Wanaume tuoneeni huruma dada/mama zenu

Wanaume tuoneeni huruma dada/mama zenu

d5e8bf458e6339c1328c949d072ff107.jpg

Katika mazingira kama haya unampendaje mtoto wako?
Rashid ni rafik yangu aliyenipa taarifa za kujifungua kwake
Wanawake hasa wenye ajira wana matatizo sana
 
Inavyoonyesha ulimtesa sana huyo mwanaume just imagine unafikia wakati kumweleza mtoto kuwa baba yake alikufa! Jirekebishe

Acha kuhukumu usichokijua. Namtesa ulikuwepo? Hata kama nilimtesa kwani si mimi ndio nilimtesa mtoto anahusika nini?
Kwa mambo aliyonifanyia baba yake ni bora asingekuwepo ningemuelewa.
 
Na sisi wadada tusigawe uchi kwa kutegemea kuolewa ama jifunze kujua siku upo mwezini,ni sayansi ndogo ukishindwa tumia Kondom,zipo za kike na za kiume!

Unadhani ckuyajua yote hayo? kama ingekua ni kutegesha mimba ili kupata kitu nisingeweza kufanya hivyo kwa huyu baba wa mtoto. Mbona nilishakua na wanaume before yeye, tena niliwapenda na wanajiweza kuliko yeye. Nishindwe kutegesha kwao nitegeshe kwake? Labda kuna wanawake wana ujinga huo ila sikuwahi kuwaza kufanya kitu kama cha kubeba mimba ili kumkeep mwanaume Never. Sababu hata nilivyobeba ujauzito niligundua huyu mwanaume ana mwanamke mwingine mbona sikutoa kama lengo langu lilikua kumkeep?. Nimelea mimba toka siku ya kwanza mpaka naenda labour hajawahi hata kunipigia cmu naendeleaje mbona sikutoa mimba? Msipende kugenerelize vitu.
 
Huyu mtoa mada ni wale wale. Siamini mwanaume anaweza kuitelekeza sperm yake bila maudhi Na kashfa SA wewe si saizi yangu. Una kibamia ambacho hakiwezi kunizalisha etc. Sasa kaishasahau na mashambulizi kwa wingi Mzigua90

Sijawahi kumdharau mwanaume kwa maumbile yake. Inaonekana mnakutanaga na wanawake wanaowaambiaga mambo mabaya sana. Sasa huyu ndio kaikataa damu yake tena kamwambia huyo mwanamke wake mtoto sio wa kwake yeye ananisaidia tu kulea kwa sababu baba wa mtoto alinikimbia.
 
WANAWAKE WANA MATATIZO SANA

wakati nakuwa nilikuta wazazi wangu wametangana
Nikapata malezi ya upande mmoja ambayo ni ya mama
Kwa kiasi flani mama alijaribu kunijengea chuki dhidi ya baba.........
Na kweli alifanikiwa nilimchukia sana baba
Nikajiapiza katika maisha yangu sitakuja kuruhusu mwanangu apitie maisha niliyopitia........
Mwaka jana mwezi wa nne nilifanikiwa kumpatia ujauzito mwanamke ambaye nimedumu nae katika mahusiano kwa zaidi ya miaka mitano na niliamini ange kuwa mke wangu siku moja
Mkasa ukaanza wakati wa huo ujauzito nimetukanwa matusi ambayo sikuwahi kutukanwa kabla na sitakuja kutukanwa tena
Wazee wakaniambia yamkini mimba yake imekuchukia ishi nae kwa umakini sana............
To shorten story jana kanizalia mtoto wa kiume lakin sina hamu ya kumuona huyo mtoto sina mapenz nae amenitoka moyoni kutokana na maneno machafu ya mama yake
Nilipopata taarifa kajifungua nikamtext kumpa hongera lakin jibu nililopewa lilifanya niamini kile nilichokuwa nakiamini enzi akiwa mjamzito
NB; Nilijitahid kumsupport financially licha sikuwa nikiishi nae

Kila binadamu ana tabia zake mkuu. Sio wanawake wote wananyanyasa wanaume na sio wanaume wote wanakimbia watoto.
 
