Wanaume wa Dar bana!

Wanaume wa Dar bana!

Misimu ya baridi mitaro hufanyiwa isafi Sana elewa "mitaro"
 
Uzuri ni kwamba nilioga jana usiku 😁

2019 nimeishi Njombe
2022 nimeishi Songea

Sasa inatakiwa tuishi kwa mazingira dar kuna baridi kali leo sijaoga asubuhi imenibidi nitumie perfyum
Songea kuna baridi?
 
Wiki iliyopita tulienda Moro tukakuta wanachoma mahindi tukaomba pilipili na ndimu acha wacheke eti "nyie wa Dar eeh, huku hatutumii hivyo vitu mahindi yetu ni fresh kutoka shamba" tukala tu kinyonge lakini hatukuenjoy
Hamkuenjoy ni kwa sababu hamjazoea mimi mhindi uwe fresh usiwe fresh sitiagi chochote🤣
Wengine wanatia ndimu sasa hiyo ni kachumbari ama😂
 
Tangu nimefika Dar angalau sasa hivi ndio naona kuna hali nzuri ya hewa ambapo ninaweza hata nikavaa shati ya mikono mirefu.

Angalau sasa hivi hata matumizi ya feni yamepungua na bill ya umeme nayo imepungua.

Angalau sasa hivi ninaweza kujifunika shuka usiku nikilala, hapo awali sikuwahi kujifunika shuka usiku.

Angalau sasa hivi hata nikipanda mwendokasi sikutani na harufu za ajabu ajabu za watu wanaonuka jasho sababu ya joto.

Kwa ufupi tu hii hali ya hewa ya Dar kwa sasa ndio inafaa kwa mtu kma mimi.

Na hakuna baridi, bali kuna kaupepo tu fulani amazing ambako ndio kanafanya watu wavae masweta hasubui.
 
Back
Top Bottom