Nakubaliana na ww 100%, lilishawahi kunitokea, mwanamke niliekuwa nae kwenye mahusiano bahati mbaya alipata ujauzito wang, nikakubali kugharamia ujauzito mpaka anajifungua mwaka 2002 kila mwezi nilikuwa natoa tshs50, 000/=, baada ya kujifungua ndo mtihani ulipoanza, ukituma tshs100, 000/= baada ya siku tatu unaambiwa hela imeisha, ukihoji imetumika vp anakuwa mkali kwelikweli, ukumbuke mwaka 2003 tshs100, 000/= ilikuwa ni pesa kubwa unaweza nunua kiwanja au shamba, ikafikia kipindi nikamwambia siwezi ongeza pesaila nitatuma hiyohiyo tshs 100,000/= mungu wangu nilichambwa balaa, "kati ya wanaume na ww unajiona mwanaume? kwanza mtoto sio wako", hiyo kauli iliniuma nikaamua kusitisha utoaji wa pesa, ndo matusi yakazidi mi kimyaa sijibu chochote, ikapita miaka10 nikapata taarifa kuwa mwanao anapata shida sana kijijini analima vibarua ndo apate kula, dah roho ikaniuma sana nikajiuliza mmm niko dsm nafanya kazi, naishi vizuri, nakula vizuri naishi kwangu inakuwaje mwanangu apate shida? nikalianzisha sekeseke la kudai mtoto lakini mama mtoto mkali balaa, nikapiga mkwara kama ni mwanangu kweli namhitaji vinginevyo akipata tatizo usinihusishe kwa lolote, akakaa akajifikiria mwisho akasema tuma nauri nikuletee mwanao, nikatuma tshs80000/=toka iringa kuja dsm lakini nayo ikaliwa, nikatulia kimya kama miezi miwili akanitafuta na kunieleza kuwa ile pesa ilitumika kumtibu mama yake kwa hiyo anaomba samahani, nikatuma tena tshs80, 000/=akasafirishwa kijana hadi dsm mpaka ss niko nae home anaendelea na masomo, mida mingine huwa tunavumilia mengi ila baadhi ya wanawake huwa wanajiwahi kulaumu tu bila kujua kuwa chanzo cha matatizo mengine husababisha wao.