Nikiwa kama mhanga wa mwanamke alieachiwa matunzo ya mtoto bila msaada wa baba naumia sana.
Hivi wanaume huwa mnawaza nini mnapotupa adhabu ya kulea watoto peke yetu na wewe baba ukiwa hai na unajiweza? Hata kama hujiwezi basi kumjali mtoto wako japo kwa kuulizia maendeleo yake mtu anashindwa kabisa. Hivi kina kaka mmejiuliza nyie baba zenu wangewakimbia mngekuwa wapi sasa hivi? Mnajua ni chuki gani mnaweka kwa watoto wenu mliowakataa? Mnajua ni laana gani mnapata kwa Mungu kwa kukataa kutimiza wajibu wenu kama wazazi? Au mnatukomoa kwa sababu mama hawezi kumuacha mtoto wake nyuma hata apate tatizo gani? Labda wewe na mama wa mtoto hamko sawa lakini ile hasira ya ninyi kutokua sawa baba usimkomeshe mama kwa kuacha kumtunza mwanao ukijua unamkomoa mama, pale unaemkomoa ni mtoto wako ambae ulimtafuta kwa mapenzi/tamaa zako mwenyewe.
Naandika nikiwa na uchungu mwingi sana moyoni. Mwanaume usiemtunza mwanao ona aibu na muogope Mungu wako kwa kitendo unachokifanya.
Jiulize ingekua ni dada yako au mwanao ameachwa na mwanaume alee mtoto peke yake ungejisikiaje?
KARMA IS A BITCH. Ukinifanyia mimi leo wakati unao dada na watoto wa kike jua itakuumiza na wew kwa mmoja kati ya hao kufanyiwa kama unavyofanyia wengine.
Baba mtoto wangu nimeshamlilia Mungu juu yako na nina hakika huyu mtoto ulieniachia nimlee peke yangu atanifuta machozi siku moja na utatamani akutambue kama baba yake utakua umeshachelewa.
Kaka/baba zangu baba Diamond akawe mfano kwenu, Obama aliekataliwa na baba yake mwishoni alikuja kuwa Rais wa marekani/dunia.

nikuchane au sikuchane.tatizo ninyi wenywe wadada mkishazaa basi mnataka mpandia mtu mezani akichelwa kurudi home umepiga simu sms aijajibiwa mumeo akirudi badala ya kuuliza kulikoni unaanzisha kasheshe usiku kucha.matusi vurugu yani balaa.kwa uchache ni pm nikupe maneno musharabu
 
Mamy Pole sana, najua unaumia kiasi gani kwsbb viatu hivyo nilishavaa pia. Mungu ni mwema atakufuta machozi siku moja.
 
Hofu yangu siku hizi hata wanawake mnatubebesha mizigo zisizo zetu. Muweni waaminifu kwanza then ndo mtubebeshe hizo lawama.
 
Tatizo wadada jeuri mmezidi hamchagui lakumwambia mwanaume pia punguzeni kubambikia watoto wababa kwa tamaa ya fedha
Isitoshe mpo kimaslahi zaidi kuliko mapenzi na mkitendwa mnakasirika sana ila tamaa y Mali inawamaliza aisee,
Mwisho wa siku mtoto ni wa mama so muwathamini wasaidizi wenu wawalelee watoto kwani hatuna uhakika wa asilimia mia kuwa ni watoto wetu
 
Makosa yanaweza kuwa ya mwanamke,mwanaume au wote wawili lakini athari kubwa inakuja kwa mwanamke na mtoto..So wadada muwe makini..Sio kila mlowekaji ni mfuaji..Wengine wanaloweka tu na kuendelea na shughuli zao..
Kaboom katika ubora wako. Umesema vizuri sana.
 
Mimi sio tu mstaarabu mkuu, huwa sipendi kusumbuana na watu. Ndio maana natafuta sehemu kama huku nakuja kutoa machungu yangu. Huwa namaliza hasira zangu zaidi kwa kulia. Sipendi vurugu na watu kabisa yani.
nimekupenda bure. ila badilisha avatar.
 
Wakikua watantafuta ndo msemo wa wengi
**sina mtt wa nje na sitarajii
We Pole ndo inakufaa
 
kwani Magu anaifahamu hii sikukuu? napika pilau kwenye sikukuu zinazofahamika na Magu only.
Anaitambua ndo mana watumishi wake hawajaenda makazini..Haya kanunue Mchele fasta
 
Mimi nawalaumu wanawake katika hilo tu, they are in control of their bodies, wanajua lini wapo safe, lini wanaweza kujiachia, wanaweza kuamua huyu nimpe coz anafaa, huyu hanifai hivyo he won't test my bits.

Ninachoshindwa kuelewa, kwa nini(pamoja na kuwa na full control ya miili yao), kwa nini mtu anabeba mimba ya mtu asiyeonyesha kuwa nae, kwa nini wanategesha mimba? Hiyo weakness kwa dada zetu inawatafuna, wanapata mzigo wa kulea watoto peke yao...so sad!...

Lakini pamoja na hayo, mwanaume kumuachia mwenzako majukumu ya malezi no dhambi kubwa!!
That's it, that's it Brother
What you said is absolutely the truth, women should take this into account ......
 
Back
Top Bottom