Lovery
JF-Expert Member
- Aug 15, 2014
- 1,602
- 3,418
Na mimba mnazobeba bila shaka ni za mashetani. So sadkweli kabisa mkuu mwenyewe najikusanya kabisa kabla sijapiga tukio akitoa fine ni kama bonus tu ila mwanaume sio wa kutegemea kabisa baba yao shetani
Ubarikiwe wew umemaliza kila kitu hasipokuelewa basiWe dada ningekuona ningekwambia uache kulilia maziwa yaliyomwagika. Ukijikuta kwenye hali kama hiyo kitu cha kwanza unajisamehe upuuzi uliofanya kisha unajipanga kuanza kutembea njia mpya. Usitafute tu mtu wa kumlaumu kana kwamba wewe hukuvurunda. Huyo mwanaume msamehe, muache aendelee na maisha yake. Ukikaa kumfikiria utakuwa unapalilia hasira, uchungu na kinyongo. Mhanga wa kwanza wa hicho kisirani ni mtoto wako. Mzazi mwenye mizigo moyoni hawezi kutoa nuru kwa mwanae. Kwa faida yako na mtoto wako kubali kuwa mko wawili ujipange ufurahie maisha.
Unaweza usielewe nikikwambia ushukuru huyo mwanaume kaondoka. Watu wengine wanakuja kwenye maisha yetu kwa kusudi fulani na kuondoka. Utakuja kuelewa baadae sana kwa nini hili limetokea hivi kama tu utatulia. Ingawa Obama hakukataliwa na babake, kutengana na baba yake na kulelewa marekani na mama na bibi zake ndo kulimpeleka kuwa Rais wa kihistoria Marekani. Baba yake aliporudi Kenya aliishia kwenye ulevi na baadae kufa. Sasa angekuwa amerudi Kenya na Barak sidhani kama Barak wa leo angekuwa hata mwenyekiti wa serikali ya mtaa huko Kenya. Hata huyo Diamond sidhani kama baba yake angekubali bibi Sandra kumpeleka diamond kwenye matamasha na mashindano ya muziki usiku.
Mifano ya watu waliotelekezwa na wazazi na kutelekezwa kwao kukawa ndo njia ya mafanikio ni wengi. Tanzania wapo na dunia nzima. Kuwa single parent mwenye matumaini na bidii kama mama wa Dr Ben Carsons. Badala ya kuwaza mwanaume aliyekuacha waza utakavyomtoa mwanao. Huyu mama katika umaskini wake aliweza kutoa mtoto mcha Mungu, mnyenyekevu, mwenye bidii, daktari bingwa duniani wa upasuaji wa mishipa ya fahamu na vingine ongezea.
Kuna baba anaitwa Chris Gardner ambaye kisa chake kilitengeneza movie ya "pursuit of happyness". Huyu alitelekezwa na baba yake na akanyanyaswa na baba wa kambo, na yeye akaja kuzaa kabla ya ndoa na akaachiwa mtoto wa chini ya miaka miwili akiwa hana ajira. Alikataa kulaumu kama wewe. Akakomaa na mwanae - kulala nae kwenye magari mabovu, stendi, kanisani mpaka kikaja kueleweka. Ni milionea aliyeacha biashara na sasa anazunguka dunia kuwatia moyo watu kama wewe na wanaume wanaokimbia watoto. Maisha yale yale ya kutelekezwa ndo yalimfanya akawa baba bora na mmoja wa wanaume waliofanikiwa duniani. Kwa hiyo kukata tamaa au kuvaa ujasiri na kufurahia au kuombelezea hayo maisha yako mapya ni chaguo lako. Amua unataka nini. Mungu huwa si mchoyo. Ukivurunda ukakubali na kumrudia anakupa nafasi ya pili na ya tatu na ya nne.
Mkuu hongera sana, wanawake wachache sana wana akili kama yako, ulichozungumza hapa ndio hali halisi ya maisha ya kitanzania. Bila wanawake kubadilika hili jambo litadumu daima.wanawake wengi tunaachia tupate mimba kwa sababu mbalimbali.wengi tunategesha mimba ili kuolewa,wengine tunategesha kwa mwanaume wenye hela tukidhan kuwa nikizaa nae ndo nitakula hela yake vizur.wengine umri umeenda anaamua kuzaa na mwanaume yeyote ilimradi naye apate mtoto wake.kwa wale waopata mimba kwa bila malengo wengi wao huwa niwale wanafunzi wenye umri mdogo ambao hawajui kujikinga.migogoro yote ya kuachiwa mtoto inatokea baada ya malengo ya kupata mimba hiyo kutotimia.wanaume wengi wanapenda raha ya kavukavu lakini wakisikia mimba kwaheri,wako radhi wamchukue mtoto akalelewe na mkewe au mama yake kuliko kumpa mtu aliye zaa nae hela ya matunzo kwa kuwa anajua akitoa hiyo hela na wewe mama mtu utakula hiyo hiyo.jambo lingine kunawanaume wengine wako tayar kuhudumia lakini hayo matumizi yanayoomba kwa ajili ya mtoto ni makumbwa kuliko hata matumizi ya nyumbani kwake na familia yake yenye idadi kubwa ya watu,yaani tunakuwa kama tunawakomesha wanaume kwa kudai matumizi makubwa mwisho wake wanaamua kukimbia au kukana watoto.tujirekebishe tukijiachia kupata mimba tujiandae na kulea na kumtunza mtoto.tusifanye mtoto kama kitega uchumi.hii itatusaidia kupunguza strees,nakuishi kwa amani.
Tutamlea pamoja sawa ana miaka mingapi nowNa kweli nimejifunza.
Hongera sana kwa kumpata mwanao na kumuendeleza kielimu, mkasa wako umefanana na wangu kwa 99% matukio yote na mkoa husika, dahNakubaliana na ww 100%, lilishawahi kunitokea, mwanamke niliekuwa nae kwenye mahusiano bahati mbaya alipata ujauzito wang, nikakubali kugharamia ujauzito mpaka anajifungua mwaka 2002 kila mwezi nilikuwa natoa tshs50, 000/=, baada ya kujifungua ndo mtihani ulipoanza, ukituma tshs100, 000/= baada ya siku tatu unaambiwa hela imeisha, ukihoji imetumika vp anakuwa mkali kwelikweli, ukumbuke mwaka 2003 tshs100, 000/= ilikuwa ni pesa kubwa unaweza nunua kiwanja au shamba, ikafikia kipindi nikamwambia siwezi ongeza pesaila nitatuma hiyohiyo tshs 100,000/= mungu wangu nilichambwa balaa, "kati ya wanaume na ww unajiona mwanaume? kwanza mtoto sio wako", hiyo kauli iliniuma nikaamua kusitisha utoaji wa pesa, ndo matusi yakazidi mi kimyaa sijibu chochote, ikapita miaka10 nikapata taarifa kuwa mwanao anapata shida sana kijijini analima vibarua ndo apate kula, dah roho ikaniuma sana nikajiuliza mmm niko dsm nafanya kazi, naishi vizuri, nakula vizuri naishi kwangu inakuwaje mwanangu apate shida? nikalianzisha sekeseke la kudai mtoto lakini mama mtoto mkali balaa, nikapiga mkwara kama ni mwanangu kweli namhitaji vinginevyo akipata tatizo usinihusishe kwa lolote, akakaa akajifikiria mwisho akasema tuma nauri nikuletee mwanao, nikatuma tshs80000/=toka iringa kuja dsm lakini nayo ikaliwa, nikatulia kimya kama miezi miwili akanitafuta na kunieleza kuwa ile pesa ilitumika kumtibu mama yake kwa hiyo anaomba samahani, nikatuma tena tshs80, 000/=akasafirishwa kijana hadi dsm mpaka ss niko nae home anaendelea na masomo, mida mingine huwa tunavumilia mengi ila baadhi ya wanawake huwa wanajiwahi kulaumu tu bila kujua kuwa chanzo cha matatizo mengine husababisha wao.
Relax sawa kubali kuanza upya ondoa vinyongo na uchungu amini ulifanya maamuzi sahihi kulea mimbaMiezi mitatu.
Inauma sanaunahangaika Na mtoto unatoa matunzo ila anamfundisha mtoto kukuona kama umemtelekeza. Akinamama acha kutumia watoto kama kinga
Jipe moyo mkuu dadaangu, Mungu wetu si kipofu anayaona yote unayo pitia na usipo zimia moyo baraka zinakujia kupitia Huyo mtoto. Baba angu alimkimbia mamaangu 1985 akiwa na mimba ya miezi 2 ambae ndo mimi, amekuja kututafuta 2016 nikiwa na miaka 30, nikiwa na degree alontaftia mamaangu kwa kuuza vitumbua na Mungu akanipa kazi serikalini sasa tunaponda raha na mamaangu.Nimemsamehe toka rohoni ila moyo wangu umeshindwa kabisaa kumthamini, kila nkitaka nimtumie pesa ghafla mawazo yanahamia kwa rafiki angu kipenzi mama nahela inatumwa kwake na nataftia na nyingine.Maisha yamemchapa kweli ila sijabahatika kumuoneo huruma. Kila nkijitahidi kumuonea huruma, huruma hazinijii kabisaaa!! Chamsingi dadaangu chakalika umlee mwanao na Mungu atakulea wewe!Nikiwa kama mhanga wa mwanamke alieachiwa matunzo ya mtoto bila msaada wa baba naumia sana.
Hivi wanaume huwa mnawaza nini mnapotupa adhabu ya kulea watoto peke yetu na wewe baba ukiwa hai na unajiweza? Hata kama hujiwezi basi kumjali mtoto wako japo kwa kuulizia maendeleo yake mtu anashindwa kabisa. Hivi kina kaka mmejiuliza nyie baba zenu wangewakimbia mngekuwa wapi sasa hivi? Mnajua ni chuki gani mnaweka kwa watoto wenu mliowakataa? Mnajua ni laana gani mnapata kwa Mungu kwa kukataa kutimiza wajibu wenu kama wazazi? Au mnatukomoa kwa sababu mama hawezi kumuacha mtoto wake nyuma hata apate tatizo gani? Labda wewe na mama wa mtoto hamko sawa lakini ile hasira ya ninyi kutokua sawa baba usimkomeshe mama kwa kuacha kumtunza mwanao ukijua unamkomoa mama, pale unaemkomoa ni mtoto wako ambae ulimtafuta kwa mapenzi/tamaa zako mwenyewe.
Naandika nikiwa na uchungu mwingi sana moyoni. Mwanaume usiemtunza mwanao ona aibu na muogope Mungu wako kwa kitendo unachokifanya.
Jiulize ingekua ni dada yako au mwanao ameachwa na mwanaume alee mtoto peke yake ungejisikiaje?
KARMA IS A BITCH. Ukinifanyia mimi leo wakati unao dada na watoto wa kike jua itakuumiza na wew kwa mmoja kati ya hao kufanyiwa kama unavyofanyia wengine.
Baba mtoto wangu nimeshamlilia Mungu juu yako na nina hakika huyu mtoto ulieniachia nimlee peke yangu atanifuta machozi siku moja na utatamani akutambue kama baba yake utakua umeshachelewa.
Kaka/baba zangu baba Diamond akawe mfano kwenu, Obama aliekataliwa na baba yake mwishoni alikuja kuwa Rais wa marekani/dunia.
Hongera kwa kushinda hilo jaribu la kutotoaWakati tunaanza alinipa story za uongo kabisa kuhusu uhusiano wake uliopita. Ila baada ya kubeba ujauzito ndio nilimjua vizuri hasa baada ya kunisisitiza nitoe. Alikua na mwanamke mwingine ndo maana alisisitiza nitoe na hata sasa hivi hataki kunisaidia sababu huyo mwanamke ameshaujua ukweli kuwa mwanaume wake amezaa nje. Ila hata kama angekua na ndoa bado ni makosa yake kunidanganya alee mtoto.
like how yani?????? asee kweli one can never understand the situation had imtokee...labda ikintokea ndo ntaelewa...
Hahahahaa.. Tatizo mnapenda mizigo ila kulea hamtaki.
Inavyoonyesha ulimtesa sana huyo mwanaume just imagine unafikia wakati kumweleza mtoto kuwa baba yake alikufa! JirekebisheLabda wanawake wa Tanga wako hivyo. Ila kwa uelewa wangu wanawake wengi wa Tanga huwa wanyeyekevu sana kwa wanaume wao yani mpaka ikatokea akakujibu hivyo jua umemtesa vya kutosha. Mimi sifa yangu kubwa ni kutokusumbuana na mwanaume. Ila kwa baby dady nilivumilia karibia mwaka mzima kwa kuamini atachange. Mpaka nimemtamkia nitamwambia mtoto baba yake alikufa ni kwa sababu niliona hakuna matumaini tena ya baba mtoto kuwa baba wa mwanangu. Nimevumilia mwaka mzima hoping that he will change his mind.
Asante mzigua mwenzangu. Karibu baba wa kambo.
Huyu mtoa mada ni wale wale. Siamini mwanaume anaweza kuitelekeza sperm yake bila maudhi Na kashfa SA wewe si saizi yangu. Una kibamia ambacho hakiwezi kunizalisha etc. Sasa kaishasahau na mashambulizi kwa wingi Mzigua90Inauma sana