizizi nishapoteza connection.

Nipo mikoa ya Iringa ya Mbeya kuna makabila kadhaa mambo ni hayo hayo tu, tukianza na Wanyakyusa wa Mbeya waliozaliwa nje ya sehemu za mizizi yao (Tukuyu ama Kyela) hawajazoeshwa kurudi kwenye mizizi yao hata undugu ni ule wa kujuana ndugu wa mjini. Ikitokea wamerudi huko kwao labda kuwe na mazishi, hali inakuwa mbaya zaidi kwa watoto wa hawa wanyakyusa waliozaliwa mijini wanaweza hata wasipajue Tukuyu.

Wengine nao ni wakinga wa huko Njombe wapo sana hio Iringa na Mbeya, watoto wanaishia kupajua mjini tu na ndugu wa mjini, Nina rafiki aliwahi kurudi kwenye msiba wa bibi yake tu tangu hapo hapajui Makete,
 
Ni utamaduni unaonishangaza sana, kila ikifika december Wachaga wote wa nje ya mikoa na nje ya nchi hukusanyika pamoja kwenye mizizi yao wanakotokea kwenye vijiji vya mkoa wa Kilimanjaro.

Mwaka jana pekee nilistuka sana baada ya kuona status za wachaga watatu wanaoishi nje ya nchi wamefika huko kwao, Yupo anaeishi China jiji la Guangzou, Marekani jiji la San Fransisco na mwengine wa Australia jiji la Sydney.

Kwa utafiti niliofanya kidogo makutano hayo ni kukutanisha ndugu wote, majirani mpaka marafiki mliosoma utotoni, watoto waliozaliwa huku mijini ama nje ya nchi wanaenda kutambulishwa kwenye mizizi yao, nadhani hata kama ulikopa duka la mangi hicho kipindi utadakwa tu.

Tukija huku makabila mengine ni nadra sana walio mijini ama nje ya nchi kurudi kwenye mizizi yao, Labda sana sana itokee kuna msiba huko kijijini watazika na kila moja kuondoka.

Binafsi kwa mzee ni kanda ya ziwa huko, Yeye alikulia kijijini huwa anaenda kila mwaka lakini mimi nilienda mara 2 tu nikiwa darasa la sita na la saba, shughuli ikaishia hapo !! kwakweli ni kipindi kirefu sana kimepita, naowahesabia ni ndugu ni wale tunaokutana mjini ila kule kwenye mizizi nishapoteza connection nao na hata watoto wakiniuliza kijijini ni wapi nawaambia ni mtaa wa mjini nilikozaliwa.

Nipo mikoa ya Iringa ya Mbeya ila kwa mfano wa kabila maarufu ntawatolea wanyakyusa wa Mbeya, Kwa wale waliozaliwa nje ya sehemu za mizizi yao (Tukuyu ama Kyela) nao mambo ya kurudi kwao ni changamoto, Kwa waliozaliwa mjini hata undugu ni ule wa kujuana ndugu wa mjini. Ikitokea wamerudi huko kwao labda kuwe na mazishi, hali inakuwa mbaya zaidi kwa watoto wa hawa wanyakyusa waliozaliwa mijini wanaweza hata wasipajue Tukuyu,

Wengine nao ni wakinga wa huko Njombe wapo sana hio miji nayoishi, Wazazi waliokulia huko vijijini huwa wanarudi rudi lakini watoto wanaishia kupajua mjini tu na ndugu wa mjini, Nina rafiki aliwahi kurudi kwenye msiba wa bibi yake tu tangu hapo hapajui Makete,
Utamduni huu upo kwa Wachaga na Wahaya tu. Wahaya wamekuwa na utamaduni huo tangu enzi na enzi. Mpaka kurudi wamekuandika kwenye vitabu vinavyotumia lugha yao. Tofauti Wahaya hawafanyi matambiko ya kichawi kama wafanyavyo wachaga. Wale walioko nje ya nchi wanakutana kwenye mizizi yao kwa muda wanaokuwa wamepanga siyo iwe kwenye kipindi kimoja cha sikukuu.

Nasema matambiko ya KICHAWI kwasababu Kilimanjaro (wilaya za wachaga) ukitoa Wapare kwa mujibu wa taarifa za NBS ndiyo inaongoza kwa kuwa na watu wenye ulemavu. Ulemavu huu si wa kuzaliwa bali ni ule wa kichwawi wa mali ambao kila disemba lazima watimize masharti ya kumwaga damu.
 
