Wanawake wengi hawawataki wanaume maskini

Wanawake wengi hawawataki wanaume maskini

Tunaweza na huwa tunapambana sana, wengine hatujazoea kukaa tu kusubiri kuletewa ila ndio hivyo inavyokuwa..
Punguzeni entitlement kwenye mali za mwanaume. Mali zibaki kuwa mali na mapenzi yabaki kuwa mapenzi. Mapenzi yakiisha kila mmoja anachukua njia yake na alichokipata kwa jasho lake
 
Wengi wa aina hiyo wanakuwa wametokea kwenye familia za kimasikini.

Huwa najiuliza, hivi wao hawajiulizi ni kwanini Mama zao waliwavumilia Baba zao kujenga familia katika hali ya umasikini?

Kama hela ni jambo la muhimu mwanaume kuwa nalo ili kudumisha mahusiano, kwanini Baba zao hawana?

Hapa kuna tabia inajengeka.

Kwamba Mwanamke anaiona thamani ya mwanaume pale tu ambapo huyo mwanaume atakua na hela.

Na sasa mwanaume akiwa na hela unakuwa unamtengenezea mazingira ya kutoona value ya mahusiano kwasababu anajua uko hapo kwasababu ya hela zake.

Automatically hiyo inakuwa inamkata stimu emotionally.
Hypergamy ni nature ya mwanamke, kuhusu ilo hatuwezi kuwalaumu moja kwa moja. Lakini angalao sasa na yeye aweze kumudu gharama za maisha aliyochagua kuishi, sio kutaka extravaganza lifestyle harafu sponsor awe mwanaume.
 
Na ukizingatia kwamba zaidi ya watanzania 47m ni masikini, mabinti wengi wataolewa na masikini watake wasitake. Bora wajiandae kisaikolojia tu.
Umeongea ukweli ambao kwa sababu wanawake sio watu wa kuwaza logically hawawezi kukuelewa. Daraja la sanaume wa ndoto zao ni kama 4% tu ya wanaume wote, kihesabu hawawezi kuwaoa wanawake wote waliopo kwenye dating pool, cha kushangaza wanawake wanafikiri duniani kuna idadi ya wanaume matajiri wa kutosha kuwaoa wote
 
Pata vitu kulingana na uwezo wako , tatizo letu tunataka pisi kali na hatuna kitu mifukoni ndio maana vilio ni vingi.

Huko kyela wamejaa wanawake kibao wala hawachagui na wapo tayari kuanza moja na wewe bwashee
Ndio maana mimi huwa nawashauri vijana waachane kwanza na suala la mahusiano,, watengeneze maisha yao. Ukiwa na maisha duni utalazimika ku-settle for less. Kesho ukizipata utamuona partner wako sio hadhi yako. Tafuta kwanza purchasing power ndio uende sokoni
 
Kamanda wangu mmoja wakati was kumuaga pale Lugalo pisi aliyozaa nayo ikaleta mzozo ipate mgawo wake isepe na mjukuu.
Wachaga wale pale pale msiban walimlipua vibaya sn bibie kuwa mtoto ni wetu ila wewe hatukujui na hatukuwahi kutambulishwa.
Hivyo oasua nyika uende.
Ulivyokula kinyemela ndio Shea yk..
 
Je, wewe baba mwenye binti utafurahi siku binti yako akikuletea mchumba hana kitu kabisa.

Umasikini ni laana, basi tu wengi wetu tunatokea familia masikini, tumekulia umasikini, tunazeeka na umasikini wetu hivyo tunaona kuwa masikini ni sifa chanya.
Tatizo ni unrealistic expectation ndugu yangu. Kinachoongelewa hapa sio umasikini wa usema kijana hana kitu wala potential yoyote inaeleweka wanaume tunapoingia kwenye dating pool tunakua hatuna thamani sasa demu wa miaka 22 kweli alitegemea mwanaume ambae ni agemate wake awe na uwezo wa kumtatulia mahitaji yake ya kifedha. Nitamuelewa demu akimpiga chini kijana masikini mwenye miaka angalao 30 kwa sababu katika huo umri mwanaume alitakiwa angalao awe na muelekeo wa maisha. Lakini kutaka kijana wa kiume miaka 21 ashindane na mashuga dady hapa tunawaonea tu vijana
 
The Haves and Have Nots lol 😆

Kwahiyo hakuna haja ya kutafuta mchawi nani basi ndomaana nakimbiwa sana😂😂kumbe shida ombaomba😝
Kumuomba mwanaume hela sio shida, as long as una intention nzuri, na huyo mwanaume atai-sense hiyo intention yako nzuri, kulingana pia na unavom-treat.. mfano huwezi ni-treat kwa kuninyanyapaa halafu uniombe hela nikuelewe, hata kama ntakupa hela lazma nikuone tapeli, kimoyomoyo ntakua na question marks Seran
 
Ndo umasikini huo sasa. Huu wa kushindwa kumudu gharama flani flani ni jambo la kawaida tu ambalo jamii tumeliwekea maana mbaya.
Ume sema kukosa matumaini ndio umasikini, hebu nieleezee matumaini na uchumi vime ingiliana vipi?.

Mgonjwa akienda kufanyiwa operation, ila haamini atapona huo nao ni umasikini?

Ikiwa kalipia fees zote, na yuko kwenye hospital bora!
 
Kumuomba mwanaume hela sio shida, as long as una intention nzuri, na huyo mwanaume atai-sense hiyo intention yako nzuri, kulingana pia na unavom-treat.. mfano huwezi ni-treat kwa kuninyanyapaa halafu uniombe hela nikuelewe, hata kama ntakupa hela lazma nikuone tapeli, kimoyomoyo ntakua na question marks Seran
Mimi. Seran ni wangu hapo vipi,?
 
Sawa ila mwanaume mwenye akili za kimasikini achukue ustaarabu wake tu, kuvuka sio kazi nyepesi!
Mwanaume huwa thamani yake inaanzia chini. Umasikini ni default starting ya almost kila mwanaume, ni tofauti na nyie ambao mnaingia kwenye dating pool thamani yenu ikiwa tayari ipo juu. Kumtaka kijana wa 20's awe na gari, nyumba, kazi na hela ya kutimiza mahitaji ya mwanamke ni kumwonea tu huyo kijana. Unachokiongelea sio umasikini kama hali ya kudumu ila ni default starting ya karibu wanaume wote
 
Back
Top Bottom