Upendo iswa
JF-Expert Member
- Aug 28, 2018
- 375
- 620
Dar es Salaam kwa sasa ni jiji lenye idadi kubwa sana ya watu lakini lenye eneo dogo kijiografia. Hali hii imesababisha msongamano mkubwa wa watu, makazi holela, shinikizo kwenye miundombinu, huduma za jamii na mazingira.
Kwa mtazamo wa Regional Development Planning, hali hii inaonesha wazi kutokuwiana kati ya population growth na spatial capacity ya jiji.
Tatizo Kuu
Dar es Salaam inaendelea kukua kwa kasi lakini imebanwa na mipaka midogo ya kiutawala. Urban growth imevuka mipaka ya Dar na kuingia maeneo ya Kibaha, Chalinze, Bagamoyo, Kisarawe na Mkuranga.
Ukuaji huu unatokea bila mfumo mmoja wa pamoja wa upangaji (integrated planning). Hii ni hali inayoitwa conurbation au urban spillover.
Pendekezo la Kitaalamu
1️. Upanuzi wa Jiji la Dar es Salaam. Ishauriwe Serikali:
Kupanua mipaka ya Dar es Salaam ili kujumuisha:
Kibaha
Chalinze
Bagamoyo
Kisarawe
Mkuranga
Hii itaunda Mega-Dar Metropolitan Region itakayopangwa kama eneo moja la kiuchumi, kijamii na kimuundombinu.
2️. Uundwaji wa Mkoa Mpya Kusini mwa Pwani
Rufiji
Kibiti
Mafia
Maeneo haya yaunganishwe kuunda mkoa mpya. Kuwe na makao makuu mapya ya mkoa
Kukuza regional balance na kuondoa mzigo wa Dar. Kukuza fursa za kilimo, utalii na uchumi wa bahari
Faida za Pendekezo
- Kupunguza msongamano wa watu Dar es Salaam
-Kuwezesha upangaji shirikishi (integrated urban & regional planning)
-Kuboresha utoaji wa huduma za jamii
-Kudhibiti makazi holela
-Kukuza uchumi wa kikanda kwa usawa
- Kulingana na mwelekeo wa miji mikubwa duniani (Mega City Regions)
Hitimisho
Kwa kuzingatia kasi ya urbanization nchini, hasa katika ukanda wa Dar es Salaam – Pwani, kuna haja ya mabadiliko ya kimkakati ya mipaka ya kiutawala.
Pendekezo hili linaendana na misingi ya Regional Development Planning, na linaweza kuwa suluhisho la muda mrefu kwa changamoto za mji wa Dar es Salaam na maendeleo ya maeneo ya jirani.