Hayo ni mawazo yako mkuu. Kama angekua kitega uchumi ningeanza nae kwenye mimba. Toka nimepata ujauzito hela pekee aliyonipa ni hela ya kwenda kutolea mimba. Na kuna kipindi nilikua sina hata 100 ila sikuwahi kumuomba hela hata ya kwenda clinic. Hata Mungu ni shahidi kama nilishawaza nitaishi kupitia hela za huyu mtoto. Bora angekua ananipa hata kipindi hicho angesema basi nilizuzuka na hela zake ila sikuwahi kuzuzuka nae. Na hata huu ujauzito niliupata kimaajabu tu.
Wewe wajiweza kiuchumi?? Kama ungelikuwa unajiweza kiuchumi usingelikuja na kilio kikali kihivyo. Tulia tu dada, wanaume kwa hasira hufanya upuuzi baadaye wakapata akili wakageukza hasira. Endapo akijua umekuja jf ataongeza umbali uliopo.
Kaeni chini myazungumze. Hiyo hela ya kuitoa hiyo mimba alikupa ukala au?? Huenda ulimwambia umeitoa, halaf akashtukia tena unamwambia bado ipo.
Sifurahii kutoa mimba wala siungi mkono ila kama alifikia hilo, kuna sababu na sababu kama haijatolewa, hamtaelewana. Akimwona huyo malaika, damu zinamsisimka kwani anajiona kuwa tiyari alishamhukumu kifo mtoto.