Mwenzenu yamenikuta na kusema za ukweli nashindwa kabisa kuelewa namna ya kutoka hapa na kusonga mbele.
Ni mume nilompenda sana sana sana. Mungu katujaalia two beautifull kids na mengine ambayo am greatfull for. Tuliishi kwa upendo,furaha na amani hadi miezi 8 ilopita nilipogundua kuwa nilivyomdhania mume wangu sivyo alivyo.
Kwakuwa nampenda na kumfahamu sana mume wangu, kuna kitu nilikuwa tu nakihisi hakiko sawa kwa muda. Baadae nikagundua he was cheating. Yaani sitaki kuelezea mstuko niloupata na jinsi ninaumia jamani. Japo aliomba sana msamaha and all that ila moyo wangu umekufa ganzi wapendwa.
Mume nilompenda sana kwasasa namuona kama jirani yangu tu, hata hamu nae sina kabisa na hata tendo la ndoa ni kama ananibaka tu. Tushaongea sana, tushakwenda hadi vacation sie wawili tu ila sioni kinachobadilika. Akisafiri kikazi au mimi nikisafiri najisikia amani zaidi and i dont miss him kabisa.
Kuna wakati nilimuomba some alone time nifikirie kuhusu mustakabali wa hii ndoa, alinipa huo muda na kwa kipindi hicho cha wiki moja kichwani mwangu nilishangaa kunazunguka watoto wetu tu na sio mume wangu. Sijamueleza mtu yeyote kuhusu hili hata mama yangu wala mshenga wetu ila linanitafuna hatari.
Wenzangu mnawezaje kusamehe wanaume wanaowacheat na kurudi katika hali zenu za kawaida? Maana mie kwasasa mume wangu namuonaje sijui, nae naona hali hii inamtesa ila ndio hivyo tena[emoji134]
Sijisikii kumpenda wala kumheshimu tena, naona kama hadeserve kwa kutokuithamini na kuivuruga ndoa yetu.
Pole sana sana mpendwa..maumivu ya kusalitiwa na uliyempenda, kumuheshimu na kumjali na kuamini inauma sana tena sana..sijui kwanini watu wengine find this post to be funny..inasikitisha sana..
Nikwambie kitu...mama dunia imeisha, dunia imeharibika..ndoa siku hizi imepoteza heshima..watu wanashabikia uzinzi na zinaa...zinaa sio ya kuogopwa tena...ona wanaume wa humu wanavyoshabikia, ona wanawake wenzio wanavyorespond kwa kukata tamaa...kwakweli sijui mustakabali wa familia zitakazo kuja kuwepo after ten years...
Usimuache mumeo, tanguliza kwanza maslahi ya watoto..omba Mungu sana akupe moyo wa kusamehe na hekma ya kukabiliana na jaribu hili..kila mwanamke kwenye ndoa lazima ameshakumbana na jaribu hili..na kama mwanamke hujakumbana nalo jua tuu siku yaja tena sanyingine accidentally unajikuta you are presented with ushahidi kwa bahati mbaya bila hata ya kukusudia..
Jiandae kisaikolojia kuishi na maumivu haya...ila ukimtanguliza Mungu, ukabadili vipaumbele na kuweka furaha yako mbele na wekeza on your well being..kama una shughuli ya kukuingizia kipato focus on it kama huna anza kujishughulisha na kujikeep busy..treat yourself well, nenda kwenye spa, buy yourself gifts..be a little selfish...tumia muda na wanao wapeleke kubembea au kwenye michezo..kua busy mama..siku zitaenda..and you will be fine..
Afya yako ya mwili na akili ni muhimu mnoo kipindi hiki..mimi nakumbuka mpaka nilipigiwa simu na mwalimu wa mtoto akiniuliza kwanini siku hizi sikagui homework za mtoto..nililia kwa uchungu sana nikashtuka kua suala hili linaafect nyanja zote za ustawi wa familia am 35 yrs lakini nilikonda mpaka 46 kgs..presha ilikua chini all the time, nilijichukia, nilijidharau na kujiuliza maswali mengi yasiyo na majibu...i prayed iwe ni ndoto tuu..lakini hapana..it was a reality....bila Mungu kukuongoza katika jaribu hili unaweza kufanya maamuzi mabaya yasiyo sahihi.
Usijisumbue kumueleza mama yako...atakuambia vumilia..
Kumbuka kua hajakukosea wewe kuliko anavyomkosea Muumba wake, wala hawezi kukuumiza wewe kuliko aliyemuumba, haukuja kwenye maisha yake uwe mhesabuji wa dhambi zake sababu hata akiwa mkamilifu huna mbingu ya kumpeleka na akiwamkosefu huna mamlaka au jehanam ya kumpeleka..usijishughulishe na madhambi ya mtu mzima..wewe na wanao muwe kipaumbele kwako...
Nakutakia kheri and i cant wait for the feedback