Wanawake tujikumbushie vituko vya leba

Wanawake tujikumbushie vituko vya leba

ahaha mm nakumbka hapo saa 2 usk nipo hoi..nikamuita Dk wa kiume !nikamwambia nisikilize vzr nachoumwa maana manesi hawatak kunpa panadol!heehe nikamweleza nitabirie dk ntazaa saa ngapi!akaniambia ww utazaa saa 11!jaman yale maumiv hayafai jaman!niliumwa uchung toka saa 1 asbh nikajiopen saa 11 alfajir !nilipelekwa labor na mume wangu !jaman nilikuwa namuuma mgongon ananiambia mbiti unaniumiza mie sielew ktu! asbh naitwa jina langu mume kaja niletea uji jaman niliangusha kilio sio cha nchi hii !bas mwenzangu akawa anacheka tu!

nilianza kutembea fresh baada ya miez 2 nilikua natembea km narudi nyuma !nikaambiwa mtoto alikalia 'masozi 'za miguu !yaan huwa tunakumbshiana na Mr nacheka hatari !najipanga nirudi tuu tena siwez ishi bila ya bbygal jaman!
 
Mmmhh shikamooh mama mie nilivyoenda leba nasikia nilisema "uwiii wanaume wote wafe" manesi wakanijibu afe wa kwangu tu maana waume zao bado wanawapenda hahahhaha sitaki kusikia leba maana akili haikuwa yangu mweehh shkamooh mama
sorry nimecheka mana wenzio woote zimenitoa machozi....wewe umenichekesha na hayo majibu ya manesii
 
wanawake wa siku hizi shida tupu...... hii nini sasa.

nani asiyejua kuwa mnazaa kwa uchungu, hata kwenye biblia imeandikwa, sasa kuja kusimuliana humu ni kujikosea heshima wenyewe, wala haina maana, mnawadhalilisha wanawake wenzenu
Shit hole go you tube uwaambie
 
Mwanamke uliyefundwa huwezi kusema haya mambo hadharani

Ni eidha ulizaa ukiwa mwanafunzi/mwanachuo au umekuwa mama kabla ya wakati wako.

Vinavyofanyika/kutokea leba ni siri, kuvimwaga hadharani hapa ni kujivua nguo. Ndio maana hata manesi/wakunga hawavitoi nje.
Dunia imebadilika chief, tupo karne ya 21 tunakimbilia ya 22
 
Wanawake wa kuwaheshimu kwa kwel. Nilimpeleka dada angu jumapili akaja kujifungua ijumaa. Mie ndio nlikua nashinda nae hospital nlikua namwambia mama na baba wawe wanakuja muda wa chakula tu na mumewe alikua anakuja jion. Kwa kwel alipata tabu sana mpaka alikonda. Alivyojifungua wa kwanza kumpigia simu nlikua mie mdogo wake akaniambia asante kaka angu kiukwel machoz yalinitoka manake nlidhan ningemkosa dada angu
 
Jamani jamani jamani kila nikiingia leba naanza na neno nitatoka salama humu? Huwa nakata tamaa kabisaaa hasa maumivu ya mgongo na kiuno yakichachamaaa euwiiiììii huwa naomba msaada hata wa mtu asiehusika. Sitakaa nisahau mwanangu wa kwanza niliteseka uchungu siku 2 mpka muda wa ku push nguvu sina ikabidi wamvute mtoto kwa vacuum thanks God nilikua kwa hospital yenye specialist mtoto hakupata madhara. Uchungu wa kuzaa hakuna mfanowe ndipo wamama wengi hufariki kwa sbb kuna wengine presha zinapanda au kushuka ghafla kwa maumivu. Wababa kule ni nusu kifo muwe mnatuombea tutoke salama
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom