Wanaume tuoneeni huruma dada/mama zenu

Wanaume tuoneeni huruma dada/mama zenu

alishindwa kukuhudumia ukiwa peke yako ukamlegezea magoti atawezaje kukuhudumia mkiwa wawil?
 
Jieleze vizuri kwa nn amekukimbia, sio unakuja kulaumu hapa, wewe ulifikiri kuwa na mtoto wake ndo iwe kigezo cha kuto kukupiga chini!
wanawake wengi mkishazaa tu, mnaanza kujionyesha tabia zenu halisi, mwanaume anakuvumilia hubadiliki anakupiga chini. Ili ulee mwenyewe. Hata kama una mtoto naye, utiifu wa mapenzi kwa mwenzio ni muhimu. Au ulifikiri mtoto wake kwako umeweka kitegauchumi bila mapenzi?

Sijaongelewa kukimbiwa chief. Nimeongelea kulea mtoto. Hata ningekua malaya, mkorofi na kilq kitu kibaya bado siyo sababu ya mtu kukataa kulea mtoto wake. Ananikomoa mimi na tabia zangu au anamkomoa mtoto?
 
Mwanamke unatakiwa uwe smart pia, usichukue mimba huku ukiwa unamtegemea mtu asiyeeleweka na sio mume... au kuwa na kazi ya kukupa kipato cha kumtunza mwanao kabla ya kuchukua mimba nje ya ndoa.. japo wanaume wana makosa ila mnaweza kupunguza extent ya watoto kulelewa kwenye umasikini kwa kuwa makini
Hakuna umasikini hatari kama ule wa kukosa upendo toka kwa mzazi wako, ni umasikini mbaya sana kuliko hata kulala njaa au kula jalalani ni umasikini unaojenga chuki na visasi vya moyo! Wanaume wenye tabia hizo hebu wamuogope Mungu
 
ilikuwaje akakuachia watoto, mlioana kwa ndoa? kama jibu ni ndio basi ujilaumu kwa kutotunza ndoa hadi mkaachana. kama haukuoana naye kwa ndoa, jilaumu kwa kuwa malaya kuvua chupi ovyo hadi jamaa kakuzalisha na kukudampu akaenda kuoa ampendaye. ilaani ile siku umevua pichu na sio kuwalaani na kuwachukia wanaume.tatizo wadada mmezidi umalaya na kuchagua chagua, nataka kila mwanaume mnayemtamani awaingilie, na kwa jinsi sisi wanaume tulivyo, mwanamke mrahisi huwa tunamtumia kwa starehe tu ila sio wa kudumu naye kwasababu tunajiuliza amekuwa mrahisi kwangu hivi atakuwa mrahisi au amekuwa mrahisi kwa wangapi. hivyo punguza umalaya uache kulalamika. utamu uliutaka mwenyewe hayo ndo matunda yake uyale sasa.

Labda ni kweli tuliozaa kabla ya ndoa sisi ni malaya ila basi hata uliolala nao kabla ya nsoa ni malaya vile vile na wew pia upo kundi hilo la hao malaya.
 
mwanaume akitaka kuzaa na wewe atakwambia tuu.na mtapanga pamoja suala hilo lakini ukiamua mwenyewe mwanamke ujue hilo lako.usilaumu mtu we lea
Dada sijui binti; mwanaume wa wewe na yeye kupanga kuhusu mtoto, awe ni mume wako tu wa ndoa, kama atawatelekeza na watoto wake wa ndoani, basi sawa. Lakini boyfriend, sijui mchumba ambaye kashakutolea mahari, sijui mchumba sugu; beba tu mimba at your own risk. Watu wanatelekezwa na matumbo yao na vikao vya harusi vishaanza. Wavulana wa sasa hivi, wanapenda hao kuitwa "baba", ila kulea sasa weeeh. Atakavyokubembeleza ubebe mimba, siku atakavyokukana hutoamini mijicho yako.
 
Mzigua mwenzangu pole sana!
Lea mwanao, Mungu atakupa wepesi!
Kama baba yake hamjali basi hata mimi baba yake wa kambo nitampa mapenzi Kama sio mahaba!!

Asante mzigua mwenzangu. Karibu baba wa kambo.
 
Mahusiano ya kimapenzi yakivunjika ujue mwanamke ndiyo tatizo. imeandikwa "mwanamke mpumbavu huivunja ndoa kwa mikono yake mwenyewe"

hii ndiyo kusema kuwa, kama mwanamke umesimama imara hata mwanaume awe chizi kiasi gani atapoa tu.

shida wadada wa siku hz mnadhani kukata mauno, kubugia dushelele na kugawa 071..ndiyo mapenzi. damn shit!!
Mmh! Usijumuishe kiivyo.
 
Wale Sauti Sol wa Kenya hawakataagi mtoto hata Nerea walimsisitiza awapelekee mtoto wao watamlea..labda jaribu kwao ila hawa wa kibongo ni Pasua kichwa dadangu.

Ila kwa jinsi ninavyotafuta mtoto kwa gharama yeyote..huyo mwanamke atakenizalia si nitamkopea mkopo wa Saccos hapa wizarani ale na mwanangu na apumzike na uchovu wa uzazi..yani ndo maternity leaves yake hiyo..!

Afu napendaga wanawake wenye watoto....they are very easy to start a relationshio with them..yaani hapa nikianza kumcare na kumpenda mtoto kwa kiwango cha dunia basi automatically na mama yake ananipenda and voila! Abracadabra!

Anyways!! Sorry can I adopt her Mzigua90?
 
Pole sana dada. Binafsi nimeshindwa kuelewa hawa jamaa wanakua na roho ngumu namna ngani. Sielewi kwa kwel. Namfahamu mmoja ameelimika kabisa - elimu ya chuo kikuu, na ana kazi serikalini lakini ndo hivyo, kamtelekeza mzazi mwenzake na mtoto.

Huyu wangu kaelimika zaidi nadhani. Kaishi kwenye nchi ambazo wanasheria kali za child support, ana maisha mazuri tu. Halafu kibaya zaidi yeye ndo alikuja na hizo mada za kusaidiana malezi akasema nimpe na amount ya matumizi kwa mwezi. Nilivyo loyal nikaamua tushee nusu kwa nusu. Na akakubali hela atakayokua anatoa yeye. Cha ajabu toka hapo akaanza kuleta visababu kwanini hatumi hela mwishoni akaamua kutopatikana kabisa. Na karudi Tanzania ila hata simu yake nikipiga hapokei. Yani bora angekua hatoi kitu sawa lakin anajali hata kuna mtoto wake.
 
Aisee hii ni sehemu ya matatizo ya kuwambia watu wafyatue tu pole dada angu nitunuku tu uyo mtoto nikusaidie kulea
 
Mwanaume mpaka afanye hivyo kwa kuuachia mtoto wake...basi ujue wewe ni tatizo...tatizo lilianza mwanzo ndio maana hakukuo...ila haujajifunza na kuendeleza ununda mpaka sasa kwenye malezi.
....acha kupiga mayowe-badilika kifikra....speaking from my experience

Ni kweli nilikua tatizo toka mwanzo sababu nilikataa kutoa mimba yake kwa kigezo kuwa sina kazi bado ikitokea yeye hayupo itakuaje kwahyo ni bora nitoe nibebe mimba yake wakati nitakapokua nimejipanga. Tatizo ndipo lilipoanzia hapo mkuu.
 
Hili suala la single parenthood linazidi kukua kwa kasi ya ajabu. Tusichokigundua ni kwamba we are raising a generation of young adults that will have so much insecurities kwa sababu ya kukataliwa na wazazi wao au kutokupata malezi ya wazazi wote wawili.

Natamani sana kila mmoja kwa wakati wake atafute movie inaitwa COURAGEOUS by Alex Kendrick , ina fundisho moja na muhimu sana kuhusu nafasi ya baba katika malezi ya wanaye. And this is not just for the single mothers out there, hii ni kwa ajili ya familia zote. Trust me you will learn something very valuable from watching this movie.
courageousartworkpic1.jpg

Nitaitafuta
 
bao la sponsor bna halitoagi kitu hata utege vipi ila kutana na sperm donor hata swimming pool utapata mimba eti
nipo poa mtu wangu

Hahahahahaa... ukweli mtupu. Yani kupata mimba ya sponsor huwa haitokei kirahisi rahisi. Ila hawa ndugu zetu sperm donor yani siku ukikosea kidogo ukauza mechi ujue ndo umejizika kwenye ubaby mama.
 
