Wanaume tuoneeni huruma dada/mama zenu

Wanaume tuoneeni huruma dada/mama zenu

We dada ningekuona ningekwambia uache kulilia maziwa yaliyomwagika. Ukijikuta kwenye hali kama hiyo kitu cha kwanza unajisamehe upuuzi uliofanya kisha unajipanga kuanza kutembea njia mpya. Usitafute tu mtu wa kumlaumu kana kwamba wewe hukuvurunda. Huyo mwanaume msamehe, muache aendelee na maisha yake. Ukikaa kumfikiria utakuwa unapalilia hasira, uchungu na kinyongo. Mhanga wa kwanza wa hicho kisirani ni mtoto wako. Mzazi mwenye mizigo moyoni hawezi kutoa nuru kwa mwanae. Kwa faida yako na mtoto wako kubali kuwa mko wawili ujipange ufurahie maisha.

Unaweza usielewe nikikwambia ushukuru huyo mwanaume kaondoka. Watu wengine wanakuja kwenye maisha yetu kwa kusudi fulani na kuondoka. Utakuja kuelewa baadae sana kwa nini hili limetokea hivi kama tu utatulia. Ingawa Obama hakukataliwa na babake, kutengana na baba yake na kulelewa marekani na mama na bibi zake ndo kulimpeleka kuwa Rais wa kihistoria Marekani. Baba yake aliporudi Kenya aliishia kwenye ulevi na baadae kufa. Sasa angekuwa amerudi Kenya na Barak sidhani kama Barak wa leo angekuwa hata mwenyekiti wa serikali ya mtaa huko Kenya. Hata huyo Diamond sidhani kama baba yake angekubali bibi Sandra kumpeleka diamond kwenye matamasha na mashindano ya muziki usiku.

Mifano ya watu waliotelekezwa na wazazi na kutelekezwa kwao kukawa ndo njia ya mafanikio ni wengi. Tanzania wapo na dunia nzima. Kuwa single parent mwenye matumaini na bidii kama mama wa Dr Ben Carsons. Badala ya kuwaza mwanaume aliyekuacha waza utakavyomtoa mwanao. Huyu mama katika umaskini wake aliweza kutoa mtoto mcha Mungu, mnyenyekevu, mwenye bidii, daktari bingwa duniani wa upasuaji wa mishipa ya fahamu na vingine ongezea.

Kuna baba anaitwa Chris Gardner ambaye kisa chake kilitengeneza movie ya "pursuit of happyness". Huyu alitelekezwa na baba yake na akanyanyaswa na baba wa kambo, na yeye akaja kuzaa kabla ya ndoa na akaachiwa mtoto wa chini ya miaka miwili akiwa hana ajira. Alikataa kulaumu kama wewe. Akakomaa na mwanae - kulala nae kwenye magari mabovu, stendi, kanisani mpaka kikaja kueleweka. Ni milionea aliyeacha biashara na sasa anazunguka dunia kuwatia moyo watu kama wewe na wanaume wanaokimbia watoto. Maisha yale yale ya kutelekezwa ndo yalimfanya akawa baba bora na mmoja wa wanaume waliofanikiwa duniani. Kwa hiyo kukata tamaa au kuvaa ujasiri na kufurahia au kuombelezea hayo maisha yako mapya ni chaguo lako. Amua unataka nini. Mungu huwa si mchoyo. Ukivurunda ukakubali na kumrudia anakupa nafasi ya pili na ya tatu na ya nne.

Thank you.
 
Wale Sauti Sol wa Kenya hawakataagi mtoto hata Nerea walimsisitiza awapelekee mtoto wao watamlea..labda jaribu kwao ila hawa wa kibongo ni Pasua kichwa dadangu.

Ila kwa jinsi ninavyotafuta mtoto kwa gharama yeyote..huyo mwanamke atakenizalia si nitamkopea mkopo wa Saccos hapa wizarani ale na mwanangu na apumzike na uchovu wa uzazi..yani ndo maternity leaves yake hiyo..!

Afu napendaga wanawake wenye watoto....they are very easy to start a relationshio with them..yaani hapa nikianza kumcare na kumpenda mtoto kwa kiwango cha dunia basi automatically na mama yake ananipenda and voila! Abracadabra!

Anyways!! Sorry can I adopt her Mzigua90?

Karibu tulee baba mlezi.
 
Nakubaliana na ww 100%, lilishawahi kunitokea, mwanamke niliekuwa nae kwenye mahusiano bahati mbaya alipata ujauzito wang, nikakubali kugharamia ujauzito mpaka anajifungua mwaka 2002 kila mwezi nilikuwa natoa tshs50, 000/=, baada ya kujifungua ndo mtihani ulipoanza, ukituma tshs100, 000/= baada ya siku tatu unaambiwa hela imeisha, ukihoji imetumika vp anakuwa mkali kwelikweli, ukumbuke mwaka 2003 tshs100, 000/= ilikuwa ni pesa kubwa unaweza nunua kiwanja au shamba, ikafikia kipindi nikamwambia siwezi ongeza pesaila nitatuma hiyohiyo tshs 100,000/= mungu wangu nilichambwa balaa, "kati ya wanaume na ww unajiona mwanaume? kwanza mtoto sio wako", hiyo kauli iliniuma nikaamua kusitisha utoaji wa pesa, ndo matusi yakazidi mi kimyaa sijibu chochote, ikapita miaka10 nikapata taarifa kuwa mwanao anapata shida sana kijijini analima vibarua ndo apate kula, dah roho ikaniuma sana nikajiuliza mmm niko dsm nafanya kazi, naishi vizuri, nakula vizuri naishi kwangu inakuwaje mwanangu apate shida? nikalianzisha sekeseke la kudai mtoto lakini mama mtoto mkali balaa, nikapiga mkwara kama ni mwanangu kweli namhitaji vinginevyo akipata tatizo usinihusishe kwa lolote, akakaa akajifikiria mwisho akasema tuma nauri nikuletee mwanao, nikatuma tshs80000/=toka iringa kuja dsm lakini nayo ikaliwa, nikatulia kimya kama miezi miwili akanitafuta na kunieleza kuwa ile pesa ilitumika kumtibu mama yake kwa hiyo anaomba samahani, nikatuma tena tshs80, 000/=akasafirishwa kijana hadi dsm mpaka ss niko nae home anaendelea na masomo, mida mingine huwa tunavumilia mengi ila baadhi ya wanawake huwa wanajiwahi kulaumu tu bila kujua kuwa chanzo cha matatizo mengine husababisha wao.

Pole mkuu. Huyo mwanamke alikua hajielewi.
 
ulivyonijibu kiustaarabu, naomba tu niseme pole na samahani. anyway, unaonekana ni mtu mstaarabu, nilikuwa nakubip ili nikusome picha wewe ni mtu wa aina gani, ulionewa au ulionea...nimepata jibu wewe ni mtu mtaarabu na huyo jamaa anatakiwa kutunza mtoto. nakuheshimu.

Mimi sio tu mstaarabu mkuu, huwa sipendi kusumbuana na watu. Ndio maana natafuta sehemu kama huku nakuja kutoa machungu yangu. Huwa namaliza hasira zangu zaidi kwa kulia. Sipendi vurugu na watu kabisa yani.
 
Nawezaje kumuomba baba wa mtoto anisaidie?

Kumbe alianza siku nyingi inawezekana ulimuibia mwanamke mwenzio i.e. ulikua Mchepuko

Pole sana, swala kumkimbia mtoto sio zuri, jipe moyo kuna siku atarudi kuomba msamaha.

Wakati tunaanza alinipa story za uongo kabisa kuhusu uhusiano wake uliopita. Ila baada ya kubeba ujauzito ndio nilimjua vizuri hasa baada ya kunisisitiza nitoe. Alikua na mwanamke mwingine ndo maana alisisitiza nitoe na hata sasa hivi hataki kunisaidia sababu huyo mwanamke ameshaujua ukweli kuwa mwanaume wake amezaa nje. Ila hata kama angekua na ndoa bado ni makosa yake kunidanganya alee mtoto.
 
Haya mambo si rahisi kama tunavyofikiri. Wanawake ni pasua kichwa anakueleza kuwa wewe achana na Mtoto wangu nitamlea hata kwa kuuza k sishindwi. Baadaye anaanza kulalamika! Hakuna Mwanaume anamtupa mtoto wake bila kuchoshwa na kejeli za mama yake. Hii inawahusu wanawake wa Tanga Mzigua90

Labda wanawake wa Tanga wako hivyo. Ila kwa uelewa wangu wanawake wengi wa Tanga huwa wanyeyekevu sana kwa wanaume wao yani mpaka ikatokea akakujibu hivyo jua umemtesa vya kutosha. Mimi sifa yangu kubwa ni kutokusumbuana na mwanaume. Ila kwa baby dady nilivumilia karibia mwaka mzima kwa kuamini atachange. Mpaka nimemtamkia nitamwambia mtoto baba yake alikufa ni kwa sababu niliona hakuna matumaini tena ya baba mtoto kuwa baba wa mwanangu. Nimevumilia mwaka mzima hoping that he will change his mind.
 
Tatizo mnapopenda mnashindwa kuwafanyia tathmini wanaume mlio nao kwenye mahusiano. Matokeo yake ndo hayo. Huenda ulikunwa vizuri ukaongeza kupanua mapaja hilo likakunyima muda wa kumtathimini mwanaume. Ila pole kila lolote likitokea ni sehemu ya funzo.

Na kweli nimejifunza.
 
Kwani mlikubaliana kuzaa au uliitegesha tu kwa sababu anajiweza ?