Hata wapare(kwa kuiga watani zao) wanaenda japo sio kwa uwingi huo.
Ishu ni umoja wa kurudi kwa pamoja, unaweza kuwaiga kwenda lakini ukifika huko unajikuta ulieenda upo peke yako, ni heri uende hata kipindi cha likizo kuliko kulazimisha kwenda kwa kuiga
 
Utamduni huu upo kwa Wachaga na Wahaya tu. Wahaya wamekuwa na utamaduni huo tangu enzi na enzi. Mpaka kurudi wamekuandika kwenye vitabu vinavyotumia lugha yao. Tofauti Wahaya hawafanyi matambiko ya kichawi kama wafanyavyo wachaga. Wale walioko nje ya nchi wanakutana kwenye mizizi yao kwa muda wanaokuwa wamepanga siyo iwe kwenye kipindi kimoja cha sikukuu.

Nasema matambiko ya KICHAWI kwasababu Kilimanjaro (wilaya za wachaga) ukitoa Wapare kwa mujibu wa taarifa za NBS ndiyo inaongoza kwa kuwa na watu wenye ulemavu. Ulemavu huu si wa kuzaliwa bali ni ule wa kichwawi wa mali ambao kila disemba lazima watimize masharti ya kumwaga damu
Ukiachana na wahaya waliokulia vijini kwao, hawa waliozaliwa mjini tupo nao mjini January to December, ikitokea wameenda aidha kuwe na msiba au mara chache wameenda na baba yao.

Kwa wachaga ukiniambia sifa zao mbaya zinazosifika kwamba kuna matapeli nakuunga mkono ila sio uchawi, haya mambo yapo ila kwa kiwango cha chini sana kwa mtu moja moja tena ni ule wa kununua kwengine maana hata kumpata mganga wa kienyeji wa kichaga utakesha.

Kuhusu kurudi December ni kipindi maarufu kwa holidays duniani kote.
 
Wahaya nao ni wale wale tu, waliokulia huko vijijini ama Bukoba wanarudigi kwao tena wapo waliojenga nyumba za kisasa lakini hawa waliozaliwa mijini hawana utamaduni wa kururudi vijijini, ikitokea wameenda labda kuwe na msiba ama ni mzee wao alikulia huko kaamua kwenda nao,
Rejea kusoma post yangu hapo kwa walioko nje ya nchi ambayo inaenda mpaka kwa wale waliozaliwa maeneo mengine na hawakurudi kipindi cha sikukuu. Wachaga ni lini wanarudi kwao na kufanya makutano ya kifamilia nje ya disemba? Hapo ndiyo utaona utofauti ulipo.
 
Kurudi December ndio msimu wa mapumziko, hata kabila la Igbo lenye mafanikio zaidi NIgeria na wakikuyu wa hapo Kenya huwa wanarudi kwao December.
 
Utamduni huu upo kwa Wachaga na Wahaya tu. Wahaya wamekuwa na utamaduni huo tangu enzi na enzi. Mpaka kurudi wamekuandika kwenye vitabu vinavyotumia lugha yao. Tofauti Wahaya hawafanyi matambiko ya kichawi kama wafanyavyo wachaga. Wale walioko nje ya nchi wanakutana kwenye mizizi yao kwa muda wanaokuwa wamepanga siyo iwe kwenye kipindi kimoja cha sikukuu.

Nasema matambiko ya KICHAWI kwasababu Kilimanjaro (wilaya za wachaga) ukitoa Wapare kwa mujibu wa taarifa za NBS ndiyo inaongoza kwa kuwa na watu wenye ulemavu. Ulemavu huu si wa kuzaliwa bali ni ule wa kichwawi wa mali ambao kila disemba lazima watimize masharti ya kumwaga damu.
Uongo, kwanza wahaya hawaendi kwao kama wachaga, tupo nao mjini January to December. Pili, wachaga ndio kabila least kwenye ushirikina, dini ya ukristo imefuta mila sana , japo kwa nadra mtu mmoja mmoja anaweza kuwa na mambo hayo, ila in general ndio kabila linaongoza kwa hofu ya Mungu, angalia idadi ya wachungaji na mapadri, we huwajui. Ignorance inakusumbua, alafu pia punguza husda. Itakusaidia.
 
