wanawake wengi tunaachia tupate mimba kwa sababu mbalimbali.wengi tunategesha mimba ili kuolewa,wengine tunategesha kwa mwanaume wenye hela tukidhan kuwa nikizaa nae ndo nitakula hela yake vizur.wengine umri umeenda anaamua kuzaa na mwanaume yeyote ilimradi naye apate mtoto wake.kwa wale waopata mimba kwa bila malengo wengi wao huwa niwale wanafunzi wenye umri mdogo ambao hawajui kujikinga.migogoro yote ya kuachiwa mtoto inatokea baada ya malengo ya kupata mimba hiyo kutotimia.wanaume wengi wanapenda raha ya kavukavu lakini wakisikia mimba kwaheri,wako radhi wamchukue mtoto akalelewe na mkewe au mama yake kuliko kumpa mtu aliye zaa nae hela ya matunzo kwa kuwa anajua akitoa hiyo hela na wewe mama mtu utakula hiyo hiyo.jambo lingine kunawanaume wengine wako tayar kuhudumia lakini hayo matumizi yanayoomba kwa ajili ya mtoto ni makumbwa kuliko hata matumizi ya nyumbani kwake na familia yake yenye idadi kubwa ya watu,yaani tunakuwa kama tunawakomesha wanaume kwa kudai matumizi makubwa mwisho wake wanaamua kukimbia au kukana watoto.tujirekebishe tukijiachia kupata mimba tujiandae na kulea na kumtunza mtoto.tusifanye mtoto kama kitega uchumi.hii itatusaidia kupunguza strees,nakuishi kwa amani.