2.Kulikua na mpango wowote Wa jinsi ya kupeana matunzo au ndio umetuletea shemeji zako labda tutalitatua?

3.Pole sana mahusiano ni magumu sana ila wanaume tujitahidi hata kama humtaki Mama basi mtoto mjali maana anaathirika kisaikolojia.

Hatukua na mpango wowote na tulikua tunatumia kinga siku zote ila ikaishia kama hivyo.
Sielewi kama tulikua hatuna mpango ndo nilitakiwa kutoa?

Mpango wa kupeana matunzo ulikuwepo ila toka uongelewe hakuwahi kutuma hata elfu kumi.

Asante.
 
Nikiwa kama mhanga wa mwanamke alieachiwa matunzo ya mtoto bila msaada wa baba naumia sana.
Hivi wanaume huwa mnawaza nini mnapotupa adhabu ya kulea watoto peke yetu na wewe baba ukiwa hai na unajiweza? Hata kama hujiwezi basi kumjali mtoto wako japo kwa kuulizia maendeleo yake mtu anashindwa kabisa. Hivi kina kaka mmejiuliza nyie baba zenu wangewakimbia mngekuwa wapi sasa hivi? Mnajua ni chuki gani mnaweka kwa watoto wenu mliowakataa? Mnajua ni laana gani mnapata kwa Mungu kwa kukataa kutimiza wajibu wenu kama wazazi? Au mnatukomoa kwa sababu mama hawezi kumuacha mtoto wake nyuma hata apate tatizo gani? Labda wewe na mama wa mtoto hamko sawa lakini ile hasira ya ninyi kutokua sawa baba usimkomeshe mama kwa kuacha kumtunza mwanao ukijua unamkomoa mama, pale unaemkomoa ni mtoto wako ambae ulimtafuta kwa mapenzi/tamaa zako mwenyewe.
Naandika nikiwa na uchungu mwingi sana moyoni. Mwanaume usiemtunza mwanao ona aibu na muogope Mungu wako kwa kitendo unachokifanya.
Jiulize ingekua ni dada yako au mwanao ameachwa na mwanaume alee mtoto peke yake ungejisikiaje?
KARMA IS A BITCH. Ukinifanyia mimi leo wakati unao dada na watoto wa kike jua itakuumiza na wew kwa mmoja kati ya hao kufanyiwa kama unavyofanyia wengine.
Baba mtoto wangu nimeshamlilia Mungu juu yako na nina hakika huyu mtoto ulieniachia nimlee peke yangu atanifuta machozi siku moja na utatamani akutambue kama baba yake utakua umeshachelewa.
Kaka/baba zangu baba Diamond akawe mfano kwenu, Obama aliekataliwa na baba yake mwishoni alikuja kuwa Rais wa marekani/dunia.
Point of collection Obama hakukataliwa na baba yake, KOMA
 
Wanaume wengi wanatabia za jogoo mzigo wakulea watoto huachia mwanamke poleni muwemakini halafu muache tabia ya kuwa ongezea umasikini wazazi wenu vijijini kwakuwarundikia wajukuu nyie mkindelea kutafuta wengine
 
Maskini! Maandishi yako yameprovoke huruma yangu ya ndani kiaina.

Yaani mpaka nimefeeel your nagging pain and suffering. Vumilia!! Mungu akifunga mlango mmoja wa bahati basi huwa anafungua mingine kadhaa.

I'm very sorry Mzigua90

Thanks my dear. Naamini Mungu hamtupi mja wake. Naamini hawezi kuniacha na mimi pia.
 
Wewe wajiweza kiuchumi?? Kama ungelikuwa unajiweza kiuchumi usingelikuja na kilio kikali kihivyo. Tulia tu dada, wanaume kwa hasira hufanya upuuzi baadaye wakapata akili wakageukza hasira. Endapo akijua umekuja jf ataongeza umbali uliopo.
Kaeni chini myazungumze. Hiyo hela ya kuitoa hiyo mimba alikupa ukala au?? Huenda ulimwambia umeitoa, halaf akashtukia tena unamwambia bado ipo.
Sifurahii kutoa mimba wala siungi mkono ila kama alifikia hilo, kuna sababu na sababu kama haijatolewa, hamtaelewana. Akimwona huyo malaika, damu zinamsisimka kwani anajiona kuwa tiyari alishamhukumu kifo mtoto.

Nilimwambia siwez kutoa mimba na nikamwambia sijaitoa. Alishamuona mtoto tayari na ndio kuanzia hapo aliseme atasaidia kulea ila mambo yakawa tofauti.
 
Wanaume akili zao wanazijua wnyw..muhimu pambana lea mwanao .....ktk maadili...apate elimu yA kutosha...huyo baba achana nae....ukilialia sana anafurahia....Kama kakataa tupa kuree ng'ombe haelemewi nA nundu yke bana!!
Atupe nini mama
 
Back
Top Bottom