Acha kuongopea wasiowajua kijana. Achana na masuala ya idadi ya wachungaji na mapadri. Eti kabila least kwenye ushirikina!!. Thubutu. Ni mchaga unayetumia nguvu kuficha uozo wenu ili wanaosoma hapa waone mko sawa. Ndugu zangu walioa na kuolewa huko. Kinachoendelea huko disemba mnakijua. Nimezunguka kwenye maeneo yenu kwa miaka 14. Utaumbuka kijana. Ulishakaa chini ni kwanini mnazika sana ndugu zenu kila baada ya disemba na pasaka?. Ukijibu hilo utajua kwanini nimesema tofauti ya nyie na wahaya ni matambiko ya kichawi

Wewe unasema wahaya uko nao january to december wakari huo huo unasema unaenda kwenu disemba..sasa hiyo disemba unakuwa nao wapi??? Ukirejea post yangu iko wazi kabisa
 
Wahaya wangekuwa wanarudi huko kwao basi kungekuwa kumejengeka huko vijijini, sio hizi picha tunazoziona vijijini kuna nyumba kibao za tope huku zile za kisasa zinahesabika zilizojengwa na wachache wanaorudi vijijini

1699820848598.png
 
wahaya waliozaliwa mjini tupo nao mjini January to December.

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpe, Ukiniambia utapeli naweza kukubali ila sio uchawi, wapi na wapi mchaga na mambo ya kutupiana mabusha, kupaa na ungo usiku, kutembea na fisi usiku, malimbwata, n.k. ? Yani hata kusikia kuna mganga wa kichaga lazima ustuke mapema huyo ni tapeli !! uchawi unaweza kuwepo ila ni kwa mtu moja moja tena ule wa kuununua kwengine.

Kuhusu kurudi December ni kipindi maarufu kwa holidays duniani kote.
Wewe unafikiri uchawi ni kutupiana tu mabusha na kupaa kwa ungo. Pole sana. Unaweza kuniambia ni kwanini mnazika ndugu zenu sana baada ya disemba na pasaka? Unasema kusikia mganga wa kichaga lazima ustuke..ebu niambie yule mzee wa pale rau madukani ukishayapita maduka kule kwenye kona mbele anafanya nini, pale rombo maarufu kcmc kuna nini, kule vunjo kitongoji anapokaa mzee manjuu wa majengo kuna nini. Usitake tuweke wazi mambo yenu.
 
Wahaya wangekuwa wanarudi huko kwao basi kungekuwa kumejengeka huko vijijini, sio hizi picha tunazoziona vijijini kuna nyumba kibao za tope huku zile za kisasa zinahesabika zilizojengwa na wachache wanaorudi vijijini

View attachment 2812108
Kurudi au kutokurudi hakuhusiani na kujenga kwenye maeneo yao. Sasa unaongelea nyumba za udongo kuwepo kwa wahaya, hizo nyumba za tope ziko kila sehemu ya nchi hii.

Niambie nyumba za hivi kwenye picha zilizojaa hapo vunjo ni na huko ndani ndani ni nini
 
Attachments

  • Screenshot_2023-11-12-23-39-00-88_40deb401b9ffe8e1df2f1cc5ba480b12.jpg
    Screenshot_2023-11-12-23-39-00-88_40deb401b9ffe8e1df2f1cc5ba480b12.jpg
    103.5 KB · Views: 10
Wewe unafikiri uchawi ni kutupiana tu mabusha na kupaa kwa ungo. Pole sana. Unaweza kuniambia ni kwanini mnazika ndugu zenu sana baada ya disemba na pasaka? Unasema kusikia mganga wa kichaga lazima ustuke..ebu niambie yule mzee wa pale rau madukani ukishayapita maduka kule kwenye kona mbele anafanya nini, pale rombo maarufu kcmc kuna nini, kule vunjo kitongoji anapokaa mzee manjuu wa majengo kuna nini. Usitake tuweke wazi mambo yenu.
Mimi sio mchaga nishaainisha natokea kanda ya ziwa,

Anyway naona hii maada unaanza kuipeleka kwengine kabisa inapoteza dira, hayo mambo ya uchawi naona unayapenda sana kuyazungumzia naona yatajaza uzi, Turudi kwenye maada kuu

Tukiachana na wachaga, Kuna kabila lingine lina utamaduni wa kurudi na kujumuika kwenye vijiji vya mizizi yao nje ya misiba?
 
Kurudi au kutokurudi hakuhusiani na kujenga kwenye maeneo yao. Sasa unaongelea nyumba za udongo kuwepo kwa wahaya, hizo nyumba za tope ziko kila sehemu ya nchi hii.

Niambie nyumba za hivi kwenye picha zilizojaa hapo vunjo ni na huko ndani ndani ni nini
Hio picha uliyoweka ni kwa wapare, Ukoo wa kina Mchomvu ni wapare, hata mtangazaji wa clouds fm Adam Mchomvu ni Mpare
 
Back
Top Bottom