Wenye ndoa zenye furaha hawajitokezi kuanza kujisifia, siku zote mtu anayejisifia Kuna kitu anaficha, kwa tabia ya binadamu,ndoa nzuri haionekani kwa wahusika kujisifia, na wahusika huwa wako makini Sana kutokuonyesha kwa watu.
Watu wanaoweza kujua ndoa nzuri ni sadists only, Hawa ni watu waliokata tamaa na Maisha yao katika nyanja zote na hawezi kukaa na kuona wengine wanafanikiwa, hawa Wana uwezo mkubwa Sana wa kujua ndoa nzuri, waharibifu Hawa huwa wanainusa ndoa nzuri na kuanza harakati za kuibomoa.
Kwa Maisha ya Sasa ndoa nzuri ziko chache Sana, huu ndio ukweli, na hii inatokana na watu kutokuishi kwa uhalisia.
uhalisia unapatikana katika uumbaji wa Mungu na asili ya vitu na viumbe mbalimbali akiwepo mwanadamu, Rehema mbalimbali alizotupa kama vipawa, elimu mbalimbali ya mazingira yetu, viumbe mbalimbali na tabia zake za asili na vitabu vyake vya dini, vinafundisha yote haya.