Pole sana sana mpendwa..maumivu ya kusalitiwa na uliyempenda, kumuheshimu na kumjali na kuamini inauma sana tena sana..sijui kwanini watu wengine find this post to be funny..inasikitisha sana..
Nikwambie kitu...mama dunia imeisha, dunia imeharibika..ndoa siku hizi imepoteza heshima..watu wanashabikia uzinzi na zinaa...zinaa sio ya kuogopwa tena...ona wanaume wa humu wanavyoshabikia, ona wanawake wenzio wanavyorespond kwa kukata tamaa...kwakweli sijui mustakabali wa familia zitakazo kuja kuwepo after ten years...
Usimuache mumeo, tanguliza kwanza maslahi ya watoto..omba Mungu sana akupe moyo wa kusamehe na hekma ya kukabiliana na jaribu hili..kila mwanamke kwenye ndoa lazima ameshakumbana na jaribu hili..na kama mwanamke hujakumbana nalo jua tuu siku yaja tena sanyingine accidentally unajikuta you are presented with ushahidi kwa bahati mbaya bila hata ya kukusudia..
Jiandae kisaikolojia kuishi na maumivu haya...ila ukimtanguliza Mungu, ukabadili vipaumbele na kuweka furaha yako mbele na wekeza on your well being..kama una shughuli ya kukuingizia kipato focus on it kama huna anza kujishughulisha na kujikeep busy..treat yourself well, nenda kwenye spa, buy yourself gifts..be a little selfish...tumia muda na wanao wapeleke kubembea au kwenye michezo..kua busy mama..siku zitaenda..and you will be fine..
Afya yako ya mwili na akili ni muhimu mnoo kipindi hiki..mimi nakumbuka mpaka nilipigiwa simu na mwalimu wa mtoto akiniuliza kwanini siku hizi sikagui homework za mtoto..nililia kwa uchungu sana nikashtuka kua suala hili linaafect nyanja zote za ustawi wa familia am 35 yrs lakini nilikonda mpaka 46 kgs..presha ilikua chini all the time, nilijichukia, nilijidharau na kujiuliza maswali mengi yasiyo na majibu...i prayed iwe ni ndoto tuu..lakini hapana..it was a reality....bila Mungu kukuongoza katika jaribu hili unaweza kufanya maamuzi mabaya yasiyo sahihi.
Usijisumbue kumueleza mama yako...atakuambia vumilia..
Kumbuka kua hajakukosea wewe kuliko anavyomkosea Muumba wake, wala hawezi kukuumiza wewe kuliko aliyemuumba, haukuja kwenye maisha yake uwe mhesabuji wa dhambi zake sababu hata akiwa mkamilifu huna mbingu ya kumpeleka na akiwamkosefu huna mamlaka au jehanam ya kumpeleka..usijishughulishe na madhambi ya mtu mzima..wewe na wanao muwe kipaumbele kwako...
Nakutakia kheri and i cant wait for the feedback