Pole sister! ila kuna kitu watu huwa hawatambui,wanaume huwa si wepesi wa kuongea yanayowasibu kwenye mahusiano ila wanaume wanateswa sana na wanawake japo siungi mkono tabia ya kukimbia familia ila kuna wanawake pasua kichwa aisee,nina jamaa yangu yeye toka ameoa ana miaka mitatu,mke hata wakizinguana kidogo anasepa kwao miezi 6 mpaka karibia mwaka.sasa saa hizi ana ujauzito huyo mdada baada ya kua akibeba unaaribika,alafu makosa yenyewe yanamtoa hom kwake ni makosa ya kawaida tu,kuna muda jamaa huwa anatamani hata amuache kabisa sasa hali hyo ikiendelea si ipo hatar ya jamaa kutelekeza mke na mtoto? sema wengi huwa mnatumia watoto kama mwavuli,ukisha kua na familia inabidi ujifunze kukaa vizuri na mwenzio kwa ajili ya ustawi wa familia,wanaume sio watu wa ku take action kirahisi ila akichukua hua aangalii side effect ya uamuzi anaochukua.Maudhi yakizidi familia huwa haina uzito sana hasa katika kuchukua uamuzi mgumu
Nakubaliana na ww 100%, lilishawahi kunitokea, mwanamke niliekuwa nae kwenye mahusiano bahati mbaya alipata ujauzito wang, nikakubali kugharamia ujauzito mpaka anajifungua mwaka 2002 kila mwezi nilikuwa natoa tshs50, 000/=, baada ya kujifungua ndo mtihani ulipoanza, ukituma tshs100, 000/= baada ya siku tatu unaambiwa hela imeisha, ukihoji imetumika vp anakuwa mkali kwelikweli, ukumbuke mwaka 2003 tshs100, 000/= ilikuwa ni pesa kubwa unaweza nunua kiwanja au shamba, ikafikia kipindi nikamwambia siwezi ongeza pesaila nitatuma hiyohiyo tshs 100,000/= mungu wangu nilichambwa balaa, "kati ya wanaume na ww unajiona mwanaume? kwanza mtoto sio wako", hiyo kauli iliniuma nikaamua kusitisha utoaji wa pesa, ndo matusi yakazidi mi kimyaa sijibu chochote, ikapita miaka10 nikapata taarifa kuwa mwanao anapata shida sana kijijini analima vibarua ndo apate kula, dah roho ikaniuma sana nikajiuliza mmm niko dsm nafanya kazi, naishi vizuri, nakula vizuri naishi kwangu inakuwaje mwanangu apate shida? nikalianzisha sekeseke la kudai mtoto lakini mama mtoto mkali balaa, nikapiga mkwara kama ni mwanangu kweli namhitaji vinginevyo akipata tatizo usinihusishe kwa lolote, akakaa akajifikiria mwisho akasema tuma nauri nikuletee mwanao, nikatuma tshs80000/=toka iringa kuja dsm lakini nayo ikaliwa, nikatulia kimya kama miezi miwili akanitafuta na kunieleza kuwa ile pesa ilitumika kumtibu mama yake kwa hiyo anaomba samahani, nikatuma tena tshs80, 000/=akasafirishwa kijana hadi dsm mpaka ss niko nae home anaendelea na masomo, mida mingine huwa tunavumilia mengi ila baadhi ya wanawake huwa wanajiwahi kulaumu tu bila kujua kuwa chanzo cha matatizo mengine husababisha wao.
 
Labda ni kweli tuliozaa kabla ya ndoa sisi ni malaya ila basi hata uliolala nao kabla ya nsoa ni malaya vile vile na wew pia upo kundi hilo la hao malaya.
ulivyonijibu kiustaarabu, naomba tu niseme pole na samahani. anyway, unaonekana ni mtu mstaarabu, nilikuwa nakubip ili nikusome picha wewe ni mtu wa aina gani, ulionewa au ulionea...nimepata jibu wewe ni mtu mtaarabu na huyo jamaa anatakiwa kutunza mtoto. nakuheshimu.
 
Back
Top Bottom