Jenerali Venance Mabeyo ametuonesha kuwa kuna viongozi wanaapa kuilinda Katiba ambayo hawaijui na hawaisomi, na ndio maana aliwakumbusha

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
15,262
9,714
Ndugu zangu Watanzania,

Nimepata uoga mkubwa sana moyoni mwangu na hofu kubwa sana akilini mwangu na kutetemeka sana mwili wangu na kupatwa na ganzi katika mwili wangu. Hapa ni pale baada ya kurejea kauli ya mkuu wa majeshi mstaafu Jenerali Venance Mabeyo aliyosema kuwa aliwakumbusha viongozi juu ya kile inachosema katiba katika tukio lililokuwa limetokea la kuondokewa na Mpendwa wetu Hayati Mwalimu Dkt Magufuli na namna madaraka ya Urais yanavyotakiwa kukabidhiwa kwa makamu wa Rais pamoja na taratibu za kufuata hatua kwa hatua kwa mujibu wa katiba yetu.

Mimi Mwashambwa Lucas nimejiuliza tumaswali tuchache kwa akili yangu hii hii kama mwananchi wa kawaida nisiye kiongozi.kwamba ni kweli hawa viongozi wetu walikuwa wameisahau kabisa katiba waliyoapa kuilinda inasema nini mpaka inafikia hatua ya kukumbushwa na mkuu wa Majeshi? Walikuwa wameshindwa kwenda kuisoma katiba yetu kabla ya kufanya maamuzi? Walikuwa wameshindwa kumtafuta na kumshirikisha hata mwanasheria mkuu wa serikali ambaye ndiye mshauri mkuu wa masuala yote ya kisheria kwa serikali? Katika kutokujua kwao au kusahau kwao juu ya katiba inasema nini.je walitaka wafanye nini au wachukue uamuzi upi kwa Taifa letu kwa mstakabali wa Taifa letu kabla ya kukumbushwa?.

Je, kuna uwezekano kuwa kuna baaadhi ya viongozi wetu huwa hawaisomi katiba wanayoapa kuilinda ,kuitetea na kuihifadhi? Unawezaje kulinda au kutetea kitu au jambo usilolijuwa wala kulielewa undani wake? Kama hawaisomi katiba ambayo ndio muongozo wao kwa kila jambo na kwa kila maamuzi wanayoyafanya hatuoni kuwa inakuwa ni hatari sana kwa mustakabali wa Taifa letu.

Nini kingetokea kwa Taifa letu na historia yake kama mkuu wa Majeshi asingewakumbusha viongozi wetu juu ya matakwa ya katiba? Nini kingetokea kama Mkuu wa Majeshi angeamua naye kukaa kimya au kama naye angekuwa amesahau kama wao? Nini kingetokea kama mkuu wa Majeshi naye angekuwa hasomi katiba aliyoapa kuilinda na kuitetea? Nani angemkumbusha mwenzake wakati inaonekana mkuu wa Majeshi ndio alikuwa mtu na kiongozi wa mwisho kukumbuka matakwa ya katiba baada ya viongozi wenzake kuwa wamesahau matakwa ya katiba?

Je, tufanye nini na nini kifanyike ili hata ikitokea viongozi wetu wakawa wamesahau juu ya nini katiba inahitaji waweze kukumbushwa kwa urahisi? Kwa sababu hatuwezi kufahamu katika matukio mengine pengine viongozi wote wanaweza kutokea wakawa wamesahau matakwa ya katiba .hamuoni itakuwa hatari kwa Taifa na hata kuhatarisha usalama wa Taifa baada ya kuchukua na kufanya maamuzi yaliyo kinyume na katiba , halafu baadaye viongozi wetu wakaja kukumbushwa na wananchi wa kawaida kuwa mmekosea na kusahau matakwa ya katiba yanataka nini? Hamuoni jambo hili linaweza kuchochea machafuko au mgawanyiko na mpasuko kwa Taifa na viongozi wetu kudharaulika kwa kuonekana kuwa wanaapa kuilinda na kuitetea katiba lakini hawaijuwi na wala hawaisomi?

Je, viongozi wetu wawe wanapewa semina ya katiba kabla ya kuanza majukumu yao na kusisitizwa juu ya kuisoma katiba yetu mara kwa mara ili wasije wakatokea wakafanya maamuzi yenye athari kwa Taifa na yenye gharama kubwa kwa nchi?

Naomba tusaidiane watanzania wenzangu kuwa nini kifanyike ili kila kiongozi awe anajuwa nini kinapaswa kufanyika katika jambo fulani hata pasipo kukumbushwa na mtu?

Mwisho naomba kwa dhati ya Moyo wangu mimi Mwashambwa Lucas kuomba radhi kwa yeyote nitakaye kuwa nimemkwaza kwa maandiko yangu iwe leo au jana au juzi au siku yoyote ile tangia nimeanza kuandika humu jukwaani.hakuna nilipofanya kwa makusudi au kwa dhamira mbaya au kwa kumchafua mtu.siku zote upendo wangu ni kwa Taifa langu na mapenzi mema kwa watanzania wenzangu.kiu yangu ni kutaka kuona nchi yetu ikiendelea kutamalaki kwa amani ,utulivu na upendo.ndio maana mnaona nimekuwa mnyenyekevu na mwenye kuchunga ulimi wangu kupitia vidole vyangu vya uandishi.

Mnisamehe sana napowakoseeni na mniwie sana radhi.sisi sote ni binadamu na hakuna aliye kamilika.najuwa Taifa letu ni changa kidemokrasia na tupo katika safari ya kupalilia demokrasia ili kufikia walipo fika mataifa kama Marekani au Uingereza au Ufaransa na mengineyo. Kwa Mataifa yetu ya Afrika wakati mwingine unaweza kuandika kama hivi ikaonekana kwa baadhi ya watu au viongozi kama vile huna adabu au una Shari au una chuki na mtu au hufai kwa lolote au huna akili au muongeaji sana.

Yote kwa yote nalipenda sana Taifa langu la Tanzania na najivunia sana kuwa mtanzania na kuzaliwa Tanzania kisiwa cha Amani ,kivumacho kwa upepo wa upendo upitao katika masikio na macho ya watanzania.

Mwisho nawapenda sana viongozi wangu na kuwaheshimu sana.nathimini sana Mchango wao kwa Taifa letu.wote waliopo madarakani na wale waliostaafu na hata wale waliotangulia mbele za haki.

Kazi iendelee, mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

 
Pia imetuonesha kwamba ccm wapo kwaajili ya matumbo yao na siyo kwaajili ya nchi.
Umesahau kuandika namba ya simu mtoa mada
 
Wanaijua wanaisoma ila wameamua kuipuuza kwa maslahi yao, ndio maana tumelilia uwepo wa mikutano ya hadhara kama vile ni hisani ya mtawala wakati ni takwa la kisheria.
 
Back
Top Bottom