Wengi wa aina hiyo wanakuwa wametokea kwenye familia za kimasikini.
Huwa najiuliza, hivi wao hawajiulizi ni kwanini Mama zao waliwavumilia Baba zao kujenga familia katika hali ya umasikini?
Kama hela ni jambo la muhimu mwanaume kuwa nalo ili kudumisha mahusiano, kwanini Baba zao hawana?
Hapa kuna tabia inajengeka.
Kwamba Mwanamke anaiona thamani ya mwanaume pale tu ambapo huyo mwanaume atakua na hela.
Na sasa mwanaume akiwa na hela unakuwa unamtengenezea mazingira ya kutoona value ya mahusiano kwasababu anajua uko hapo kwasababu ya hela zake.
Automatically hiyo inakuwa inamkata stimu emotionally.