Your opinion please! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Your opinion please!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Dec 6, 2007.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Dec 6, 2007
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,456
  Likes Received: 81,692
  Trophy Points: 280

  Waungwana,

  Yule mpenda ligi (mashindano) na walio majuu Issa wa Michuzi kwa mara nyingine tena ameweka huu mjadala huko kwenye Blog yake. Nasema ni mpenda ligi kwa sababu kila kukicha hupenda kuweka mjadala huu na nia yake kubwa ni kutaka kuonyesha kwamba Watanzania walio nje wana maisha duni.

  Kwa maoni yangu Watanzania inaelekea priorities zetu ziko kimgongo mgongo. Nasema ziko kimgongo kwa sababu life span yetu ni 45 years, mtu akifikisha 50 huyo amekula chumvi nyingi mno. Hospitali zetu hazina vifaa vya kisasa na madaktari ni wachache. Mahospitalini vitanda hakuna, wagonjwa na hata akina mama wajawazito wanashare vitanda au kulala chini. Mashule yetu hayana walimu, hayana madawati na kama mjuavyo rasilimali zetu zinaibwa mchana kweupe na wageni wakisaidiwa na viongozi wabovu wanaosaini mikataba mibovu kila kukicha na kujilimbikizia mali wakati wengi wa Watanzania wanaishi maisha ya dhiki.

  Nasema priorities za Wabongo zimekaa kimgongo mgongo kwa sababu kuna mambo mengi ya maana ya kujadili kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu. Hili la kujadili wabongo walio majuu warudi nyumbani naona si mojawapo.

  Kama mazingira ya nyumbani yakiwa mazuri watakaotaka kurudi watarudi na kuna wengine huko waliko ndio wameshafika wao kuja bongo ni kutembea kwa muda tu maana wameridhika na hali ya maisha huko waliko na 'wameshapoteza Utanzania wao'

  Kazi kwenu, nanyi mchakarike kutoa mawazo yenu.

  *~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*~*

  .
   
 2. H

  Haika JF-Expert Member

  #2
  Jun 10, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  I love life in Bongo, but prefer to live in other regions especially in arusha or moshi when I am rich.
  foreign contires do not work for me as I money is not the only thing that makes me tick.
  I have to at home.
  not stared at enjoying the culture, not learning some culture and pretend that it is mine,
  speaking a foreign language year in year out. (i speak several)
  I just enjoy Tanzania more, but I can live somewhere else if I really need the cash.
  Now I live in Dar, (Bongo) when i am richer, i will move to Arusha or moshi.
   
 3. Freetown

  Freetown JF-Expert Member

  #3
  Jun 11, 2008
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  mimi ni mmoja ya watu wanaofanya kazi abroad, kazi nzuri ya professional yangu na mshahara mzuri, lakini home is home, nakupenda nyumabani, nipo huku tu kufukuzia hizi $.
  kila mtu ana malengo yake, lakini hili la kukaa nje maisha yote naona si wazo zuri. kuna vingi sana tunavikosa huku ugaibuni.
   
 4. B

  BeNoir Member

  #4
  Jun 11, 2008
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 97
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa moyo wangu wote na akili yangu yote napenda kuishi Tanzania, japo nimesoma, nimeishi na kufanya kazi nje na kulipwa mshahara mzuri sana kwani nimefanya kazi kwenye fani niliyosomea na si vinginevyo. Kwangu mimi yote ni muhimu. Kipato ni muhimu lakini ustawi wangu na kuenjoy life including insurance ya kuwa karibu na ndugu na jamaa ni muhimu sana kwangu. Sipendi kuishi nje kutokana na kutojisikia kuwa mmoja wao (belonging) au kutokuwa mmoja wao. Pia imeniwia vigumu kubadili au kuacha baadhi ya mila na desturi zangu.

  Lakini pamoja na ukweli huo, si kila mtu anapata kuwa na nafasi ya kuangalia jambo hilo kama nilivyoliangalia mimi. Ni kutokana sababu hiyo naheshimu na namsupport mtu atakayeamua kuchagua kuishi nje ya Tanzania, ili mradi anakidhi maisha yake. Na hilo nimelikubali na nalilisisitiza kwa ukweli ninauona nyumbani wa watu kutoweza kufanya kitu kwani mazingira hayatuwezeshi.

  Kuna faida gani kumaliza shule vizuri halafu huna ajira, wakati ukiwa nje una uwezo wa kupata ajira bila kujalisha ni ya aina gani lakini una kipato unapata. Ile hali ya kuweza kuwa na kipato ukikalipia kodi ya nyumba, kununua kagari kako japo mkweche, kuweza kujinunulia chakula, nguo na mahitaji mengine nadhani ndio heshima na utu wenyewe wa mwanadamu. Kwa kufikiri hivyo, ndio maana sina tatizo kabisa na mtu kuamua kubaki nje kama kurudi kwake nyumbani kumtafanya asiweze kukidhi mahitaji yake au ya watu wengine wanaomtegemea.

  Mazingira ya nyumbani kwa kweli ni magumu na yanaogopesha, japo mimi sikusita kufanya uamuzi huo. Lakini naamini kabisa kuna sababu zingine za msingi zilichangia kuopt kwangu kurudi nyumbani, ikiwa ni pamoja na kwamba nilikuwa na kazi, hivyo nilikuwa najua ninakoenda na kazi hiyo ilikuwa na good prospects. Kwa mtu ambaye hilo halipo, shaka lazima iwe kubwa, kwani utakuwa uzalendo potofu kama utajali tu kurudi nyumbani bila kujali prospects zako.

  Ubaya wa nje ni pale tu unapojikuta mara uitwe"Immigrant", mara "Alien", mara "Migrant", mara "Second Class citizen", na menginyo mengi. Kupata kazi za nyanja uliyosomea si rahisi na ukiipata kuna mikwara mingi sana. Ni kazi kukubalika kabisa kwenye jamii zao na kuna sisi wengine sio wavumilivu, hilo kidogo ni shida. Of course ukiamua kubaki nje ujue pia mila na desturi za kwenu ndio vimeyoyoma na vizazi vyako vitakuwa vinasikia tu mila na desturi zetu kama hadithi ya "Kusadikika".

  I respect both, wanaopenda kurudi nyumbani kwa uzalendo wao, lakini pia nawaheshimu wanaoamua kubaki nje kutokana na hali halisi.
   
 5. H

  Haika JF-Expert Member

  #5
  Jun 11, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  pia uamuzi kwamba hela ya kusotea nje ya nchi imetosha sasa ni muda wa kurudi nyumbani umefika, hupangwa na mhusika mwenyewe.
  Siwezi kumuambia mtu eti umejenga nyumba nzuri, umeanzisha biashara nzuri kwa hio rudi home, itambidi mwenyewe awe huru,
  manake kuna watu wako huko, wanaogopa tanzania sana, ni sababu ya mazingira walioyaacha yanawazunguka, tunawaelewa kabisa.
  Lakini hata kwa Tanzania kuna sehemu mbalimbali ukiishi, unakufa mapema hata kama una pesa (kama Dar) na nyingine ukiishi miaka inaongezeka kama una pesa, kama lushoto.
   
Loading...